Kwamba akionwa aombwe kwa upole ahame nchi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwamba akionwa aombwe kwa upole ahame nchi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Apr 16, 2011.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asubuhi hii Paul Makonda (UVCCM- Moshi Mjini) karudia maneno yake ya jana kupitia ITV lakini kwa msisitizo mpya kuwa RA akionwa popote AOMBWE KWA UPOLE aondoke nchini kwani ndiye chanzo cha ufisadi wote na kwamba ana uhakika kuwa ameshahamisha familia yake na yuko katika mazingira ya kuwa na uraia zaidi ya nchi moja.

  Maswali:

  1. Ndg. Paul hivi mtu akithibitika kuwa amefisadi nchi na kukidhoofisha chama adhabu yake ni kumwomba kwa upole ahame nchini? Yaani huku ndio unasema kuwa wewe na wenzako (UVCCM) mnakwenda si kujivua gamba tu bali kuchuna ngozi?

  2. Ndg. Paul hivi kama una uthibitisho wa mtu kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja ukiwemo wa TZ (wakati huu), umechukuwa hatua gani kumripoti Uhamiaji au Polisi au hata Usalama wa Taifa (maana hatujui makusudi yake) na utupe maelezo hatua gani zimechukuliwa au hazichachukuliwa na ni kwa nini wakati hilo ni kosa la jinai.

  3. Kama leo unaweza kutoka mbele ya TV na kusema huyu ndiye Dowans na madudu yote je unaweza kutuaminisha kuwa yeye mwenyewe tu kama mtu mmoja ndiye alikuwa mbunifu, mpangaji na mtekelezaji wa ufisadi wote kila mahala huko bila usaidizi wa wengine? Na kama unasema uchunguzi unaendelea kuwatafuta wengine, sasa utakamilishaje uchunguzi wako wakati huyu umeshamwomba aondoke!

  Zaidi ya yote, alipouzwa swali kuwa mna mazoea ya kuwa wambea wambea hivi na kutumwa na watu fulani fulani, akajibu straight kuwa hilo analikubali kabisa!!

  Sasa nami nahitimisha kuwa naona nawe kijana Paul umetumwa kuanzisha propoganda za kumtorosha mtuhumiwa lakini hujui kuwa katika karne hii uelewa wa watu uko juu sana.
  Yaani anataka baadaye tukisikia kua jamaa katoweka basi amseme tulishakubaliana kuwa tumwombe atupishe nchini kwetu. Mimi sitakuwa sehemu ya makubaliano hayo ya kipuuzi!

  Mimi natoa taarifa katika vyombo vya usalama popote kuwa mkiwaona Paul na RA msiwaombe chochote wakamateni wakaanze kutoa maelezo yao kuwasaidia Polisi uchunguzi kabla ya kuwafikisha mahakamani waliotufisadi na wale waliozembea kutoa taarifa au kushiriki kuwaficha mafisadi kwa namna moja au nyingine.

  Jamani ni ajabu sana katika karne hii mtu anakwenda mbele ya TV na kuongea aliyoyasema Paul na bado waTZ tuko kimya tu tunashangaa shangaa na kusema kijana huyu shujaa!! n.k

  Kwa nini Mtuhumiwa asikamatwe na vijana kama hawa wenye fast hand infomation wakaisaidia Polisi? Hata wezi wa kuku vijini sijasikia wanaambiwa kuwa waombwe waame kijiji wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake.

  Maelezo yaliyotolewa mbele ya TV na Paul ni MATAMU SANA lakini nasikitika kusema si MAZURI na yanakosa welezi katika kuchambua mambo.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  I once said people dont know Rostam Aziz! so as Makonda!

  Issue za hawa mafisadi ni very complicated , wameshinda kwenye majimbo yao, wanaweza kuhamia vyama vingine na wakashinda tu! wana nguvu ya fedha.

  System ililala , ikawalea, wamekomaa na ina taka kuwaondoa kirahisi rahisi.

  Nchi zingine ikifikia hivi usalama wa taifa wanaingia kazini na kuwa-assasinate hawa watu.Maisha yanaendelea

  what happening here is that akina MAKONDA wote ni tima za akina RA kwa umakini mkubwa wanawadanganya watu.

  Aondoke nchini anajua RA anamadeni kwenye mabenki mangapi? mtu ana makosa , jela, otherwise shu-up!
   
 3. s

  smz JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Makonda nilidhani ana ujasiri wa kusema na kusuggest solution zenye mashiko. Lakini nimekuja kugundua ni shallow minded person. Huwezi kusema huyu ni fisadi namba moja halafu ukaja na solution ya kusema Tumwombe kwa upole atupishe nchini kwetu. Upuuzi mtupu. Yaani kwa lugha nyingine akatumalize kabisa.

  Kwani hiyo RA yuko juu ya sheria? na hawa waliojivua magamba wanasema wamewapa siku 90 wajipime na wachukue maamuzi sahihi maana yake nini?? Siku zote 90 za nini, wape siku saba na infact uwaambie na cha kufanya, kama ni kurudisha kadi sema hivyo, na uende mbele zaidi kuwa wasipofanya hivyo utawachukulia hatua gani, siyo kuwapa option.

  Kweli nimeamini RA anatisha.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Wakuu mmesahau ya JK na EPA aliwaambia warudishe pesa then hakuna kilichotokea na eeeti pesa imerudishwa na imepelekwa kwenye ruzuku ya kilimo tukatulia tu! sasa mlitaka huyu mtoto wamafisadi asemeje wakuu! mnampa mwenjenu wakati mgumu saana!
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...and that is the whole Point of the matter. Hii ni comedy tu. Nitawashangaa sana watanzania wa CCM wakiandamana mchana wa jua kali ati kuunga mkono kujivua Gamba!
  Haiwezekani mwanachama mtukutu anayeleta tafrani ndani ya Chama bado uamuzi wa kujitoa kwenye Chama uwe juu yake na sio juu ya Uongozi wa Chama. Hii ina tofauti gani na yale ya Mwenyekiti wao kuwa na Orodha ya Majizi na wavuta unga lakini anawapa MUDA WA KUJIREKEBISHA!
  Kama hawa Mafisadi walikuwa kweli walikuwa wanakichafua Chama huwezi tena ukawapa Miezi Mitatu ya kuendelea kukichafua Chama! Ni hapo hapo wanarudisha kadi ya Chama na kisha kutupwa nje kwenye giza la kilio na kusaga meno! this is just another comedy from our Msanii, nothing less.
   
 6. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Aombwe kwa upole nini? Huyu ni wa jela tu.
   
 7. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Code:
  Kwani hiyo RA yuko juu ya sheria? na hawa waliojivua magamba wanasema wamewapa siku 90 wajipime na wachukue maamuzi sahihi maana yake nini?? Siku zote 90 za nini, wape siku saba na infact uwaambie na cha kufanya, kama ni kurudisha kadi sema hivyo, na uende mbele zaidi kuwa wasipofanya hivyo utawachukulia hatua gani, siyo kuwapa option.
  SMZ, asante.Hayo ni maneno ya mtu mwenye uelewa wa taratibu ziongozazo na uchungu wa nchi yake na si kama yale tuliyosikia leo ya mtu kujiwahi asubuhi kwenye TV na kutupakulia chakula kitamu lakini hatari kwa afya zetu!
   
 8. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Who is Makonda in this country by the way? Is that small boy of uvccm?
  Mwenyekiti wake wa chama anasemaje kuhusu RA?
  Yeye ndo kamtuma amwambie RA aondoke au katumwa na watu wengine wanaotaka urais 2015?
  Nitakuwa mtu wa mwisho kuuona ushujaa wa makonda kwani nawajua ccm..
   
Loading...