Kwako Zungu, Waziri wa Mazingira

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,506
51,111
Nichukue fursa hii kukupongeza kwa kuteukiwa kuwa Waziri. Ama hakika Wizara uliyoteuliwa ni Wizara nyeti mno, maana maamuzi na sera za wizara yako zina athari si kwa binadamu tu bali viumbe mbalimbali wanyama, mimea, ndege, wadudu, miti nk.

Baada ya hayo naona nije sasa katika dhumuni la kukuandikia huu uzi hapa JF. Mheshimiwa ningependa kukueleza haya yafuatayo ili uyafanyie kazi.

1. La kwanza mifuko ya plastic imeanza kurudi tena kinyemela.

Katika hili watu wanaokwenda.masokoni, magengeni kununua bidhaa watakuwa ni mashahidi. Vipo vimifuko vidogo, vya plastic nyeupe vinatumika.

Binafsi nilifurahishwa sana na operesheni ya kuzuia mifuko ya plastic. Kama kuna jambo jema na la muhimu sana ambalo serikali ya awamu hii imefanya ni kwenye kuzuia mifuko ya plastic. Nakuasa kuwa endeleza juhudi hizi, plastic ni adui mkubwa kabisa wa mazingira. Hakikisha mifuko ya plastic inatokomea kabisa, usiache leeway hata kidogo!

2. Dar es salaam inanuka

Mheshimiwa, pindi ukishuka kwa ndege Dar es salaam kutoka nje ya nchi, hsikuchukui muda baada ya kutoka airport kuanza kusikia hili jiji linavyonuka. Hii ni aibu kubwa sana kwetu kama binadamu, na ni miongoni mwa sababu ambazo wageni wanatuona kama SHITHOLE.

Unukaji huu wa Dar es salaam ni real, wala siweki chumvi. Pita. mitaani utaona chemba za mavi zinazovuja, utaona uvundo mkali mweuzi wa matope ya mvua iliyopita, utaona kona za kuta zilizokojolewa na wapita njia, Yaani mheshimiwa Jiji la Dar es salaam. linanuka vibaya mno, Fanya namna la sivyo hao watalii watakaokuja nchini watarudi na sifa mbaya za huu mji na kutushangaa tunaoishi katika mji unsonuka namna hii.

3. Uchimbaji madini na uharibifu wa mazingira

Wachimbaji madini wanachakata madini kwa kuyaoshea na kemikali wanazoziingiza kwenye vyanzo vya maji kama vile mito, mito inatiririsha maji hadi kwenye ziwa au bahari, Samaki wanakula vyakula kwenye maji yaliyo contaminated, kisha wananchi tunakula samaki hao. Hii inaweza kupelekea hatari kubwa sana ya maradhi ya kansa, au kufikia hatua hafa nchi za ulaya zinazonunua samaki wetu na kutuingizia fedha nyingi za. kigeni kusitisha ununuzi huo. Hii ni hatari sana. Nakushauri hili ulifanyie kazi

4. Tatizo la taka bado ni kubwa

Zipo aina nyingi za taka, disposable na non disposable, hizi taka zikichanganyika jata ufanisi wa kuzidispose ni mgumu sana. Nilikuwa nasoma kwenye mtandao namna wachina wanavyodeal na tatizo hili. Katika jiji la shanghai, serikalinya mji imepitisha sheria ya kutenganisha taka, kila kwenye dustibins basi zinawekwa dustibins za aina mbili, moja ni kwa ajili ya non disposable materials nyingine ni kwa ajili disposable materials, raia wamefundishwa kutupa taka husika katika dustbin husika ili kurahisisha uchakataji baadae, masna kiukweli mtu anayetupa let say maganda ya ndizi na chupa ya maji kwenye dustbin moja anafanya mchakato wa kutreat hizi taka kuwa mgumu sana.

5. Sewage systems ni janga

Almost nchi nzima haina sewage system ya kuridhidha, matokeo yake watu wanachimba vyoo na kuvitumia huku hali hiyo ikihatarisha afya zao pindi. mvua zikinyesha vinyesi vinatoa na kwenda na. maji ya mvua mitaani, Wakati. mwingine mabomba ya maji yanapita karibu na vyoo hivyo na hivyo kama vina leakage kidogo vinapelekea contamination ya maji hayo na ni hatari. mno kwa watu. Sasa katika vitu vya msingi unavyopaswa kufanya ni kutafuta namna ya kupata fedha ili kusuka hizi sewage systems hususan za miji mikubwa, la sivyo haya ni majanga makubwa

6. Mheshimiwa miji yetu haina bustani za kutosha/parks

Na hii ni aibu nyingine, hebu nenda kwenye majiji makubwa kama vile Jo'berg, Ports Elizabeth, Tokyo, Shanghai, angalia mabustani kibao yaliyopo kwenye miji hiyo, sisi huku kwetu tunambwelambwela tu. Mheshimiwa hebu anzisha mabustani makubwa katika miji yetu. Nilikuwa naangalia ni sehemu gani zilizo green hapa DSM, may be ni Gymkhana wasipoenda waswahiii, Ikulu, UDSM mlimani kidogo, wapi pengine? Mheshimiwa tengeneza parks za maana

Baada ya hayo nakutakia mema kwenye ujenzi wa taifa

Ni mimi Missile of the Nation Kombora hatari sana la Ulinzi wa Taifa
 
Kwenye jimbo lake tu pale Ilala ni hatari tupu, Madimbwi kila kona,harufu kama kawaida.
Pita Soko la Ilala ni kuchafu hatari ,alafu inyeshe Mvua daah ni balaa.
 
Kwenye jimbo lake tu pale Ilala ni hatari tupu, Madimbwi kila kona,harufu kama kawaida.
Pita Soko la Ilala ni kuchafu hatari ,alafu inyeshe Mvua daah ni balaa.

Sijui tunafeli wapi, ndo maana tunaitwa SHITHOLE countries, miji yetu INANUKA, huo ni ukweli mchungu
 
Tuna tatizo viongozi wetu wengi siku hizi hawaoni umuhimu wa kuacha legacy.

Ni kitu kikubwa na kinaacha heshima ya milele kwa kiongozi husika hata baada ya kustaafu au kufariki. Atakumbukwa tu.

Zungu achague mojawapo kati ya hayo iwe legacy yake. Asikubali kuondoka hivi hivi.
 
Back
Top Bottom