Newbies
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 1,477
- 2,148
Mhe. Tundu Lissu nakusalimu.
Wewe ni miongoni wa watanzania wanaotetea sana lugha ya Kingereza pengine pasipo kujua kuwa lugha ni uchumi na inafungamana na mielekeo, tamaduni na falsafa za watumiaji wa lugha hiyo (Prof Clara Momanyi Kenyatta University)
Hivyo unapoendeleza lugha ya kigeni (Kingereza ) maana yake unakuwa unawanufaisha wale wenye lugha hiyo.
Ndio maana wao wana mashirika yenye nguvu na hufanya uwekezaji mkubwa kwaajili ya kuendeleza lugha yao wakilenga kujinufaisha kiuchumi.
- Tunapaswa kuelewa kwamba hakuna nchi yeyote yenye maendeleo ya kweli inayotumia lugha ya watu wengine (Prof Aldin Mutembei Udsm)
Unayajua Haya ?
- Sera ya lugha inasemaje? (Tz)
Mwaka 2014 Sera ilipitishwa kuwa kiswahili pamoja na Kingereza zitakuwa lugha za kufundishia kutoka shule za awali mpaka chuo kikuu. (Haijatekelezwa)
- Tafiti zinasemaje?
Tafiti zote zilizofanywa zinaeleza kuwa lugha inayoweza kuwapa watanzania maarifa na wao wakawa wavumbuzi ni lugha ya kiswahili. (Rejea utafiti wa Mzee Makweta (1991)
- Kiswahili kinaweza kutumika kufundishia katika miktadha yote ya Academia?
Jibu ni Ndio kutokana na tafiti zilizofanywa! Utasema hakuna vitabu au publication na makorokocho mengine yameandikwa kwa Kingereza lakini hapa tafsiri inaweza kutumika na nimiongoni mwa Kazi za BAKITA &TATAKI kama vilivyotafsiriwa vitabu ya sayansi vya Hubort na Lambert mwaka 1972 ) na kama walivyotafsiri mataifa mengine kama ujerumani uingereza maarifa kutoka katika lugha ya kiyunani na kiarabu.
NB natambua umuhimu wa kingereza lakini ushauri wangu kwako, asaa sudi utakuwa Rais , lugha hii inaweza kufundishwa shuleni katika ngazi zote kama kozi na sio kama somo kama inavyofanyika sasa na ikiwezekana watafutwe waalimu wazawa wa lugha hiyo. Huku kiswahili kikitumika kufundishia masomo mengine. Watanzania wote hakuna anayejua kingereza hata hao wanaojinasibu kukijua wanakijua kwa uchache sana pengine katika kiwango cha 3.0 ,( Lugha sio msamiati pekee )
Kukicha nitaendea
#mawazohuru