Kwako Seleman Jafo

Mkyamise

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
455
557
Hongera kwa majukumu yako ya kila siku.

Najua unapitapita humu jukwaani. Kuna jambo la kimazingira ambalo pengine halisemwi ila lipo katika maisha yetu ya kila siku. Jambo lenyewe limetoa ajira kwa watu wengi ila ni hatari kwa mazingira yetu.

Jambo lenyewe ni namna bora ya uteketezaji wa vioo vinavyotumika kwenye madirisha au milango ya aluminium. Katika hali ya kawaida vipo vipande vipande vingi vinavyobaki kwenye ukataji wa vioo hivi. Ukipita kwenye maeneo madirisha haya au milango hii inapotengenezwa utashuhudia hili.

Cha kushangaza maeneo mengi utakuta vipande vipande hivi vinatupwa majalalani. Je, kuna sera ipi ya uteketezaji au ufuatiliaji wa jambo hili?

Vipande hivi kwa uelewa wangu ninadhani ni miongoni mwa taka hatarishi (Hazardous waste).

Maeneo mengi hasa katika level za wilaya sidhani kama kuna ufuatiliaji wa namna ya kuteketeza au kurejeleza (recycling).

Nikushauri kwamba kabla hatujafikia hali mbaya ni vyema elimu ikatolewa kwa mafundi husika, maafisa mazingira, maafisa afya, n.k.

Ili yasije kutufika ya mifuko ya plastiki maana vioo haviozi kirahisi. Kuwe na utaratibu wa ukusanyaji wa vipande hivi ili kuvirejeleza au kuviteketeza kwa namna inayofaa.

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom