Kwako Roma Mkatoliki Part 2

kinondoniilala

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
988
762
Nakusalimia kwa mara nyingine Roma Mkatoliki popote ulipo

Naendelea kukumbusha mambo muhimu ya kuzingatia katika kipindi hiki.

1. Nakukumbusha kuzingatia mawasiliano yako ya simu unayofanya, katika hili naomba utambue kwamba mawasiliano yako yataanza kudukuliwa kupitia namba zako za simu ulizosajili kwa majina yako.

Uzingatie texts na maongezi utakayoyafanya, nakushauri badilisha line za simu zako zisomeke kwa namba za nje, chukua hata line ya Safaricom kutoka Kenya uwe unatumia.

2. Naomba ujiandae kisaikolojia katika hili la kufuatiliwa kila uendapo, katika hili itabidi uwe mpole na usiwe ni mtu wa hasira ingawa kufuatiliwa ni jambo linalokera sana kwa sababu linaondoa privacy yako ya kuweza kukutana hata na mchepuko, lakini katika hili jitahidi kuwa makini kutokuwa mtu wa jazba wala hasira.

3. Kuna tabia zitakukera hususani za kukuna vichwa kwa watu usiowatambua wala hawajulikani pia watakuwa busy sana na kuchati na simu zao lakini kwa kuwa wanatumia mkondo wa juu sana wa sms ambao hauwezi kudukuliwa, hali hii nakushauri uichukulie kawaida, tafadhali chonde chonde usichukie na usiwe na hasira wala jazba.

4. Wasanii wenzako kuwa nao makini kuanzia hapo studio unaposhinda siku nzima hadi katika festivals mbalimbali ndani na nje ya nchi, jitahidi kuwa nao makini, hususani katika vinywaji unavyotumia na chakula unachokula, kwa sababu baadhi ya hao wasanii ni undercover, na watakuwa wapo kazini pindi watakapokuwa na wewe.

5. Don't trust anyone, who come to your way. Trust will kill you so be careful.

Naomba kuwasilisha kwa siku ya leo.
 
hakuna wa kuhangaika naye huyo ni msanii ametumia uhuru wake wa kikatiba. Hajatukana mtu.

na siku zote nawaambia kosoa kwa staha ama kisanii zaidi sio kama zuzu.
 
hakuna wa kuhangaika naye huyo ni msanii ametumia uhuru wake wa kikatiba. Hajatukana mtu.

na siku zote nawaambia kosoa kwa staha ama kisanii zaidi sio kama zuzu.
Hata TL alikua ni mbunge akitumia haki yake ya kikatiba kutoa hoja na maoni yake Bungeni lakini yakamkuta ya kumkuta, so tahadhari ni muhimu
 
Kila ufanyalo ni lazima utafakari na uwe tayari kulipia gharama.
 
Back
Top Bottom