Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,633
- 29,506
Kwako Mkuu wa Mkoa,
"Other tings kept constant", kwa hili la Kuwaomba Wachina watujengee uwanja wa Michezo na wakakubali nakupongeza sana, maana mpira wa miguu ni sehemu ya burudani na ajira ya vijana wengi.
Niende kwenye Point moja kwa moja, ule uwanja ambao mumeweka jiwe la msingi pale Temeke ni Uwanja wa Chuo Cha Bandari, sijajua hasa huu msada uliouomba wewe kama RC mwishowe umiliki wa ule uwanja utakuaje, Ni Mamlaka yako na Ya Bandari kwa pamoja au utaendelea kubaki chini ya Chuo Cha Bandari.
Msaada inasemekana ni wa US$ 450,000 x Tshs 2,222/$ = Tshs 1,000,000,000/= (Tshs 1 Billion). Hizi ni hela nyingi sana kwa ukarabati au ujenzi kama zikisimamiwa vizuri. Hata kama hazitotosha lakini Kwa uwezo wa Kuchangisha misaada nina uhakika unaweza kuchangisha tukapata Uwanja Mpya kuliko kukarabati viwanja vya watu.
Mimi Ushauri wangu kwakua umesema utaendelea na zile heka 1,500 za bwana Iqbal basi ni vyema Uwanja huu mpya ukajengwa pale. Hii ni kwa sababu Lile eneo ni kubwa sana, pakitumiwa vizuri pale hata eneo la Parking za Magari litapatikana kuliko kwenda kubanana Bandari. Uwanja Mkubwa wa maana na parking zake sizadhani kama utachukua hata heka 20 (1.3% only ya heka 1,500)
Pili Temeke tayari kuna Viwanja vikubwa tu vya kimataifa kama Uwanja Mkuu wa Taifa, Shamba la Bibi na Chamanzi. Kuendelea kukarabati Bandari kiwe cha kimataifa labda ni kama upendeleo tu. Kwa Wilaya nzima ya Kigamboni sijaona Uwanja wa Maana, so pakijengwa Uwanja Mpya pale itasaidia pia,
Tatu ni kuhamasisha Soccer katika Wilaya hii Mpya. Kigamboni mwanzo ilikua chini ya Temeke, sasa inajitegemea hivyo inahitaji kujijenga sasa. Uwepo wa Huu Uwanja utaongeza hamasa ya soccer kwa wakazi wa Wilaya hii mpya.
Ni hayo tu Ndugu RC.