Ni wazi kuwa wenye ujasiri wa kuandika nyuzi kama hizi kwa maslahi ya taifa ndani ya vitisho vilivyopo si wengi, hivyo tafadhalini msiwe sehemu ya kuwanyamazisha.
Wanasema nani mwenye kumfunga paka kengele? Ni muhimu sasa bila ya kupoteza muda zaidi wala kumung'unya maneno, tumfunge paka huyu kengele vinginevyo twafa tukijiona.
Wenye ujasiri wamejitahidi kuweka jitihada binafsi kuwahami wananchi.
Heko baba askofu Niwemugizi. Pongezi anazoendelea kuzipata baba askofu huyu ni wazi kuwa hatua za namna hii ndizo zilizokuwa zikihitajika kwa muda sasa.
Mh. Rais tafadhali tuachane na mambo ya uchumi na siasa. Ugonjwa huu utamaliza watu kwa uzembe wenu.
Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita.
Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukishughulikia suala hili tangia mwanzoni wewe kama mtendaji mkuu imetugharimu kweli kweli. Hatukuweza kuuzuia ugonjwa
huu kuingia nchini, na wala hatukumwona hata mmoja katika safu zako aliyewajibishwa au kuwajibika.
Umekuwa ukilishughulikia suala hili kuuzuia ugonjwa huu kusambaa na bado ugonjwa unasambaa. Hatujamwona hata mmoja katika safu yenu aliyewajibishwa au hata kuwajibika.
Kwa mwendelezo huu ni wazi kuwa hatunayo nia ya dhati (seriousness) wala hatuchukulii umuhimu wowote mafanikio
au kushindwa katika vita hivi nyeti ambavyo hakuna taifa hata moja duniani lenye watu makini waliojaribu kuidunisha.
Kwa sababu ugonjwa huu unaenda kutuathiri kimaisha moja kwa moja (sisi na wapendwa wetu), kwa vile wawakilishi wetu labda hawakufikishii maoni yetu vilivyo, na kwamba eti wewe huyaoni haya, tunaomba kutumia maneno yako wewe mwenyewe:
"Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukiendesha vita vya ugonjwa huu, tafadhali sasa NO!
Tunakupenda sana mheshimiwa. Lakini mheshimiwa kwenye hili la Corona, big No!
Kwa nini angalau Dar na Zanzibar haziko locked down? Mh. rais, Big No! Tumevumilia kweli kweli hadi tumelazimika kukupa ukweli huu. Mkuu big No!"
Cha kufanya kinafahamika. Kenya Rwanda na Uganda walio kama sisi wamefanya nini na sasa wanaudhibiti juu ya ugonjwa huu na karibu wanaanza kurejea kwenye shughuli zao za kawaida?
Please, Big NO!