kwako mhe Nahodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwako mhe Nahodha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nyandulu, Jan 22, 2012.

 1. n

  nyandulu Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAHODHA FANYA KAZI ILA USISIKILIZE MAJUNGU
  Kwa hivi karibuni waziri wa mambo ya ndani ya Nchi MHE Shamsi Vuai Nahodha ameamua kuimrika idara ya uhamiaji nchini kwa kiasi kikubwa na kulingana na unyeti wa idara hiyo, inabidi watumishi wake wote wazingatie maadili. Waziri kwa sasa amehaidi kuisambalatisha safu ya viongozi makao makuu, kwa hili sina shida nalo endapo kama waziri ana uhakika safu nyingine atakayopanga itakidhi malengo ya kazi anayotarajia Mh Nahodha.
  Katika malalamiko mengi yanayoikabili idara hii ya uhamiaji ni kushindwa kuwadhibiti wahamiaji haramu kuingia nchini hususani wa mataifa ya Ethiopia na Somalia, kwa hiyo matarajio ya waziri ni kwamba safu mpya ya uongozi atakayo panga itamaliza tatizo hili kitu ambacho nina uhakika haitawezekana na waziri atalazimika kuipangua safu hii tena.
  Ni vema ikumbukwe kwamba watumishi wa idara ya uhamiaji ni askari waiopitia mafunzo kama askari polisi ,magereza nk, na hawa wanaambiwa ni walinzi wa mipaka yetu ambao mbali ya kutokuwa na silaha hata kilungu tu hawana je huo ni ulinzi kweli?
  -wahamiaji haramu ni mtandao wa kihalifu wana mbinu mbalimbali, wanapita katika mapori na misitu minene, na baharini je ? huyu askari wa uhamiaji asiye na silaha wala boti na askari wa maji ataweza kudhibiti.
  - Najua ulinzi wa mipaka unahusisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama je wahusika katika vyombo hivyo hawawaoni hawa wahamiaji haramu, jeshi la polisi wanao askari wa doria wenye silaha, pia zipo barrier vizuizi sehemu barabarani na askari polisi wapo je hawwawaoni watu hao wanapopita? Inasemekana wahamiaji haramu wanakuja kwa boti na majahazi kupitia baharini tunao askari jeshi wa doria baharini je hawawaoni? Nilishawahi ambiwa na mtu mmoja kwamba wakati mwingine watu hawa wanapita katikati ya hifadhi zetu zilizoko mpakani huko kuna askari wa wanyama pori kwani hawawaoni , au wao hawana mamlaka ya kuwakamata , kuna nini hapo?
  - kwa hili la wahamiaji haramu hususani wanaotokea mataifa yapembe ya afrika idara ya uhamiaji inapewa zigo isiloliweza,
  Ni vema waziri akarisghulikia hilo kwa umakini kwanza kwa kushirikisha wadau wote wa ulinzi wa mipaka kama JWTZ, polisi, Usalama wa Taifa, Askari wa tanapa na uhamiaji.pia uhamiaji wajengewe uwezo wa mafunzo na vitendea kazi.
  Pili katika ngazi ya kimataifa, ashirikishe nchi wanazo toka , nchi wanazopita, na nchi wanazokwenda, taarifa zisizo rasmi ni kwamba watu hawa hupata hifadhi ya ukimbizi katika nchi ya malawi vile vile Afrika kusini inawatambua kwa kuwapa vibali kufanyia kazi, ushiriki wa nchi hizi katika majadiriano unawezakutoa ufumbuzi wa tatizo hili.
  Waziri pia amelenga kuondoa tatizo la wafanyakazi wa kigeni ambao hawana vibali, pia wale wenye vibali ambao hawakustahili,lawama kubwa bado imeelekezwa katika idara ya uhamiaji, sio kwamba nataka kutetea maovu, nataka tuangalie ukweli , serikali yenyewe haijaiwezesha idara hii kukabiliana na changamoto hiyo, pia haw uhamiaji wameamua kukaa kimya kuna vibali vingi vilivyotolewa kwa watu wasiostahili ambavyo vimetolewa kwa shinikizo la wakubwa serikalini, ni wazi kwamba asilimia kubwa ya vogogo walioko serikalini wana hisa katika makampuni mbali mbali ya kigeni yaliyopo hapa nchini na ndio wa kwanza kwenda uhamiaji kutoa mashinikizo ya kupewa vibali.
  Mbali na hapo sera yetu ya uwekezaji haijaweza kuwabana wawekezaji kutii sheria za nchi hivyo mara nyingi hawa wawekezaji ndio wa kwanza wanao ivuruga idara hii wamekuwa wakiwaajili wafanyakazi wa kigeni bila hata kufuata taratibu, na mara nyingi askari wa uhamiaji wamekuwa wakizuiwa na walinzi magetini wanapotaka kuingia katika makampuni mengi, wanapotaka kukagua, au kucheleweshwa kuingia na wale wageni wanapjificha ndo wao wanaruhisiwa, kama mtakumbuka sakata la Waziri Masha na askari wa Uhamiaji , pia kuna kampuni moja ilishawahi kuzuia kamati ya Bunge kuingia basi kuzuiwa kuingia katika makampuni kwa hawa mnaotegemea wadhibiti wafanyakazi wasio na vibali ni kawaida.
  Kuna makampuni yanataka utoe apointment bila hiyo appointment hugusi ndani, je uhamiaji kama wanaenda kwa appointment unatarjia watakamata mtu.
  -Ni vema idara hii iwezeshwe kwanza kabla ya kutupiwa lawama na viongozi wake kuishi katika hofu ya kungolewa na waziri ni vema ikalaumiwa panapo stahili. Waziri awe fair asifanye kazi kwa majungu na kusililza upande mmoja tu , kazi itamshinda
   
Loading...