Kwako kipenzi changu pennina.....2

Kwako kipenzi changu pennina.....2

yamoyoni mwangu

Senior Member
Joined
Oct 25, 2013
Posts
106
Reaction score
31
Basi bwana
Nakumbuka vizuri july 16 mwaka 1998 mimi pamoja na ndugu wachache walionisindikiza kutoka mwamashimba wilaya ya kwimbwa mkoani mwanza hadi mwanza mjini... tayari kwa safari ya kuelekea masomoni mkoani kigoma kuendelea na kidato cha 5 na 6 katika shule ya sekondari kigoma.. nilitegemea kuondoka kesho yake asubuhi kwa treni hadi tabora... kisha kusafiri tena kwa treni itokayo dar es salam kwenda kigoma.... usiku wa siku hiyohiyo... kabla ya safari yangu mama alinihusia mengi kuhusu maisha magumu niliyoyaacha nyumbani.... kwani nakumbuka ndugu wengi hawakukubaliana na mama mzazi ambaye yeye alitaka mimi nisome mpaka chuo kikuu.... ndugu zangu wengi walishauri badala ya kutumia pesa nyingi kwa ajili ya masomo ya A-level ni bora nigeomba ualimu tuu ili nipate ajira mapema... mama mzazi hakukubaliana na wazo lao.. yeye alisema ataendelea kujitoa kwa moyo wake wote ili niendelee na masomo hayo.....

Baba mzazi alitutelekeza miaka mingi iliyopita... na kwenda kuoa mwanamke mwingine... sababu kubwa ilikuwa ni mimi mwenyewe...baada ya kufaulu kujiunga na seminari ya makoko kwa ajili ya kidato cha kwanza hadi cha nne... baba mzazi alikataa kata kata na kusema hawezi kuuza ng'ombe wake kwani yeye aliamini zaidi katika kilimo na ufugaji yeye suala la elimu hakulipa kipaumbele kabisa... mifano mingi aliyoitoa akasema "ona kijana wa mzee fulani amesoma lakini hawasaidii chochote kwao na wala hajawahi kurudi hapa kijijini.." baada ya kuona mama bado anang'ang'ania tuu ndipo akamua kutuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine kijiji cha jirani.. akauza kila kitu isipokuwa mashamba mawili tu yaliyokuwa na viazi kipindi hicho... huo ndo ukawa mwanzo wa maisha magumu katika familia yetu...

Kabla ya safari yangu... mama alinihusia mengi akanieeza maisha magumu ninayo yaacha nyumbani..., dhiki kubwa ya chakula.. kwani nakumbuka kipindi hicho kilikuwa cha mavuno ya mpunga... mama aliamua kuuza chakula karibia chote ili apate angalau fedha kichele yakunipeleka shuleni... mama akaniambia "najua sasa umeshakuwa mtu mzima... suwezi kukuzuia kuwa na mpenzi.. lakini nakusihi jitahidi sana ujiepushe na masuala hayo kwani wengi wameshindwakufikia mafaniko yao kwa sababu ya mapenzi" mama aliongea mengi akanieleza namna alivyokuwa anauza mbogamboga ili sisi tusome..."mwanangu wewe ndio mkombozi pekee wa familia hii... kasome kwa uchungu... tena jiepushe na marafiki wasiopenda shule... kijiji kizima kinatuangalia sisi na maisha yetu mwanangu usiniangushe...."

"Mama nitajitahidi na nakuahidi nitakwenda salama na nitarudi salama... kwani tulianza na mungu na tutamaliza na mungu" niliongea maneno haya kwa uchungu sana... majira ya mchana nikaanza safari kutoka mwamashimba-kwimba kwa baiskeli hadi mwanza mjini mimi pamoja na ndugu wachahe.. nakumbuka tulifika mwanza jioni sana... katika stesheni ya mwanza kusini nilipaki mzingo yangu na kutafuta kijisehemu nikalala... ndugu wengine walienda kwa ndugu yetu mjomba aliyekuwa anaishi mabatini... usiku mzima sikulala nilikuwa nawaza kwa nini sisi tana maisha magumu kiasi kile.. nikaapa kutamusamehe baba yangu...

Majira ya saa 11 alfajiri tulianza safari kutoka mwanza hadi Tabora... kisha usiku niliendele na safari kwawa treni hadi kigoma kwa tren iliyokuwa inatoka dar es salaam.. asubuhi tuliwasili kigoma... moja kwa moja nikaenda had shuleni pale kigoma.. maisha yangu yalikuwa tofauti sana na wanafunzi wengi pale shuleni.. maisha ya kiseminari kule makoko yaliniathiri sana.. nilkuwa nashangaa sana ninapoana wanafunzi wengine wakiwa wamelewa.... katika maisha yangu nilipenda sana kucheza mpira wa miguu.. kila siku jion nilikuwa nukifanya mazoezi ya mpira pale uwanjani.... nilikuwa golkeper mzuri sana... baada ya mwezi mmoja yalianza mahindano ya UMISSETA...mashindano ya wanafunzi shule za sekondari... baada ya mashindano yale timu ya wilaya ikaandwa huku mimi nikiwa miongoni mwa walinda mlango wa timu hiyo iliyotakiwa kwenda kasulu kwa mashindano ya mkoa.... pale TTC kasulu... basi baada ya wiki moja timu yetu ikaungana na wilaya nyingine pale kasulu....

Siku moja wakati timu yetu ikfanya mazoezi katika uwanja wa sekondari Bogwe... kulikuwa na timu ya mpira wa pete iliyokuwa ikifanya mazoezi karibu na sisi pia.. sikuweza kujua maramoja kuwa timu ile ilikuwa ya wilaya gani... wakati natafakari suala lile.. nikamuona msichana mmoja mrefu alikuwa akieleka pale uwanjani... naomba nikili wazi kuwa katika umri wangu ule sikuwahi kuona binti mzuri kama yule.. licha ya kuwa mrefu mweupe, alikuwa na shingo ndefu kama ya twiga..., alikuwa ana umbo fulani la kike... zuri wakati naendelea kulimwangalia kwa makini... nikasutishwa na kipenga cha mwalimu wetu henjewele.. aliyekuwa anatuuita... baada ya maongezi yale sikuweza kumuona tenaa...

Tukutane ijumaa....

NTAKUKUMBUKA DAIMA KAKA MPENDWA.... REST IN PEACE...mwandishi wa hadithi hii kwa sasa ni marehemu.... tarehe 15/12/2013 atatimiza mwaka mmoja tangu atutoke.....
 
Laiti wanaume tungepewa uvumilivu na subira kama moyo wa mama kwa mwanawe. Nakumbuka nikiwa mdogo sana baada ya Baba kufariki, Wazee wakafanya maisha kuwa magumu sana (si unajua mali a marehemu anapoondoka Baba?) kwa kweli alinyanyasika sana kipindi hiko, Nakumbuka na namuona akilia akisema ''Ngauka iha wanawako ni nacho ewaombera? Ngeka nawo maa kikacha kyi'' (nikiondoka nani atawalea wanangu, nitakaa nao liwalo na liwe) Mungu awabariki wamama wote kwa moyo wa upendo mlionao kwa watoto wenu. Nawaheshimu sana wanawake kwa kweli.
 
Amen Amen.asante kwa kutambua umuhimu wetu
 
mkuu kuna akina mama kweli wabarikiwe duniani mpaka mbinguni.......
 
Ahya tukutane Ijumaa mungu akipenda, ila uirefushe kidogo ipate kuisha mapema
 
Sijui kwa nini mimi mvivu sanna wa kusoma
 
:A S-confused1::A S-confused1:Aseeeee thread ndefu mno!:A S-confused1::A S-confused1:
 
Laiti wanaume tungepewa uvumilivu na subira kama moyo wa mama kwa mwanawe. Nakumbuka nikiwa mdogo sana baada ya Baba kufariki, Wazee wakafanya maisha kuwa magumu sana (si unajua mali a marehemu anapoondoka Baba?) kwa kweli alinyanyasika sana kipindi hiko, Nakumbuka na namuona akilia akisema ''Ngauka iha wanawako ni nacho ewaombera? Ngeka nawo maa kikacha kyi'' (nikiondoka nani atawalea wanangu, nitakaa nao liwalo na liwe) Mungu awabariki wamama wote kwa moyo wa upendo mlionao kwa watoto wenu. Nawaheshimu sana wanawake kwa kweli.

haika mbe! ruwa nakuenenge ngoyo necha usiwaache watoto wako wateseke,,,, ila wamama wa kichagga ni mafighter nawapa hongera kubwa,,,,,
 
Mungu ambariki mama Molembe nakumbuka alivyokuwa anaokota kuni kwenda kuuza kuhakikisha napata mlo na kuninunulie mahitaji muhímu ya shule atakayekugusa nitakufa nae mchana kweupe mungu akulinde akutie nguvu na akupe maisha marefu nina uhakika kupitia mimi maisha unayoishi si haba ila si cha kukulipa mama na siwezi kamwe chíni ya mbingu ninaweza kukulipa ila tu ni kukurudishia fadhila kidogo kwa wema wako, Wabarikiwe wa mama wote ambao wana moyo kama wa mama yangu,AMINA.
 
Last edited by a moderator:
Laiti wanaume tungepewa uvumilivu na subira kama moyo wa mama kwa mwanawe. Nakumbuka nikiwa mdogo sana baada ya Baba kufariki, Wazee wakafanya maisha kuwa magumu sana (si unajua mali a marehemu anapoondoka Baba?) kwa kweli alinyanyasika sana kipindi hiko, Nakumbuka na namuona akilia akisema ''Ngauka iha wanawako ni nacho ewaombera? Ngeka nawo maa kikacha kyi'' (nikiondoka nani atawalea wanangu, nitakaa nao liwalo na liwe) Mungu awabariki wamama wote kwa moyo wa upendo mlionao kwa watoto wenu. Nawaheshimu sana wanawake kwa kweli.

Tunashukuru kwa kweli acha mama aitwe mama
 
Back
Top Bottom