Kwako bwana Amon Mpenja: Sio Kosa kwa asasi zinazotoa misaada ya kisheria kutoa elimu kwa wapiga

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,015
Ndugu wanajanvi,

Nimemsikia naibu katibu mkuu wizara ya sharia na mambo ya katiba bwana Amon Mpenja akiyaasa mashirika ya kiraiya yanayotoa misaada ya kisheria yaache kutoa elimu kwa wapiga kura sijui kosa liko wapi.

Haya yanakuja huku serikali ikiwa imeyabana na kuyanyima fursa ya kufanya hivyo mashirika yenye uwezo mkubwa wa kufanya hivyo.

Tumeshuhudia mashirka kama KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINAADAMU na HUMAN RIGHT DEFENDER yakinyimwa haki ya kutoa elimu kwa mpiga kura kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ule ulionajisiwa.

wapenda haki wote tunajua kwamba watawala wanapenda watu waendelee kuwa wajinga ili wanufaike na ujinga wao. Tunajiuliza kwamba kama kweli uchaguzi ni huru na wa haki kama ule wa Malawi kwanini watu wasipewe elimu ya mpiga kura kadiri inavyowezekana?

kama kweli serikali imeleta maendeleo kwa watu wake kiasi cha kuingia uchumi wa kati huu uoga unatokana na nini hasa. Tulishuhudia figisu kama hizi za mashirika kunyimwa haki ya kutoa elimu kwa mpiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019. matokeo yake kila mpenda haki aliyaona yakitokea. haki za watu zilisiginwa kwa kuchaguliwa viongozi wa mitaa na vijijiji na majuha yakijitapa kwamba nchini kunamaendeleo.

Ndugu mpenja na wanaomtuma wanapaswa watueleze mashirika hayo kutoa elimu kwa mpiga kura wa Tandahimba na Namundu yanafanya au kukiuka sheria gani hasa.

Mmetunyima hata haki ya kuona bunge live huku nyinyi mkimulikwa hata mkienda kwa WAGANGA NA WALOZI kama mlivyofanya huko malawi na kwingine.

mmevinyima vyama haki ya kufanya mikutano nyie mkivaa matambara yenu ya kijani hata mkienda kuzindua shimo moja la choo tena cha msaada wa mabeberu.

Bwana mpenja kumbuka nchi hii wananchi hawatakaa wakiwa wajinga miaka yote wala usijidanganye. pia usijidanganye kwamba CCM inapendwa kiasi cha kufanya ifanyavyo hapana. CCM inasaidiwa na dolatu wala sio kingine.

Ndimi, mwanamageuzi niliyekuwa nakushika mkono tukiwa masomoni UDSM Japo utasema sio mzalendo kwakuwa sikubaliani na wewe.

Asante.
 
Back
Top Bottom