Kwako Ansbert Ngurumo: Mwisho wa zama

Tarishi

Senior Member
May 9, 2008
105
150
Ansbert Ngurumo; mwisho wa zama

Imeandikwa na Maxmilian Alexander

Baada ya aliyekuwa mpika propaganda za Chadema na baadaye Ukawa, Saed Kubenea kuvamia siasa na sasa nazo zimemmeza, mwanahabari mwingine na mnazi wa kambi hiyo anajaribu kuziba nakisi hiyo.

Tofauti na Kubenea, Ansbert Ngurumo ni mwanahabari mahiri na aliyejitahidi kupitapita shule.

Hata hivyo tangu avamie siasa na kushindwa ubunge kupitia Ukawa mwaka 2015, katika kujaribu kujikung'uta vumbi upya ameanza kujipambanua kama mbadala wa Kubenea.

Anajipambanua kwa kutumia kalamu kuwakilisha na kuwasilisha mtazamo wake wa kisiasa na mara nyingi akipinga sera na muelekeo wa Serikali ya Rais Magufuli kwa kuitumia tasnia adhimu ya uandishi wa habari kuipinga Serikali.

Kuipinga Serikali sio tatizo lakini ukweli kwamba Ngurumo anatumia hoja dhaifu na za kipropaganda kuhalalisha mitazamo ya siasa zake ni dhahiri kuwa kunazidi kumshushia heshima yeye na sasa pia anainajisi taaluma ya habari.

Nimesoma andiko lake la wikiendi hii kwa mfano anajifanya kutaka kumsaidia Rais John Pombe Magufuli kwa kumpa ushauri kitu ambacho nàamini Rais kama atausoma atatikisa kichwa na kumwachia mwenyewe.

Ushauri usio na jema hauna jema.Rais aliposema atafanyakazi bila kufuata siasa wala kubanwa na mitazamo ya siasa inaonekana akina Ngurumo bado hawajamwelewa.

Mfano ktk andiko lake hoja zote za Ngurumo ni hoja za Ukawa na hilo sio tatizo.

Sio tatizo kwa sababu,kama mwanasayansi za siasa, siamini kwamba Rais au Serikali haitaki kufanyiakazi hoja za Ukawa, la hasha.Naamini Serikali inapaswa kufanyiakazi hoja zenye tija hata kama zinatoka Ukawa.

Ukiitazama hoja ya kwanza ya Ngurumo:eti Rais ndie amezuia Bunge kuwa live utaona ubatili wa hoja zake.Ngurumo anamtaka Rais aruhusu Bunge kuwa live kwa sababu inawapa shida wananchi.

Ngurumo aache kutetea ajenda za kifisadi.Amefanya wapi huo utafiti lakini pili hivi nchi zote duniani ambako Bunge haliko live maisha ya wananchi yakoje?Je Bunge kuwa live ingekuwa kigezo cha demokrasia Marekani au Uingereza wasioonesha wangekuwa wapi ktk historia?

Watoa ushauri wa aina hii Rais aachane nao kwa sababu kwanza hakuna sheria,ukiondoa miswada anayotakiwa kupitisha na maslahi ya Bunge, inayompa Rais madaraka ya kuingilia utendaji wa kila siku wa Bunge.

Mzee Magufuli kumbuka kuwa hawa hawa wanakulaumu kuwa wewe hufuati sheria leo wanakushauri uvunje sheria ili waibuke waseme zaidi?

Ni hawa hawa ulipotoa ushauri muhimu wa ufanisi Mahakamani walikujw juu eti umeingilia Mhimili huo lakini leo wanakutaka uingilie Mhimili wa Bunge?

Ngurumo na Ukawa wajipange zaid kwani hata ushauri wa namna ya kuongoza nchi anaoutoa si yeye wala wakubwa zake wenye uzoefu huo kwani hawajawahi kuendesha hata mkoa na pale ambapo walau wana Halmashauri juzi tumejionea ripoti ya CAG ikiziumbua Halmashauri za chini ya Ukawa nyingi zikiwa zimekithiri ufujaji wa mali za umma.

Ngurumo hana mawazo makuu ya kuzidhauri Halmashauri hizo ili zifanye vyema?

Nimesoma pia Ngurumo akilialia kuhusu wasaidizi wa Rais kuwa hawamsaidii.Hii inashangaza kwa sababu kama wasaidizi hao hawaripoti kwake anawezaje kujua kuwa hawamsaidii Rais?This is the lowest link.

Nimesoma pia akilalamikia mikutano ya siasa kuzuiwa na kimtaka Rais aingilie kati.Wapi na wapi?Sheria ya Jeshi la Polisi ndiyo inayowapa mamlaka polisi kudhibiti mikusanyiko. Hakuna mahali Rais alipo na mamlaka ktk eneo hilo kwa mujibu wa sheria hiyo.

Na hapa Ngurumo anayejipambanua kuwa mshauri mzuuuuuuri anataka kumuingiza Rais mkenge aliagize jeshi lisifuate sheria ili yeye na kundi lake waibuke na kuunguruma kuwa ni dikteta.

Au ndio kusema Ngurumo anataka ushauri wa Rais kufuata sheria usiwahusu yeye na kundi lake yaani koote afuate lakini yakija maslahi yao avunje.Ndio demokrasia wanayoipigania hiyo?

Ngurumo amerukaruka hoja nyingi mara Rais hasomi hotuba mara hivi mie nadhani asitumie nguvu sana kuhangaika na JPM.

Kwanza anachokisema anajua si kweli:yapo maeneo Rais binafsi nimeona amesoma na ilipobidi ameongeza mambo mapya kutokama na muitikio wa hadhira
Hii dunia nzima ipo.

Lakimi Ngurumo anahangaika na huku kisa nini?Kuna bosi wake hajawahi kusoma hotuba iliyoandikwa na hata alipojaribu aliishia kutetemeka na kusema itawekwa ktk website...huyu nilidhani anahitaji zaidi msaada wake kuliko kumshauri JPM.

Wapinzani wa nchi hii hawana jema. Ushauri wangu kwa Ngurumo ni huu: JPM anawashauri wa kutosha sana na ambao ananguvu za hata wakikosea kuwabadilisha na kuwa na wengine na kwa idadi atakayo.

Kuna watu hawana washauri kabisa na ni aibu kwa siasa za nchi na mustakabali wa Taifa.

Kuna watu juzi waliwaponda mafisadi kwa kutokwa povu lakini leo wanawatetea mafisadi hao hao hawa tunahitaji na kwa hakika tunasubiri ushauri wa Ngurumo kwao.Hawa unasemaje Bw. Mshauri makoni Ansbert Ngurumo.
 
Hapa utajua kiwango chako cha elimu ni kidogo sana. Lazima utofautishe utawala na uongozi na utawala/uongozi wa sheria. Tatizo la first 46 Lumumba FC elimu ni ndogo,hawajui tofauti ya uongozi na utawala,taasisi ya urais,utawala wa sheria nk
 
Ansbert Ngurumo; mwisho wa zama
By Maxmilian Alexander
...Je Bunge kuwa live ingekuwa kigezo cha demokrasia Marekani au Uingereza wasioonesha wangekuwa wapi ktk historia?
Tarishi aka Maxmilian Alexander, nimekuita hivyo kwa sababu moja, kama Tarishi asingekuwa Maxmilian Alexander hangethubutu kuleta uongo, upuuzi na ujinga huu JF. Mathalan hebu tuchukulie kwamba wewe Tarishi siye Maxmilian Alexander, una tofauti gani na mtu anayeokota kopo barabarani halafu anaanze tu kubugia kilichomo ndani ya yake? Kwa sentensi niliyoinukuu hapo juu ni kama vile umeokota kopo, ukalibeba hivyo hivyo na kulileta humu...kumbe kopo limejaa kinyesi.

Maxmilian Alexander, aliyewaambia bunge halionyeshwi "live" Marekani na Uingereza ni nani? Hakuna nchi ya Kidemokrasia bunge linafanya shughuli zake gizani. Kama umeamua kubugia kilichomo ndani ya kopo, rhuksa, lakini usijaribu kutulisha sisi wenye akili timamu. Ni kweli viko viumbe vinavyoishi kwa kula kinyesi na amini usiamini viumbe hivyo vimenona kweli kweli.
 
Ngurumo ni mwandishi mahiri hapa Tanzania. Hapa katikati alipotea kidogo. Ila sasa naona kaamua kurudi katika tasnia hiyo kwa nguvu. Nilimsoma wiki iliyopita katika Mwanahalisi. Caliber ya Ngurumo ni Jenerali Ulimwengu; na Kondo Tutindaga.

Huko Uhuru mna waandishi au makanjanja tu?
 
Ngurumo ni mchumia tumbo aliyevuka mipaka..yupo tayari hata kisema uongo ili kuhalalosha hoja zake dhaifu
 
Wewe na Ngurumo nani aliechambua mambo kwa undani akaeleweka? Hivi viroba mnavyokunywa ni hatari kwa afya yenu na akili pia
Buku7 wanazopewa wananywea viroba halafu wanakuja jf kutapika pumba
 
Isee Wewe Alexandra sijui Nani ondoa uchafu wako huku. Kwanza mtiririko huna hueleweki unatetea kipi, unajikoroga point huna. Barua ya Gurumo ipo open sana inaeleweka na mpangilio na maelezo yapo wazi na kimsingi ndio tunayosikia na kuona huku mtaani. Wewe ndio wale aliowasema mnaogopa kusema ukweli Bali mnaona Bora mseme Mkuu anachotaka kusikia. Gurumo sio level yako, njoo upige story na wanangu ndio level yako katika kuchanganua mambo.
 
Muandishi ama ni muongo asiye na aibu au ni hopelessly pumbavu
Ati Makufuli hakuzuia mikutano bali ni polisi,huu ni ujinga ambao ni mwana kijiji wa Chamwino tuu anaweza kuamini
Peleka ujinga huu kwenye vijarida vya Uhuru/Mzalendo
 
ANSBERT HAJAWAHI KUANDIKA UWONGO

Hakuna mwandishi muongo kama Ansbert Ngurumo, anawaandikia wajinga wasioweza kutafakari, nenda katika facebook yake uone waandishi wenzako wanavyomgaragaza live, kule hawafichi majina kama huku kwetu, ni watu anaofahamiana nao fika, na wanamwambia live, huu ni uongo!
 
Back
Top Bottom