Kwahili nakubaliana na FAIZA FOXY

Kwahili nakubaliana na FAIZA FOXY

Baada ya kupitia uzi unaomuongelea mtoto wa miaka mitatu mwenye uwezo wa kufanya hesabu na kuongea kiingereza' nimepitia comment za watu tofauti lakini nachelea kusema naungana na Faiza Foxy kwamba huyo mtoto anaendeshwa na nguvu ya ziada.

Nasema hayo nikiwa na mfano hai' kama mtakumbuka Sheikh SHARIF IDD ilikuwa habari nyingine kabisa' yaani toka Yuko tumboni mwa mamaake inasemekana alikuwa anaongea (nasema inasemekana kwa sababu sijawahi kumsikia zaidi ya kuhadithiwa Tu)'' sasa Leo hii huyo Sheikh Sharif ni tapeli mwalijua hilo?

Kwa sababu kwa hali ya kawaida watu ambao ni 'majiniazi', 'ujiniazi' wao hauanzi kutoka kusikojulikana'. Yaani mtu baada ya kufundishwa kitu ndipo anafanya kwa kiwango cha juu na kuongeza vitu ambavyo mpaka mfundishaji anashangaa kuona', mpaka nafsi ya mtu muwezeshaji inakubali na kusema huyu mtu atakuwa na uwezo wa ziada.

Sasa huyo mtoto eti anafanya hesabu za Sekondari kafundishwa wapi? Na nani mfundishaji wake? Bora angekuwa anaongea kiingereza tu tungesema labda anasikia kutoka kwa watu wanaomzunguka, lakini hili la kusolve hesabu kuna ???? Nyingi Sana.

Majiniazi wengi ambao wana uwezo mkubwa hata kabla ya kupelekwa shule. Uwezo wao huonekana kwenye vitendo, mfano utaona mtoto anabuni kutengeza kitu fulani mpaka unayemuona unashangaa kajulia wapi? Lakini sio kufanya vitu vinavyofanywa kwa formula fulani kama hesabu.

Na watu wa namna hiyo hata asipopelekwa darasani au kufundishwa kitu anakuwa na uwezo mkubwa wa utendaji kwenye fani fulani, mifano mingi juu ya hilo mtakuwa nayo wenyewe!

Kwahayo machache nakubaliana na mtazamo wa FaizaFoxy juu ya huyo mtoto upo sahihi kabisa, anayebisha na abishe Tu!!

Tujitahid kumuomba Mungu atupe jicho la tatu; yaani tuwe na uwezo wa ziada wa kuyatizama mambo na sio kuamini kila unachokiona na kukiskia. Hivyo huyo mtoto ana jini ndilo linalofanya hayo yote.

YESU au Nabii ISSA mwenyewe alizaliwa kama mtu wa kawaida kabisa ila matendo yake ndio yaliyowafanya watu waamini kuwa huyu mtu sio wa kawaida.


Faizafoxy yupi au yule mdini? Kama ni huyo na wewe huna hoja ya msingi pia.
 
Faizafoxy yupi au yule mdini? Kama ni huyo na wewe huna hoja ya msingi pia.
Kumbe hoja inayeyuka akiwa huyo unaemdhani wewe? Kwahiyo hata akiwa na hoja ya msingi' kwako inapoteza uzito wake kwasababu ni Faizafoxy?
 
Mh nimebahatuka kumuona huyu mtoto..hakika ni genius duuu huyo mtoto ana watoa nishai hata watangazaji....hahhahaha duuu
 
Back
Top Bottom