Kwahili Muhongo nakupa tano

Kwahili Muhongo nakupa tano

Kiutendaji Muhongo namkubali, ni mtendaji mzuri sana. Uwepo wa Muhongo, Magufuli na Mwakyembe ndiyo angalao unaofanya serikali ya Kikwete ionekane ina uwezo wa kufanya baadhi ya mambo muhimu.

Lakini 2015 ni lazima CCM iondoke maana tunataka serikali iliyokamilika siyo ya mawaziri wenye uwezo wa kufanya kazi watatu tu.
 
kama mngejua toka aingie kwenye wizara ya nishati, kaongeza madeni huko tanesco kiasi gani msingekaa kuleta uzi wa kishoga kama huu

ni hero madeni yanayoelekezwa katika masuala ya maendeleo hata ukimwmbia mtoto mdogo atakuelewa kuliko Yale ya kununua ndege ya raisi ambayo toka day one haijawahi kuonekana kwanini watu tulikula nyasi ilimradi tu inunuliwe
 
hakuna maajabu hapo,,, hayo ni majukumu yake na serikali.... hapo tunaweza sema akiwa kama waziri wa nishati ametimiza majukumu yake, asingefanya tungemlaumu kwa kutomiza majukumu yake na kwa kuwa amefanya basi hatuhitaji kumpongeza ni kazi yake kama mzazi kulea mwanawe.
 
Mtamsafisha sana lakini hamtoweza maana hata CCM wameshatoa maazimio ya kumtosa bila kumuangalia usoni! JK anashindwa afanyeje kwakuwa Jamaa aliletwa na USA kuhujumu TANESCO na kuhakikisha GAS haiwanufaishi Watanzania... Huyu Jambazi hatufai ... Fedha za ESCROW alizowagawia ili mumsafishe ni bora mka-save maana zitakwisha kwa kununua Bundles ...

unaweza kutudhibitishia haya uloyaandika?
 
Wewe ni chizi fresh, muanzilishi wa mpango wa umeme vijijini ni Ngeleja, hela zote tunakatwa kwenye mafuta na luku na wanaosimamia mradi ni Tanesco. Sifa mnazompa huyo Muhongo na hata mkate viuno namna gani haitasaidia maana lazima atoswe, then mtaona kama umeme vijiji hautawashwa

Hakika hata mimi ninawashangaa hawa walionunuliwa kupiga debe kwa asiyestahili na mwenye dharau kuliko mawaziri wote waliowahi kuwapo na watakaokuwapo.
 
Sospeter Muhongo ni kiongozi aliyeonesha ufanisi mkubwa kiutendaji ndani ya muda mfupi sana, big sana.

Afanye ufanisi kiutendaji kwa kuwataja watu waliopata mgawo wa pesa za ESCROW ACCOUNT zilizopitia STANBIC BANK (70% ya zote), hata kama ikitokea na yy yumo.
 
Pasipo kumung'unya maneno muhongo ni kiongozi anayeongea ukweli unao uma na so uongo wa kutufurahisha. Ki utamaduni na siasa za tz tumeshaaminishwa kuwa siasa ni uongo na ndio tunao upenda wengu wetu. Ki msingi majibu aliyoyatoa huyu mheshimiwa hayana tofauti kabisa na ya mh rais, hivyo yeye alisimamia jibu LA serikali siyo matakwa yake binafsi

Wito
Ni vyema tukawa watu wa kupima hoja kisha kufanya maamuzi. Mathalani ktk moja ya majibu yake juu ya vitalu vya gesi na uwekezaji wake, alitaja wafanyabiasha wakubwa kuwa ndo wanyonyaji wa nchi hii, mfano ndugu mengj ambaye ana miliki ardhi Kubwa yenye madini lkn hata hajafikiria kuiendeleza. Kwa mantiki hiyo ndug mengi amezuia ajira nyungi na bado anaikisesha kodi serikali
Kama hiyo haitoshi. Alishasema pale wizarani waende watu wenye nia njema ila rushwa mwiko rejea mazungumzo yake na viongozi wa dini.
Mwisho, wanasiasa wameshika matarajio yetu chanya lkn ndio hao hao wameshika matarajio yetu hasi, yatupasa si kuwasikiliza tuu Bali nasi tuwapime kwa kuwasikiliza kisha kupima
 
wananchi vijijini wamemuona prof.muhongo kuwa ni mkombozi wao kwa kusimamia vilivyo usambazaji wa umeme vijijini. wananchi wamekuwa wakimzawadia mbuzi kuku na mazao mbalimbali ya mashambani wengine wameenda mbali kwa kumuombea dua zenye rehema tele.
 

Attachments

  • 1422047895252.jpg
    1422047895252.jpg
    30.1 KB · Views: 157
Unamsafisha ili iweje?
Kama kuna mipango ya umeme vijijini ndiyo ulikuwa wajibu wake. We ulitaka afanye nini alipoteuliwa waziri?
Kwa hili swala la wizi wa Escrow hasafishiki hata mfanyeje.
 
Unamsafisha ili iweje?
Kama kuna mipango ya umeme vijijini ndiyo ulikuwa wajibu wake. We ulitaka afanye nini alipoteuliwa waziri?
Kwa hili swala la wizi wa Escrow hasafishiki hata mfanyeje.

weka ushahidi wa haya madai yako kama mie nilivyoleta,usituletee porojo.
 
Mwongo (muhongo) mwizi fact ziko cag,takukuru na rejea riport ya pac.jizi lile mpango wa rea ulikuwepo na he ought to supervise it,wizi ni mpango wake so hawezi kujsafshia gvt long term plan....no no no,muhongo is muongo and fraud.
 
wananchi vijijini wamemuona prof.muhongo kuwa ni mkombozi wao kwa kusimamia vilivyo usambazaji wa umeme vijijini. wananchi wamekuwa wakimzawadia mbuzi kuku na mazao mbalimbali ya mashambani wengine wameenda mbali kwa kumuombea dua zenye rehema tele.

Hivi watanzania mkoje?
 
Back
Top Bottom