Kwahili la Kagera, serikali isahau misaada ya majanga tena

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,300
23,022
Baada ya wananchi, mashirika, makampuni na hata nchi mbalimbali zilizohusika katika kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililoikumba kagera, nahisi hii itakuwa michango ya mwisho toka kwao.

Wengi waliochangisha walitegemea fedha hizo zitawafikia wananchi walikokumbwa na tetemeko hilo katika kuwawezesha kujenga miundombinu na fedha za matuizi ktk kipindu cha mpito.

Kitendo cha serikali kuitumia fedha hizo kwa matumizi ya kukarabati miundombinu yake, kimewafadhaisha sana wadau waliohusika kutafuta na kuchangia maafa haya.

Ilikuwa ni jukumu la serikali kujenga miundombinu yake pasipo kutegemea misaada iliyotoka kwa wasamaria wema.

Tumeshuhudia serikali nyingi na makampuni mengi kujenga na kukarabati shule zilizoharibika.

Serikali inapaswa kutoa fedha hizo zilizotolewa na wasamaria wema kama ilivyokusudiwa na waliotoa fedha.

Hii itakuwa ni misaada ya mwisho kwa watu kuchangia pindi ikitokea janga jingine, kwani itazoeleka fedha zinachangishwa lkn haziwafikii wahusika na kufanywa kwa matumizi mengine.
 
Wameingia choo cha kike ...na hiyo 90bn iliyobaki sijuhi watafanyaje make isingekuwa ni ujinga wao naamini wachangiaji walikuwa tayari kuendelea kuwachangia wenzao sema kwa huu ujinga wa hivi hayupo tena wa kusaidia.

Wajibebe wenyewe, tamaa zao zimewaponza
 
Back
Top Bottom