Kwaherini wana_Forum



Pole Ngida1...

Na Hizi je??
 

Attachments

  • ARI1.jpg
    26.7 KB · Views: 34
  • ARI2.jpg
    12 KB · Views: 41
  • ARI3.jpg
    12.9 KB · Views: 46
  • ARI6.jpg
    31.7 KB · Views: 48
maisha bora kwa kila mtanzania

Labda sisi ambao hatupata maisha bora basi si Watanzania...eeeh sasa tusemeje? wenye nchi yao weshajipatia gud life tayari...
 
Ndio uhuru wa JF. Ameamua kutoa burudani kuwaondoa watu kwenye fikra nzito ili watafakari mambo mepesi. Siku nyingine atasema anataka kuachana na kuvuta hewa hii ya bure kwa kuwa mafisadi wanapolute sana. Hapo napo atapata wachangiaji kibao!

Leka
 
Jiendee salama na Mungu akubariki, jamii forum ni mtakuj, soon utarudi
 
Unaniacha hoix3. Kijana mdogo unaogopa kupambana? Yaonyesha u mdhaifu sana kimwili, kihisia na kiakili.
 
Mhh jamani hivi kila mtu kama angekimbia nani angetuletea uhuru katika bara hili la Africa??!!!. Hakuna mtu yoyote kutoka dunia nyingine atakuja kutuletea maisha bora kwa kila mtanzania, bali sisi wenyewe. Watanzania kwa pamoja tukiendelea kuelimishana, kupinga mabaya, kusifia yaliyo mazuri, kufanya kazi kwa bidii na kujituma na mengine mengi, mimi naamini kabisa iko siku tutafika tuuuu.
Of course njia ya mkato ya kufika mapema ni kumpata kiongozi aliye msafiiii, atakayekubali na mwenye ubavu wa kuwaface hawa mafisadi. Ukikutwa na hatia za wizi kama hizi basi WAPIGWE RISASI WAFE, WANYONGWE KAMA VILE INAVYOFANYIKA HUKO CHINA. Wakipigwa risasi watu kama 100 hivi nawaambieni viongozi watashika ADABU, hakutakuwa na wizi mbaya kama tulio nao sasa. Viongozi lazima wajuwe kuwa wanapochukuwa form za uongozi wanaipenda nchi yao na wanataka kuitumikia, ni sawa na kuwa padre, au sister kanisani (RC).
Kama mtu hawezi kuwatumikia watanzania kwa hicho kipato kidogo anacholipwa aache asiende huko, akatafute kazi kwenye makampuni ya SIMU, MATANGAZO, BIA, SIGARA, nakadhalika. Aiache na atuache watanzania salama salimini. Viongozi wasiingie kwenye kazi za siasa wakitegemea kutengeneza PESA KWA NJIA ZA WIZI wa aina mbalimbali.


Ndugu Ngida1 karibu tena ulingoni, kukimbia matatizo siyo kutatuwa matatizo. Ukiyakimbia matatizo ya nchi yako, unategemea nani ayatatuwe??? haya ni ya kwetu wote mimi na wewe, sisi na wewe, tusichoke mpaka kieleweke.

Aluta kontinua mapambano yanaendelea. Pamoja tutaweza.
 
Kukimbia JF Sio mwisho wa matatizo hata mitaani utasikia 2 habari za mafisadi magazetini wanaandika habari za hao jamaa hata TV utakuta wanaongelea maswala ya ufisadi utakimbilia wapi?
 
pumzika kwa amani kaka!
ila naamini kuwa mda si mrfu utarejea
 
Ngida1 kesha rudi, tunaye hapa mstari wa mbele katika vikosi vya JF. Nadhani ndo mwanzo wa mapambano, hakika tutafika salama. Naimani, humu ndani baada ya mafisadi, tutapata waziri mkuu humu ndani ya JF hata raisi tutampata humu ndani.
Ngida1 ahsante sana, kwa poat yako inafundisha, inatia moyo.
 
Mimi ni msomaji wa magazeti pendwa na hasa interest yangu ni hadithi na makala za mafunzo hasa ijue afya yako na ile tafsiri ya kitabu maarufu "you are what you eat" lakini hivi karibuni magazeti haya yananichefua hasa yanapoandika habari za aliyekuwa mrembo wema kila siku. Hivi hamna jipya. Mkidhan mnamuumbua kumbe mnajaza vichwani mwa wasomaji na siku akigombea ubunge ataupata hivihivi. Tafuteni jipya. Soryy wale wa kwaherini wana- forum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…