Zanzibar 2020 Kwaheri ya kuonana CCM

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,934
3,805
Salaam kutoka Zenji ,kuna uhakika kutoka kila pembe kuwa sasa ni rasmi CCM imeshazikwa Zanzibar,hilo halina mjadala ,jukwaa la CCM Zanzibar CCM huchawanyika na kumuwacha/chia baba na mwana kwenye jukwaa.
Huyu baba ameenda kufanya nini mbona anamharibia mwanawe ? Husein unahisi ana ukakasi fulani ,huwezi kurapu ukaeleweka kama mzee wako yupo pembeni.

Ukweli ni kuwa CCM haipo imeshafutika kwa wananchi ambao ndio wapiga kura,kila lifanywalo na kupangwa na kina Bashiru kutoka Tanganyika huwekwa uwanjani,mipango na mbinu zote zinajulikana na wananchi sasa kama wananchi au tuseme WaZanzibari walio wengi wanajipanga kupambana na hila hizo ovu,

CCM ijue Zanzibar watu wao wanauelewa wa uraia wao na hawababaiki na mambo ya siasa wanaangalia zaidi muelekeo wa Nchi yao na hatari inayoikabili ,kusema kweli CCM wamevuruga kumuweka Husein Mwinyi,wangeweka nokoa yeyote yule Mzanzibari kuliko kumuweka mtu ambae hata mitaa ya Zanizibar haielewi,na kusema kweli wamempa wakati mgumu sana Husein Mwinyi ,sasa hajui achague nini kati ya dini na dunia.

Mipango ya Bashiru au tuseme CCM yote ipo njenje na inaeleweka tena inaeleweka hatua kwa hatua,kuna ulazima gani kulazimisha ushindi ? Kwamba ni lazima CCM ishinde,wakati haikushinda chaguzi zilizopita ambapo kulikuwa na wagombea waZanzibar atakuja kushinda huyu ambae CCM wenyewe wametifuana ndani wenyewe kwa wenyewe na hawajakaa sawa hadi leo.

CCM acheni mbinu chafu mtaumbuka na mpira utakuja kuwaangukia watumika.
 
Hii ya wafanyakazi wa Zanzibar kupiga kura tarehe 27.10.2020 badala ya 28.10.2020 inatakiwa iangaliwe upya japo iko kwenye utaratibu wa ZEC.
 
Nasubiri kuona CCM watakuja na mbinu gani safari hii (tangaza tu watatjiju, kujecha, engua engua etc), Senate ya Marekani inapiga darubini kali na "Babu Madevu" (Sauti ya, na kejeli za, kiumbe kinaitwa Polepole) amejipanga. CCM iwe tayari kukubali ushindi wa kura vinginevyo watakaribisha balaa la umma kuwang'oa.
 
Hii ya wafanyakazi wa Zanzibar kupiga kura tarehe 27.10.2020 badala ya 28.10.2020 inatakiwa iangaliwe upya japo iko kwenye utaratibu wa ZEC.
Hii ya kupiga kura 27.10.2020 ni wafanya kazi wote au ni wale maalum watakao simamia uchaguzi?
 
Maalim apati kitu na akibweka saana basi umakamu wa Rais wa kwanza utamuhusu,amalizie maradhi yake ya sukari kwa miaka mitano,akamiliza hiyo mitano atupishe.
wembe ni uleule.
 
Yule Babu ndo ataing'oa CCM ?
Hilo ndio tatizo la CCM mnavamia na kumvaa mtu,sasa wewe kwa akili yako Maalim Seif unaweza kumkisia ana umri gani labda tukitumia hesabu za Mtume Muhammad Salallahu alaihi wasalamu wastani wa umati wake ni miaka 70 hapo unacheza na plus au minus tu.

Kwa hiyo ili Maalim asitawale au asiwe kiongozi inabidi CCM mpo tayari kuuwa ,sasa kwa hesabu zenu hizo mjue hampambani tena na Maalim Seif mpo na mnapambana na umma wa Wa WaZanzibari Maalim yupo katika extra time tu japo ninaweza nikafariki mimi au wewe maana sio ajabu kuanguka korokochi ikabakia nazi juu ya mnazi..
 
Zanzibar ya upinzani hoja kadhaa eti...
Skuli zote zitakua za ghotofa
Nitafuta madeni yote...
Dah, babu kachoka kwa kweli maana hapa hata mtoto wa darasa la pili B humdanganyi..
 
Hii ya kupiga kura 27.10.2020 ni wafanya kazi wote au ni wale maalum watakao simamia uchaguzi?
Hio janja imeshafichuliwa ila wamemdanganya afande Siro kuwa ni kwa wafanyakazi wa serikali na polisi,uwongo kitu kibaya sana,sasa mpange majambo ikiwa mpo wengi na mnaaminiana,leo ndani ya CCM ni Zanzibar ni wanachama mabomu matupu ,maana kuna waliotifuana juu ya mgombea wamo wamejaa tele wamo wenye imani kali za dini wamo wamejaa tele na wamo wale pangu pakavu tia mchuzi,wale ukiwapa ndururu,hutapika vilivyo.

CCM wa Zanzibar wa leo ni hatari kufanya nao mipango watakuja kuwasababishia aibu ya karne,kama mnanisikiliza achaneni nao kabisa,na kama mnaona wanaficha mikakati endeleeni nao.
 
Zanzibar ya upinzani hoja kadhaa eti...
Skuli zote zitakua za ghotofa
Nitafuta madeni yote...
Dah, babu kachoka kwa kweli maana hapa hata mtoto wa darasa la pili B humdanganyi..
Deni linalodaiwa na Zanzibar dhidi ya serikali ya Muungano ni kubwa balaa,hilo peke yake litajenga daraja kutoka Tanga hadi Pemba mtakuwa mnakuja kwa gari zenu,na pia kujenga njia ya chini kwa chini ya bahari tokea Ngazi mia hadi Saruji dar.
 
Back
Top Bottom