Kwaheri vita dhidi ya rushwa, Kwaheri Siasa safi, kwaheri Ukweli

Mao Tanzania

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
210
231
Asalam,
Mbiu zilipigwa, Kelele zilisikika, Wazalenda wakasema Sasa huu Ni mkuki wa mwisho kwa Adui Rushwa.

Msamiati wa kukata ukatamalaki, Mwenezi Polepole akafoka, kila alipopita akaonekana mbabe, mwenye nguvu, kuliko Hata Katibu Mkuu Kakurwa Bashiru.

Watia nia walimuogopa, alionekana Hana Mbwembwe. TAKUKURU ikasema inaiachia CCM imalizane na watu wake. Wazalendo wakakaa mkao wa kula.

Walioitwa walarushwa wameshinda, mkataji akasoma majina yote, akapokea taarifa zote, akaona Hata ambayo wananchi hawakuyaona. Lakini wameshinda.

Kwaheri Vita ya Rushwa, hitima imeshafanyika, Sasa tumeingia rasmi Siasa za nguvu ya pesa. Masikini na wanyonge tunawaombea heri katika maisha yenu.

KARIBU NGUVU YA PESA
 
Nikikumbuka mikwara ya Polepole na vita yake ya rushwa ndani ya chama nacheka saaana,hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
JamiiForums-1995350078_390x520.jpg
 
Magufuli ameshidwa vibaya sana tusitegemee mambo mapya. Rushwa imeamua. Kwa Katambi chuki imeamua mbelembele kule usukuma na ukanda ukatawala. Sasa ni rasmi viriba vile vile mvinyo mbovu zaidi. Mabadiliko yangeanzia kwa kuingiza sura nyingi mpya,Back to 1990s.
 
Kwan kuna siku uliwai amini kwa ccm hii ipo siku Rushwa itaisha
 
Magufuli ameshidwa vibaya sana tusitegemee mambo mapya. Rushwa imeamua. Kwa Katambi chuki imeamua mbelembele kule usukuma na ukanda ukatawala. Sasa ni rasmi viriba vile vile mvinyo mbovu zaidi. Mabadiliko yangeanzia kwa kuingiza sura nyingi mpya,Back to 1990s.
Huwezi kuingiza sura mpya kwa kamati ya maadili inayoongozwa na kibabu
 
Mimi ni mtia nia CCM, nimeamua kuhamisha majeshi, kesho nachukua fomu ACT.

Ngoja sisi watoto wa masikini tuwaachie wanyonge wala rushwa na ccm yao
 
Rushwa Rushwa Imetamalaki Tuliambiwa na Pccb kuwa imejipanga vizuri kupambana na Watoa Rushwa wakati wa kura za Maoni,Baadae Pccb wanatuambia Suala la Rushwa Wamewaachia CCM Wenyewe,Wenye Akili Kubwa tukajua Maji yamezidi Unga
 
Back
Top Bottom