Kwaheri 2016 karibu 2017

Kwenye familia ya Baba yangu tukikaa tunabishana sana kwenye masuala ya siasa na sisi tupo wanne vijana ila wote tunatofautiana kuna CCM na vyama mbadala kama CDM ila hatuwezi chukiana ni ujinga na upuuzi.

Hata ikithibitishwa kwamba baadhi ya watu wanapotea kwa ajili ya masuala ya siasa ni suala la kuangalia upya sisi ni ndugu moja na hata tofauti zetu ni kwa maslahi ya Nchi yetu tu na sio vinginevyo.
Happy new year in advance
Msimamo wangu uheshimiwe .
 
2016 NENDA BABA TUNASHUKURU KWA YOTE.

1. Tumetumbuliwa majipu mpaka chunusi nenda tu baba...
2. Tumewaona waliofaulu wakiitwa vilaza, tuliumia lakini tufanyaje.. Nenda tu baba
3.umefanya kabeji iwe nyingi kuliko nyama siku ya Christmas nenda baba
4. Umefanya tujue kulikuwa faru john na faru hadija yatosha baba
5. Ajira imezidi kuota mbawa,baba wasalimie mwambie 2017 akija anisajili kuwa mwanasiasa huenda nikapata dili.
6. Tumeshuhudia homa ya zika ikileta kizaa zaa nenda baba
7. Tumeshuhudia wimbo mpya wa taifa muziki-darasa,acha maneno nenda 2016
8. Tumeshuhudia watu wa Dar wakitamani kurudi mikoani wasijue kote namba zinasomeka nenda baba
9. Baba kugombania rimoti na watoto ,ataenda wapi pesa hakuna acha atulie kama daktari wa zamu..nenda baba
10. Tumeshuhudia ufunguzi wa daraja jipya na watu tunakesha kufanyia shooting na kupiga picha, tuliliona wapi asante baba
11. Tetemeko likawatesa ndugu zetu wa kagera na watu wakataka kupiga pesa kupitia mgongo wake ,2017 usifanye kama mwenzako baba
12. Mvua za masika nazo zimekuwa adimu sijui nazo zinahakikiwa? nenda baba
13. Sijasahau bomberdier zikanunuliwa watu wakaziita panga boy asante baba..
14. Simba wakaongoza ligi ,kaa nao baba wamekuwa wagumba muda mrefu
15. Hakuna siasa subirini hadi 2020 baba vyama vya siasa vina kazi gani sasa??... Nenda tu baba 2017 usiwe hivi baba
16. Tumeshuhudia Bunge likiongozwa toka kwa Mkulu! Bunge mtepeto kuliko yote, Bunge la kuimba mapambio ya kuusifu ukulu wa Mkulu.
17. Tumeshuhudia haki za ki Mahakama zikielekezwa toka kwa Mkulu. Huku mawakili wa serikali wakitumia sheria za makaburu kupata sababu za kugandamiza uhuru na Katiba yetu!
18. Ulikuwa mwaka mbaya kwa wanaohoji ukweli maana hawakuchukua muda "kutoweka"!
19. Ulikuwa mwaka ambao kupotea kwa mnyama kulipewa uzito kuliko zaidi ya binadamu zaidi ya saba waliouwawa, kufungwa kwenye viroba na kutupwa majini!
Ongezea nyingine hapo kumuaga 2016
 
Back
Top Bottom