Kwaajili ya Uhai wa Wasio na Hatia Huko Ukraine, Tuendelee Kuomba, Mwanga Umeanza Kuonekana

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,071
Mtawala shetani ni laana kwa watu wake, ni laana kwa majirani na Dunia nzima.

Hatukuwahi kushuhudia wala kusikia hata mara moja kuna kombora au hata risasi moja imerushwa toka Ukraine au nchi yoyote ya NATO kuishambulia Urusi.

Lakini mwanzoni mwa mwakajana, Dunia ilishuhudia kiongozi shetani wa Russia, Putin, akienda kuivamia Ukraine kwa vile tu aliamini Taifa lake lina nguvu kubwa za kijeshi, na hivyo anaweza kufanya chochote dhidi ya Taifa lolote.

Putin akasababisha mauaji ya kinyama ya watoto, wazee na watu wengine wengi wa rika zote, kwa maelfu nchini Ukraine. Putin pia amesababisha mauaji ya askari wengi wa nchini mwake na Ukraine, bila ulazima.

Mtu mmoja tu, Putin kasababisha roho za watu maelfu zipotee, na watu kwa maelfu kuwa wakimbizi. Bila shaka, watu wengi ndani ya Ukraine, na sisi wengine tulikumbushwa kuwaombea wananchi wa Ukraine walioingizwa kwenye mauaji na mateso ya vita.

Mungu hujibu maombi ya mwanadamu kwa wakati wake ufaao, na kwa namna ile ifaayo, na wakati fulani hata kwa namna ambayo haikutegemewa.

Leo, Dunia nzima, habari kuu, ni maasi ya askari wa kundi la Wagner dhidi ya jeshi la Urusi. Mpaka sasa kundi la Wagner limekwisha ua baashi ya wanajeshi, wamekwishadungua ndege 5 na jeshi la serikali zilizokuwa zimelenga kuwashambulia.

Wapiganaji wa Wagner wanaelekea Moscow huku wanajeshi wa Serikali wakiamua kusalimu amri. Ndege ya Rais Putin imeruka na kuelekea kusikofahamika, lakini Serikali imesema Putin bado yupo Moscow (ni kweli au uwongo, hatujui). Putin, mapema amelihutubia Taifa, kwa sauti na kauli ya kinyonge, na kusema kuwa hili ni pigo kubwa.

Hivi ndivyo Mungu wa haki anavyotenda kazi, akitaka kumpa ushindi mnyonge anayeonewa. Leo siyo Ukraine inayopambana na jeshi la Urusi, bali ni warusi dhidi ya warusi. Hii ni kumkaanga samaki kwa mafuta yake mwenyewe.

Wana wa Mungu, tumshukuru Mungu kwaajili ya maisha ya wasio na hatia huko Ukraine. Tuzidi kuomba ukuu wa Mungu dhidi ya Putin na wauaji wengine wote.
 
Mungu? This is nonsense.

Kwa nini hakujali mlivo fanywa watumwa na hao hao Western imperialists na kukoloniwa ?

Ni muda gani sasa Israel yapambana kuiangamiza Palestine ? Huku Israel ikiungwa mkono na hao hao western!.

Is your God blind&deaf in Palestine massacre done by Israel with blessings from Western ?
 
Alieanzisha vita Ukraine sasa anaishi shimoni kama panya 🤣🤣🤣
 
Attachments

  • Screenshot_20230624-184205.jpg
    Screenshot_20230624-184205.jpg
    68.6 KB · Views: 2
ukraine na russia vita yao ni psyop.. usishangae Ukraine aka"shinda" ili Biden apite 2024..kama vile Obama alivyo"muua" Osama 2011
 
Mtawala shetani ni laana kwa watu wake, ni laana kwa majirani na Dunia nzima.

Hatukuwahi kushuhudia wala kusikia hata mara moja kuna kombora au hata risasi moja imerushwa toka Ukraine au nchi yoyote ya NATO kuishambulia Urusi.

Lakini mwanzoni mwa mwakajana, Dunia ilishuhudia kiongozi shetani wa Russia, Putin, akienda kuivamia Ukraine kwa vile tu aliamini Taifa lake lina nguvu kubwa za kijeshi, na hivyo anaweza kufanya chochote dhidi ya Taifa lolote.

Putin akasababisha mauaji ya kinyama ya watoto, wazee na watu wengine wengi wa rika zote, kwa maelfu nchini Ukraine. Putin pia amesababisha mauaji ya askari wengi wa nchini mwake na Ukraine, bila ulazima.

Mtu mmoja tu, Putin kasababisha roho za watu maelfu zipotee, na watu kwa maelfu kuwa wakimbizi. Bila shaka, watu wengi ndani ya Ukraine, na sisi wengine tulikumbushwa kuwaombea wananchi wa Ukraine walioingizwa kwenye mauaji na mateso ya vita.

Mungu hujibu maombi ya mwanadamu kwa wakati wake ufaao, na kwa namna ile ifaayo, na wakati fulani hata kwa namna ambayo haikutegemewa.

Leo, Dunia nzima, habari kuu, ni maasi ya askari wa kundi la Wagner dhidi ya jeshi la Urusi. Mpaka sasa kundi la Wagner limekwisha ua baashi ya wanajeshi, wamekwishadungua ndege 5 na jeshi la serikali zilizokuwa zimelenga kuwashambulia.

Wapiganaji wa Wagner wanaelekea Moscow huku wanajeshi wa Serikali wakiamua kusalimu amri. Ndege ya Rais Putin imeruka na kuelekea kusikofahamika, lakini Serikali imesema Putin bado yupo Moscow (ni kweli au uwongo, hatujui). Putin, mapema amelihutubia Taifa, kwa sauti na kauli ya kinyonge, na kusema kuwa hili ni pigo kubwa.

Hivi ndivyo Mungu wa haki anavyotenda kazi, akitaka kumpa ushindi mnyonge anayeonewa. Leo siyo Ukraine inayopambana na jeshi la Urusi, bali ni warusi dhidi ya warusi. Hii ni kumkaanga samaki kwa mafuta yake mwenyewe.

Wana wa Mungu, tumshukuru Mungu kwaajili ya maisha ya wasio na hatia huko Ukraine. Tuzidi kuomba ukuu wa Mungu dhidi ya Putin na wauaji wengine wote.
Nafuatilia issue hii kuna mengi ya kujifunza.
 
Njia za MUNGU hazichunguziki pale unapowaza kufanya ubaya eti kisa Tu Una nguvu na jeshi kubwa hapohapo MUNGU anaweza kupindua Nia yako....
Dunia ya Leo ya Karne ya 21 huwezi kufanya alichofanya Putin na ukashinda, Acha tusubiri mwisho wake utakavyokuwa
 
Mungu? This is nonsense.

Kwa nini hakujali mlivo fanywa watumwa na hao hao Western imperialists na kukoloniwa ?

Ni muda gani sasa Israel yapambana kuiangamiza Palestine ? Huku Israel ikiungwa mkono na hao hao western!.

Is your God blind&deaf in Palestine massacre done by Israel with blessings from Western ?
Ukraine inahusikaje na mambo ya western kwa hapo amevamiwa western au UKRAINE?
 
endelea kujidanganya.

Rusia imeamua kufnya propaganda za kivita ili kuihadaa ukrine.
 
Hii post hadi chozi limenilenga lenga Acha Mungu aitwe Mungu
 
Mungu? This is nonsense.

Kwa nini hakujali mlivo fanywa watumwa na hao hao Western imperialists na kukoloniwa ?

Ni muda gani sasa Israel yapambana kuiangamiza Palestine ? Huku Israel ikiungwa mkono na hao hao western!.

Is your God blind&deaf in Palestine massacre done by Israel with blessings from Western ?
Usilinganishe mapigano ya Israel na Wapalestina na hii ya Russia dhidi ya Ukraine.

Ufahamu pia kuwa hakuna wakati hata mmoja ambapo Israel ilitangulia kurusha kombora lolote kwa Wapalestina. Ni makundi ya Wapalestina wenye misimamo mikali, mara zote ndio wanaotangulia kurusha makombora kwa Waisrael. Waisrael wanapojibu mapigo, ndipo hapo watu wasio na hatia hupoteza maisha.

Mauaji ya watu wasio na hatia kwa wapalestina, kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na makundi ya wapalestina wenye misimamo mikali.

Viongozi wenye hekima na wenye misimamo ya kati toka pande zote mbili, mara kadhaa, wamekaribia kufikia makubaliano fulani, lakini yale makundi ya Wapalestina yenye itikadi kali, wakati wote imekuwa ndiyo tatizo. Wao wanasema taifa la wayahudi linatakiwa kuangamizwa Duniani. Hakutakiwi kuwa na wayahudi.

Mgogoro wa Israel, inahitajika hekima. Lazima Wapalestina wakubali kupoteza kiasi na kupata kiasi, na upande wa Israel ni hivyo hivyo. Njia nyingine ilikuwa ni kwa wote kukubaliana kuishi kwa pamoja kama Taifa moja. Maana kwenye hali ya kawaida, uliona wapi nchi mbili ziwe na makao makuu ya nchi zao kwenye mji mmoja? Palestine kwa miaka yote huko nyuma haikuwa nchi. Ilikuwa ni sehemu ya nchi ya Israel. Wakapigania, wakapewa mamlaka inayojitegemea, na baadaye wakatangaza kuwa ni nchi. Lakini baada ya kutangaza kuwa nchi, tena wana dai jingine eti Jerusalem iwe makao makauu ya nchi ya Israel na Palestine. Je, hilo kweli litawezekana? Ni masharti ambayo kwa vyovyote yanaendeleza mgogoro.

Watu wengi na mataifa mengi yamejitahidi sana kushughulikia mgogoro wa Israel na Palestine, suluhisho linakuwa kama linakaribia kupatikana, lakini katikati ya kuelekea makubaliano, wapalestina wenye misimamo mikali wanarusha makombora kwa Israel. Majadiliano yanaishia hapo hapo.

Hali hiyo ndiyo inayofanya hata UN kutoilaani Israel. Kwa sababu Israel inasema kuwa inajilinda dhidi ya mashambulio. Wakati wote Israel inalaumiwa kutochukua tahadhari za kutosha kulinda watoto na raia. Lakini hawalaumiwi kupambana na wanaoishambulia Israel.

Kwa ujumla ni situation tofauti sana na ile ya Ukraine.
 
Njia za MUNGU hazichunguziki pale unapowaza kufanya ubaya eti kisa Tu Una nguvu na jeshi kubwa hapohapo MUNGU anaweza kupindua Nia yako....
Dunia ya Leo ya Karne ya 21 huwezi kufanya alichofanya Putin na ukashinda, Acha tusubiri mwisho wake utakavyokuwa
Putin amemwomba Rais wa Belarus, Lukashenko aongee na Prigozhin, kiongozi wa Wagner, kumwomba asiende Moscow. Haijafahamika bado Prigozhin amejibu nini.
 
endelea kujidanganya.

Rusia imeamua kufnya propaganda za kivita ili kuihadaa ukrine.

Fikra zako zinakutuma hivyo. Huwezi kusema kama ni uhalisia.

Hiyo ni dhana unayoiamini wewe, usiiweke kama ni kitu ulicho na uhakika nacho. Tujifunze kutofautisha kati ya hisia au fikra na jambo ambalo limethibitishwa.

Hilo ulilolisema halina uhakika.
 
Kwahio hao wasio na Hatia wakati wanauwawa walikuwa hawaombi au alikuwa anasubiri maombi yako wewe ili azuie maumivu yao ?

Kila kinachotokea huku ni happenstances na causative inapatikana huku huku A certain action gives out a certain reaction....
 
Back
Top Bottom