Kwa yaliyotokea Mwanza halipo Jipya

Kwa yaliyotokea Mwanza halipo Jipya

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Kwa yaliyotokea Mwanza kwa utawala huu kama ilivyokuwa kwa awamu ile, hakuna jipya.

Nisiache kumlilia hayati baba wa Taifa (rip) kiongozi mzalendo aliyejawa haiba zote za haki, uhuru na usawa:



Kudai haki, uhuru, demokrasia na maendeleo hakujawahi kuwa rahisi. Ni jukumu zito la kizalendo na kihistoria linalosongwa vilivyo na kila aina ya shari, uzandiki, vikwazo, hatari, visa, vifungo na hata vifo.

"No easy walk to freedom" -- aliyaona Nelson Mandela.

Ni kujitolea kuliko kwa kiwango cha juu sana kuipita njia hii katika hali ya uaminifu uliotukuka.

"Viva kamanda Mbowe, kamanda Heche na makamanda wote kokote kule mliko. Ama kwa hakika hamko peke yenu."

Hapa tulipo, ni mwanzo tu. Kurudi nyuma siyo uchaguzi. Tuendako ni kugumu zaidi lakini haki haijawahi kushindwa. Inshallah tutafika.

IMG_20210704_051559_619.jpg


Tangu lini yatima akadeka? Kama ulivyo mtaji wa masikini, mtaji wake ni nguvu zake mwenyewe.

IMG_20210707_084839_278.jpg


"Tusipowakataa na kuwapinga viongozi kama hawa, basi janga kubwa linakuja na tabia zao ni za kidikteta" -- Julius Nyerere.

IMG_20210707_085335_184.jpg


Ni dhahiri zaidi sasa kuwa katiba mpya ni muhimu na ya dharura sana kuliko wakati mwingine wowote.

Muhimu mipango mikakati mipya ikaelekezwe kwenye kujilinda na kuwafidia wahanga wote wa harakati hizi tukufu.

Aluta Continua!
 
Tangu lini Chaggadomo mkawa wafuasi wa Nyerere ?
 
Hata yangelikuwepo bado mngemtukana tu, kwani Mara ngapi hayupo na bado Lisu anamsema kwa mabaya! Pia hata kama angekuwepo Leo hii asingekubali haya mambo yanayo endelea Sasa hivi,
Nchi gani ambayo watu hao hawatii mamlaka ya nchi.
 
Baada ya maji kufika shingoni wanaona bora kupitia upande huo ili wafikie wanapopataka 😁!.

Although hii nchi ni nyepesi sana tatizo ni raia wake ndiyo wagumu kupindukia (waoga)

Maji gani ya shingo hapo sasa? Kwani tulipo hata kama mngekuwa nyie ni watoto wa kunyonya, tuseme ndiyo mngekuwa tayari ziwa mngeachia?

Chakula kuwiva ni shuruti kutokota vilivyo kwanza!

Kwamba mtakomaa mbona tuliyajua zamani sana? Pia tunajua mtajitahidi kukomaa hata zaidi?

Huu uzi ni wa June 20:


Ninakazia:

IMG_20210722_105127_480.jpg


Tuko imara leo kuliko wakati wowote katika historia.

Peleka habari hiyo kama mlikuwa hamjui.
 
Hata yangelikuwepo bado mngemtukana tu, kwani Mara ngapi hayupo na bado Lisu anamsema kwa mabaya! Pia hata kama angekuwepo Leo hii asingekubali haya mambo yanayo endelea Sasa hivi,
Nchi gani ambayo watu hao hawatii mamlaka ya nchi.

Kwamba?

"Hata yangelikuwepo bado mngemtukana tu, kwani Mara ngapi hayupo na bado Lisu anamsema kwa mabaya!"

Matusi unayajua? Matusi ni nini? Unamsomaje huyu mheshimiwa:

IMG_20210707_084839_278.jpg


Nyerere angekuwapo asingekubaliana na wewe. Nyerere hakuwa coward na wala cowardice haikuwa hulka yake. Hakuwa na nafasi na wanafiki.

Nyerere alikataa ukondoo (cowardice) na vyote vinavyoambatana nao. Labda kama unamuongelea Makongoro 😂😂!

"Alisema kweli daima fitna kwake ilikuwa mwiko. Binadamu wote walikuwa ndugu zake na kwake Afrika ilikuwa moja."

Angekuwapo mwalimu:

"Si ajabu mwendazake hata asingeupata uraisi. Kama angeupata, basi si ajabu kuwa Nyerere angeongoza harakati za kumfurusha 'unceremoniously' kutoka madarakani."

Fuatilia yaliyomkuta Mwinyi Senior kupata kujua.

Someni muifahamu historia. Historia siyo UNGWINI. Wala historia siyo hii ya kukaririshwa ya vishindo hewa vya awamu zenu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kazi ipo.

Kazi haiwezi kuwa ndogo au kutokuwepo. Leo hii tuna mayatima hapa nchini:

IMG_20210704_051559_619.jpg


"Julius?:
.
.
.
Tulikuwa naye siku zote za mapambano:
Mwenzetu,
Ndugu yetu,
Mwalimu Nyerere.

Ametuondoka wakati tukimhitaji:
Mwenzetu,

Ndugu yetu,
Mwalimu Nyerere.

Sasa Twende wapi tukapate ushauri:
Mwenzetu,
Ndugu yetu,
Mwalimu Nyerere.

Kiza kinene kimetanda hatuna pa kukamata:
Mwenzetu,

Ndugu yetu,
Mwalimu Nyerere.
.
.
.
....
"
 
Maji gani ya shingo hapo sasa? Kwani tulipo hata kama mngekuwa nyie ni watoto wa kunyonya, tuseme ndiyo ungekuwa tayari ziwa mngeachia?

Chakula kuwiva ni shuruti kutokota vilivyo kwanza!

Kwamba mtakomaa mbona tuliyajua zamani sana? Pia tunajua mtajitahidi kukomaa hata zaidi?

Huu uzi ni wa June 20:


Ninakazia:

View attachment 1863029

Tuko imara leo kuliko wakati wowote katika historia.

Peleka habari hiyo kama mlikuwa hamjui.

Cc: BAK Erythrocyte Salary Slip technically
Hata wenzako huwa wanajipa moyo as you wrote, so haishangazi kujitutumua kwa hilo although huwa hamuwezi kuandika yaliyo fail hata kwa sekunde moja!.
 
Hata wenzako huwa wanajipa moyo as you wrote, so haishangazi kujitutumua kwa hilo although huwa hamuwezi kuandika yaliyo fail hata kwa sekunde moja!.

Kuna mambo ya wazi lakini:

1. Kwamba mkutano wa Mwanza ulizuiliwa kwa sababu ya Corona? Hata mtoto mdogo anajua kuwa huo ni uongo wa mtu mzima hovyo, asiyekuwa na chembe ya aibu.
2. Kwamba kongamano lile lilikuwa kinyume cha sheria? Hata wewe utakuwa unajua si kweli.
3. Kwamba CCM ndiyo watoto pendwa ambao wako huru kufanya watakalo, ila hawa wengine ndiyo walio watoto yatima kwenye familia hii ya yule mama (mwovu kabisa) wa kambo? Bila shaka hata wewe unajua hivyo.
4. Kwamba wewe hudhani mustakabala huu wenye sheria za kibaguzi (zenye kuegemea utashi wa mtu kwa kuwa yuko madarakani kwa wakati huo) ni jambo la hatari kabisa lenye kuhitaji ufumbuzi wa haraka?

Kwamba ni kweli kwa dhati yako kuwa huoni hivyo? Au labda ni kwa sababu ya unafiki tu? Au ni kuwa u mnufaika wa "status quo?"

Si kila mtu anaweza kuukubali ukondoo (cowardice) tunazoshinikizwa wengine kuuishi. Kuukataa ukondoo si hatia. Pia kuukataa ukondoo kwa gharama yoyote hakuna maana ya kujitutumua kama unavyojaribu kujidanganya wewe.

Kwa maana yako ya kujitutumua, basi hata huyu mwuungwana utakuwa unamhusu:

IMG_20210707_084839_278.jpg


You must be kidding!

Kwamba?

"... although huwa hamuwezi kuandika yaliyo fail hata kwa sekunde moja!"

Hakuna recorded failures duniani katika madai ya haki, achilia mbali hapa kwetu.

Labda kama unataka kutuchagiza kuandika failures zisizokuwapo mkuu?!
 
Hata yangelikuwepo bado mngemtukana tu, kwani Mara ngapi hayupo na bado Lisu anamsema kwa mabaya! Pia hata kama angekuwepo Leo hii asingekubali haya mambo yanayo endelea Sasa hivi,
Nchi gani ambayo watu hao hawatii mamlaka ya nchi.
NB: Hata makaburu walisema hivyo hivyo kwamba wananchi wa Afrika Kusini lazima watii mamlaka ya nchi, wakoloni vile vile walitumia lugha kama hiyo na hata Hitler, Idi Amin wote amri yao ilikuwa ni hiyo hiyo.

Kwa hiyo hamna jipya hapo. The more things change, the more they remain the same.
 
Kuna tetesi Kuna zengwe anaundiwa mama ili aachie usukani ndani ya chama 2025, inasadikika mkakati unapangwa na vigogo ccm na serikalini.Lengo Ni kumfanya mama asikubalike kwa umma...
 
issue wala siyo katiba mpya, kuna jambo fulani ovu linalotakiwa; hii ni njia inayotumika ni namna tu ya kupita na kujaribu kuwapumbaza watu fulani wasing'amue ni nini haswa kinachoendelea..........nashukuru, nao wapo macho na makini kweli kuangalia haya yanayoendelea ingawa bado wapo kimya kwani ikifika muda wa kusema watasema. wameshahisi kitu, kuwa kuna na jambo......tena jambo haswaaa!!
 
Back
Top Bottom