Kwa yaliyonikuta...

Waterlemon

Senior Member
Sep 2, 2016
137
178
Kwa yalionikuta,

Wiki iliyopita jioni narudi toka kibaruani, nipo ndani ya basi, limejaaa watu wamesimama mpaka kubanana. Mbele yangu kuna mdada kajaa mzigo nyuma na kajaaliwa... ananiegemea.

Basi likiyumba yumba huwa huzidi kujiegemeza na kwa hali ilivyozidi kuwa mbaya najikaza kisabuni maana mzee mzima nitaumbuka. Hivyo najaribu kuwasukuma abiria nyuma yangu japo nami nipate kupumua huku kidogo.

Nilipoona yamezidi nikaomba kushuka basi japokuwa nilikuwa bado vituo vichache kufika nyumbani. hamna tabu nitatembea isiwe usumbufu.

Nikapita genge moja naona kijana anachoma mahindi, nikaona bora niwachukulie watoto kidogo na mama yao huko nyumbani. Ile Natia mkono mfukoni kulipa, naguswa bega, mdada yule yule niliyemkimbia kwenye basi kanishtukiza nyuma yangu ananisalimu... Oohoooo

----------------------------------------------------------------------------
######################################
Majanga hayakuishia hapo. Yanaendelea chini baada ya utafiti
######################################
----------------------------------------------------------------------------

Nianze kujitetea kwa yafuatayo,

Huwa si kawaida yangu kushawishika hasa na anasa za maisha ya mitaani. Binafsi huiweka kichwani ya kuwa mruka njia kuisaliti familia yake ni matakwa ya mtu dhaifu asiejijua na wala kujua yapi mazuri kwake. Kusaliti familia yangu... mke na watoto wangu nyumbani... sijajiwekea.

Ila binaadamu tumeubwa na kasoro... na ukosefu fulani.

Mdada anajitambulisha (jina nitamhifadhi) ananiambia ananijua kimbali... yaani kawaida huniona sana kwenye pirika zangu nikielekea na kurudi kazini. Hupanda usafiri mmoja nami mara kwa mara na kawaida yake kunichora bahati hatujapata kunzungumza. Leo kaamulia. Nia yake tujuane japo kupoteza mawazo kwa mazungumzo.

Machale yananicheza lakini nashindwa kujibu kiakili halisi. Kufuatwa na watu ninaowajua na hata nisiowajua si mchezo niliozoea. Kwa mara ya kwanza nafeli mtihani wa kwanza hapa. Tunakubaliana kukutana ijumaa mahala kupata za ubaridi.

Anaondoa kuelekea upande wake nami wangu, mahindi mkononi naona yameota sumu. Siyaamini. Nayatupa vichakani njiani nyumbani.

Nafika nyumbani natafakari lakini nayawekea pembeni. Wiki nzima iliyobaki nashikwa na aibu fulani lakini ibilisi kanijaa kwa shauku hata la kupata kujua ni lipi litakatokea hiyo weekend? (Curiousity killed the cat!)

Haya ijumaa inafika nazunguka na shughuli zangu mda kuuangalia hausogei uzuri. Inafika muda najipa ujasiri kama hamna baya ninalofanya, hata condom ndani ya waleti yangu sijaweka. Najua nikiikosa hiyo angalau itakua kama ngao ya kutofanya lolote baya.

Muda inafilka kuibuka rendez vouz mdada tayari keshafika yuko shwaaaari ananisubiri. Tena anavutia zaidi ya nilivokuwa namkumbuka. Mdada tena kiufupi wala sio saizi yangu... alivojipodoa na kuutoa tena mpaka moyoni najiuliza hivi kweli haya? huyu mdada anaweza kunipenda mimi? lakini ibilisi kanishika shati sina jinsi.... haya twende.

Katika maongezi mdada tunaporoja kiwepeeeesi yaani ... mpaka kunifanya ile aibu na machale yangu yote kuondoka. Hali moyoni imenikaa uzuuuuri.. tunaongea mengi tu ambayo hata sitoyataja hapa... Niko so relaxed tayari, sina hata chembe ya wasi wasi. Mpaka mdada kuunyoosha mkono wake na kunipapasa kiganja cha mkono huku wangu ukipiga masaka kupima ujoto wa mapaja yake hapo pembeni ufukuni mwa meza. Yaani rahaaaa.

Kati kati ya mongezi nageuka, macho yanagongana na shoga yake mkubwa wife wangu kakaaa upande wa pili wa baa ananichora ....

Moyo unaniruka kutoka kifuani. Nikapiga kiti teke na kuinuka, mbio hata kuaga siagi. (bahati nzuri nishalipa hivyo siitiwi mwizi) Mahatua makuwa kutokomea nyumbani. Shoga wa wife namjua vyema, hana siri hivyo na habari nyumbani najua itafika kabla sijafika, mzee mzima nishaumbuka.

Nafika nyumbani kimyaaa. Namuangalia wife kwa wasi wasi. Lakini hasemi kitu. Sijui yameshamfia au vipi. Lililonibaki mimi ni wasi wasi tu. Wikiendi inafika shoga lile la wife linakuja nyumbani, mie huku tobaaaa... Naingia huku natoka huku, wasi wasi mtu na kichwa. Lakini inafika mpaka anaondoka wife naona yupo hali ile ile. Sijui keshaambiwa ila ananiachia niteseke na nafsi yangu au ndio hajaambiwa? Kumuangalia usoni vizuri siwezi.

Baya haswa sijafanya lakini nakiri nililikusudia hapo mwisho pale shetani aliponipanda. Sasa waungwana fikra zenu tafadhali nazihitaji. Nende mwendo gani hapa?
 
Hahahaaaaa! Mwenyewe atanilewa tu, ni swahiba wangu kitambo. Ana uvumilivu wa kutosha hatanishtaki kwa moderators
inasemekana hata Mungu na Shetani walikuwa maswahba

lkn kilinuka siku moja tu

sababu eti Shetani aliacha kiti chake na kukimbia kisicho chake

kikinuka nitashika jembe niende shamba
 
inasemekana hata Mungu na Shetani walikuwa maswahba

lkn kilinuka siku moja tu

sababu eti Shetani aliacha kiti chake na kukimbia kisicho chake

kikinuka nitashika jembe niende shamba
Kwa hiyo mkuu kikinuka utanitenga? Nadhani ndio utakuwa mtetezi wangu aisee
 
Kwa yalionikuta,

Wiki iliyopita jioni narudi toka kibaruani, nipo ndani ya basi, limejaaa watu wamesimama mpaka kubanana. Mbele yangu kuna mdada kajaa mzigo nyuma na kajaaliwa... ananiegemea.

Basi likiyumba yumba huwa huzidi kujiegemeza na kwa hali ilivyozidi kuwa mbaya najikaza kisabuni maana mzee mzima nitaumbuka. Hivyo najaribu kuwasukuma abiria nyuma yangu japo nami nipate kupumua huku kidogo.

Nilipoona yamezidi nikaomba kushuka basi japokuwa nilikuwa bado vituo vichache kufika nyumbani. hamna tabu nitatembea isiwe usumbufu.

Nikapita genge moja naona kijana anachoma mahindi, nikaona bora niwachukulie watoto kidogo na mama yao huko nyumbani. Ile Natia mkono mfukoni kulipa, naguswa bega, mdada yule yule niliyemkimbia kwenye basi kanishtukiza nyuma yangu ananisalimu... Oohoooo

Waungwana kitu kama hiki kikikutokea wenzangu huwa mnaichukulia vipi hii? Mnaiminya na kulaumu ibilisi au kichwa hucheza machale na kutimka mbio?
Nasubiria muendelezo mkuu aisee..
 
Usipokuwa mwangalifu unawezakuta unakitupa kwenye boxa af ikawa fedheha kulowa mbele ya kadamnasi........siku nyingine kemea pepo.....mana ni mapepo hayo
 
Back
Top Bottom