Kwa yalitokea Arusha sioni polisi wakilinda raia na mali zao!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wadau, hii dhana ya kusema polisi wanalinda raia na mali zao inaelekea kuisha. Kinachojionesha ni kwamba pale raia wanapotaka kuandamana kwa amani ili kutoa dukuduku zao wanaingiliwa na jeshi la polisi kwa kile kinachodaiwa "kuzuia uvunjifu wa amani." Kama polisi wanazuia uvunjifu wa amani wasingeweza kuwapiga raia wasio na silaha na kuwajeruhi kiasi hicho na hata kuwaua baadhi yao na kuharibu mali zao. Niliona baadhi ya polisi wakivunja gari moja lenye rangi nyekundu vioo - sijui nako kulikuwa kuzuia maandamano au ulofa!

Nijuavyo, kwa sheria za Tanzania, polisi hawapaswi kuombwa ruhusu ya kufanya maandamano bali kujulishwa na kutoa ulinzi wakati wa hayo maandamano. Lakini, kwa vile wamekuwa wakiombwa ruhusa, wamekua wakiwanyima Watanzania haki ya kuandamana kwa amani. Siamini kabisa kama polisi ndio wenye mamlaka ya kutoa haki ya kuandamana. Naona kama wanatumia 'arbitrary power' kuzuia maandamano ya amani na kama hali hii ikiachwa kuendelea polisi na raia watageuka kuwa maadui badala ya kuwa marafiki.

Kwa yaliyotokea Arusha, Mkuu wa Jeshi la Polisi na askari waliowapiga, kuwajeruhi au kuwaua raia wanapaswa kuwajibika!
 
Back
Top Bottom