Kwa wingi wa matochi barabarani, twaweza kukubali kutendeana haki na si kubambikiziana kesi?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,862
Wakuu kwa habari za vijiweni hivi sasa barabara zote Tanzania zimesheheni tochi vilivyo. Ninaamini lengo ni kuondoa kabisa ajali barabarani wala si kuongeza mapato kama wengi wetu tunavyodhani.

Kwa maana hii tunaweza tambua thamani ya maisha ya mtanzania mmoja ni kubwa kuliko makusanyo kusanyo ya bilioni mbili mbili kwa wiki tuzisikiazo dar kila leo.

Tunakoelekea bila ya shaka ni kumalizika kwa ajali kwa mujibu wa ahadi za mh. Waziri Kangi Lugora. Hata hivyo ilikuwa ni muhimu pia tukakubaliana katika ya msingi japo yafuatayo:

1. Tochi hizi zitayahusu magari yote barabarani yasiyokuwa katika misafara rasmi Bila kujali jina wala cheo cha mtu.

2. Vibao vya usalama barabarani vikiwemo vyote vya maonyo na amri vitayahusu magari yote yasiyokuwa katika misafara rasmi pasi na kujali cheo wala jina la mtu.

3. Polisi watajiepusha na mashitaka uchwara na ya kubambikiziana kama vile ni makazi ya watu wakiacha vibao na vibao tu kuwa ndiyo dira pekee ya adhabu au onyo.

4. Kila shitaka au picha ni shuruti iwe na ushahidi usio na shaka kuwa imepigwa katika eneo husika na si vinginevyo.

5. Kazi ya polisi na tochi isiwe adhabu peke yake. Ya adhabu na ya onyo yajulikane wazi wazi kwa wote.

6. Namna ya ku escalate grievances iwe wazi, timely na effective.

7. Tuelimishane tujue accuracy, tolerance, capability, weaknesqsqq, effectiveness na hata ufanyaji kazi wa hizi camera.

8. Kujifunza tokea kwa nchi zingine kuhusiana na matumizi, tolerance na hata mode ya adhabu na uzoefu toka kwa waliotutangulia sisi siyo kisiwa.

Itambulike kuwa ni jambo lisilo na tija kumwadhibu mtu kwa kosa la kubambikiziana no matter what the motive is.
 
Back
Top Bottom