Kwa wewe uliyeomba nafasi za kazi uhamiaji tegemea yafuatayo

mambali

Senior Member
Oct 16, 2012
172
64
Usaili utaanza tarehe 09/06/2014 hadi tarehe 26/06/2014 saa mbili asubuhi ktk ukumbi wa baraza la maaskofu kurasini, barabara ya Nelson Mandela wote walioitwa wanatakiwa kufika kwa tarehe walizopangiwa, hawa ni costable na coplo tu, tangazo limetolewa na kamishina mkuu wa uhamiaji, waombaji wanatakiwa wawe na viambata vifuatavyo, birth certificates origional, academic sertificates origional, living certicates origional, two passport sizes, any certificaticates of extra courses, wasailiwa wawe nadhifu, mchemekeo wa haja na tai ,viatu vyeusi ,kwa wasichana nguo za mbano na fupi hazitaruhusiwa wavae nguo za heshima, wale wenzetu waislam hijabu na barakashea zinaruhusiwa,kumbuka kuweka simu yako silent pindi utainiwapo au zima kabisa,mazoezi ya kupasha miili moto yanaweza kuwepo au yasiwepo, pia maswali yanaweza kuwa ya ana kwa ana ,dialogue au ya kuandika,vigezo na masharti kuzingatiwa.

Kwa wale Assistant Inspector mwajiri wao ni katibu mkuu, hivyo nao watapa taarifa za usaili kutoka kwa katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani ya nchi. Wale watakaofaulu kwenye usaili watapewa taarifa na watatakiwa kupima afya zao kwa lazima, na ujauzito, alama za tatoe kwenye miili ya watakaochaguliwa hazitatikiwa, kwa wale watakaokutwa na vvu na mimba nao pia hatakiwa kujiunga na mafunzo, Wale watakaochaguliwa watatakiwa kujiunga na recriting course miezi 6 au 9 Katika mojawapo ya vyuo vitatu vya mafunzo, ambavyo ni Police Academy Moshi, Prison Academy au chuo Jkt Ruvu, wale watakao bahatika kwenda mafunzo watalazimika kufuata sheria, taratibu na kanuni za vyuo husika mpaka watakapo maliza mafunza ya awali, bila kuvunja taratibu za vyuo husika.

Mara wamalizapo mafunzo ajira zao zitaanza mara moja,staili nyingine kwa wanavyuo mtaelezwa baadae, kwa kifupi hayo ndiyo yanaweza kujitokeza ila
mabadiliko ya mitaala na mafunzo yanaweza badilika kutokana na kasi mpya ya uaendeshaji wa idara na mabadiliko ya makamishina huko
makao,na mpango mzima wa bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi from jikoni.
 
Umesomeka Mkuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Dah aisee kweli Tanganyika imefika pabaya. Enzi zetu unabembelezwa kupewa posti kama hizi na unaringa bila aibu.!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom