Kwa wenyeji wa Arusha ONLY

Ntu

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
950
549
Wakuu nlikua nafanya kazi mkoa fulani na sasa nmepata kazi hapa Arusha. Na kwa bahati nzuri nmenunua kijibanda hapa, hivyo nadhani patakua makazi yangu ya kudumu. Dhumuni langu ni kujiunga na chama cha kufa na kuzikana, Plz mwenye kujua anijuze wapi nawezajiunga.
 
Hongera mkuu.
Ulitaka vya kikanda,yaanni vya kikabila au chochote.
Kama ni vya kikabila/kanda, fahamisha ni kanda au kabila gani unataka.
 
Mkuu chochote kile ilimradi kiwe na strong background and committed members katika masuala kufa na kuzikana!
 
Hivi vinakuwa vya kikanda,mfani, watu wa kaskazini,watu wa kusini,na pia kuna vya watu wa kanda ya ziwa.Kwa hiyo inabidi tujue we ni wa kanda ipi ili tukuelekeze vizuri. Itashangaza we asili yako Kagera ujiunge na chama cha watu wa kusini. Kila kanda ina mila na desturi zake kwa mfano chama cha wachaga wana mila zinazokazia marehemu asafirishwe akazikwe Moshi kijijini, kanda zingine unakuta hiyo sio issue sana,anazikwa popote.
 
CHAMA CHA KUFA NA KUZIKANA ndiyo mmdudu gani tena huyo Mkuu? Huwa siendekezi sana masuala ya ukanda na ukabila, kama mtu ni kabila langu tukikutana tunachat tu haina haja ya kuwa na chama. Chama pekee ni jamii inayonizunguka, marafiki zangu ndiyo ndugu zangu wa kufa na kuzikana. Kwetu ni mbali sana na ninapoishi, lakini nipo na amani ya kudumu.
 
Mkuu, Kanda ya kaskazini! Natanguliza shukurani katika hili.
 
Mkuu, Kanda ya kaskazini! Natanguliza shukurani katika hili.

Mkubwa,
Pia, kwa kuwa wewe ni mwanajamvi wa JF, napenda nikufahamishe kuwa hapa Arusha kuna umoja wa wana-JF, ambapo tuna katiba na fund inayo'serve purpose kama unavyohitaji. karibu sn, tuma PM kama utakuwa interested.
 
CHAMA CHA KUFA NA KUZIKANA ndiyo mmdudu gani tena huyo Mkuu? Huwa siendekezi sana masuala ya ukanda na ukabila, kama mtu ni kabila langu tukikutana tunachat tu haina haja ya kuwa na chama. Chama pekee ni jamii inayonizunguka, marafiki zangu ndiyo ndugu zangu wa kufa na kuzikana. Kwetu ni mbali sana na ninapoishi, lakini nipo na amani ya kudumu.

nimeipenda hiyo.congr
 
Dah kumbe humu JF tuna watoto sana eti mtu hajui chama cha 'maafa' huyo bwana anayeomba aelekezwe anaonekana ni mtu mzima mwenye majukumu, na ndio maana haulizii chama cha starehe kama ulivyotaka mkuu Amoeba, we bado mdogo sana hujapatwa na matatizo. Mkuu Ntu ntaku-pm kukuelekeza ofisi ya umoja huo.
 
Shurani sana Mkuu!!!
 
Back
Top Bottom