Kwa wenye mtaji kuanzia 50,000/- tuungane tuwekeze katika hili

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Habari wakuu,twende katika hoja.

Napendekezo la kushirikisha wadau wenye mitaji kuanzia 50,000/- na kuendelea tuungane katika uwekezaji katika mradi wa nishati inayo tembea (mobile energy).

Project ambazo nitaziwakilisha hapa tayari binafsi nimesha zijaribu na kuona kuna fursa lakini pia marrjesho ya uhakika ya kiuchumi.

1.MRADI WA MTAMBO WA KUENDESHA MASHINE YA KUNYOLEA (MOBILE BARBER) INAYO TUMIA MFUMO WA SOLAR (mradi huu umesha jaribiwa na unaweza kuhakikiwa).

Mitambo inayotunza umeme ambayo itatumika katika kuendesha mashine za kunyolea maeneo ya vijijini.

Mtambo huu unakuwa unaweza kubebeka katika baiskeli,ambapo kijana wa kunyoa anakabidhiwa vifaa vifuatavyo

i.Mtambo wenyewe
ii.Baiskeli
iii. Vifaa vya kunyolea (mashine,kioo,dawa n.k)

UTENDAJI WA KIBIASHARA.
Kijana anakua akitembea na baiskeli katika kaya mbalimbali kutoa huduma ya kunyoa,ambapo anakuwa na uwezo wa kutembelea vijiji vya jirani ili kutoa huduma hiyo.

Pia atakuwa akitumia mikusanyiko ya minada,mashule na vilabu vya pombe kutoa huduma hiyo.

UPATIKANAJI WA KIJANA WA KUNYOA.

Kwa majaribio nilio fanya katika vijiji hua kuna vijana ambao wananyoa kwa kutumia vitana na wembe,mara nyingi hao ndiyo huwa wanafahamiana na wateja wengi wa kunyoa wa maeneo hayo na pia hao huwa rahisi kufundishika kutumia mashine ya umeme kunyoa.

Baada ya kumpata kijana huyo mnakubaliana katika malipo na mnaenda kukabidhiana na kuandikishiana katika ofisi ya kijiji ambayo huyo kijana ni mkazi.

Baada ya hapo unamkabidhi baiskeli na mtambo na vifaa vyake.

GHARAMA ZA MTAMBO MMOJA.

i. Mtambo na mashine yake ya kunyolea jumla ni 620,000/-
ii. Baiskeli 150000
iii.Vifaa vingine 30000

JUMLA Tsh 800,000/-

MAPATO NA MFUMO WA KUYAKUSANYA.

Mtambo huu umewekwa kifaa ambacho kinapima matumizi ya mtambo kwa masaa.

Jinsi mashine inavyofanya kazi ndivyo kipimo kinavyo soma,Kwa mashine moja ya kunyolea kipimo kitasoma point 1 baada ya mashine ya kunyolea kufanya kazi kwa masaa masaa 10,na point 2 baada ya masaa 20 na itaendelea hivyo hivyo kulingana na masaa.

Siyo lazima mashine ifanye kazi kwa masaa 10 mfululizo hapana hata kama inawashwa na kuzimwa mfano.

Mteja wa 1:kanyolewa dakika 45
2:Kanyolewa dakika 30
3:Kanyolewa lisaa 1

JUMLA itakua masaa 2 na dakika 15,hivyo itakua bado masaa 7 na dakika 45 kutimia masaa 10.

Baada ya kutimiza masaa 10 ya kazi kipimo kitaandika point .

Hivyo makubaliano ya malipo yatakuwa kulingana na pointi ikiwa na maana unaweza kukadilia kila lisaa 1 la kazi iwe unalipwa 1000/= kwa masaa 10 ya kazi utalipwa 10,000/=

Mita ya malipo itasoma muda pale tu wakati mashine ya kunyolea imewashwa. Na itasimama mashine ya kunyolea ikizimwa.

Hivyo kutokana na mfumo huu ni rahisi kufatilia malipo na kuepuka udanganyifu.

Unaweza ukawa unakusanya malipo yako baada ya kila pointi kadhaa ukijua kabisa kila pointi 1 ni sawa 10000 n.k

MAJARIBIO YA MASHINE NA WAZO LA MRADI.

Baada ya kuunda mashine hii niliitangaza hapa kwa kuiuza ila wadau wengi walionekana kuto zingatia sana sababu ni kitu kipya na baadhi wakawa waoga kujaribu.

Hivyo nikachukua jukumu la kuipeleka mashine field na kuangalia utendaji wa kazi na marejesho.

Kuna kijiji kipo wilaya ya kisarawe mkoa wa Pwani ambapo Mashine imepelekwa kule ambapo nikapata msimamizi na kinyozi.

Wastani wa mapato kwa wiki ni Tsh 50000

- Ambapo siku za minada ananyoa hadi 17,000/- kwa bei ya mkubwa 1000 mtoto 500. Ambapo kwa kule minada ni siku 2

Na siku za kawaida ananyoa kati ya 7000 hasi 10000 kati ya vijiji viwili hadi vitatu anavyo tembelea.

Tulivyo kubaliana kinyozi anachukua asilimia 40 ya mapato
Na mwenye mashine anachukua asilimia 60 ya mapato.

Hivyo kinyozi anachukua 2800 kwa siku sawa na 20000 kwa wiki sawa na 85000 kwa mwezi.

Mwenye mashine atachukua 4200 kwa siku sawa na 30000 kwa wiki sawa na 128000 kwa mwezi.

Uchangamfu na speed ya kinyozi,mazingira ya mabonde na milima,na idadi ya watu,idadi ya kaya,uwepo wa shule vinaweza kuathiri makadilio haya chanya au hasi.

Hivyo nashauri wadau ambao wanalengo la kuthubutu tujiunge tutengeneze kikundi,cha mradi huu.

Wadau tukutane tujuane tujue tunaweza kuwekeza kiasi gani,tutembelee kule ambako mashine ya majaribio imewekwa kwa uhakika na kujifunza zaidi.

Ikionekana tija ya jambo hili tunaweza unda uongozi wa kikundi tukafungua akaunti ya kikundi na watu wakaamua kuwekeza katika mradi huu.

UPDATE

WHATSUP LINK
......................

.................

PhotoEditor_20190719_213714538.jpg

Kwa maelezo ya miradi hii pakua pdf hii
 
Attachments

  • PhotoEditor_20190719_214446841.jpg
    PhotoEditor_20190719_214446841.jpg
    168.7 KB · Views: 36
  • Mobile energy.pdf
    25.2 KB · Views: 34
Biashara kichaa yaani uwekezaji wa 800,000/= pia kuna process ndefu naiyo process yenyewe iwe imekamilika faida 120,000/= kwamwezi.

Biashara ya uwekezaji wa 1M+ faida 180,000/= tena kwa process ndefu na iyo process yenyewe iwe imekamilika.

Huwo mtambo hauna faida unless ukae chini kufanya reserch tena utakuwezesha vipi kuingiza pesa.
 
Hahaa Eti process ndefu....hata hivyo asante kwa wazo mkuu
 
Inahusu nini si ungeweka wazi hapa hapa ili ambaye haimuhusu anakuwa anapita unataka kila mtu mpaka aanze kupakua pakua vitu tena ukute hakuna mchongo wowote unamuhusu
Hiyo hapo mkuu...mawazo tanahitajika
 
Habari wakuu,twende katika hoja.

Napendekezo la kushirikisha wadau wenye mitaji kuanzia 50,000/- na kuendelea tuungane katika uwekezaji katika mradi wa nishati inayo tembea (mobile energy).

Project ambazo nitaziwakilisha hapa tayari binafsi nimesha zijaribu na kuona kuna fursa lakini pia marrjesho ya uhakika ya kiuchumi.

1.MRADI WA MTAMBO WA KUENDESHA MASHINE YA KUNYOLEA (MOBILE BARBER) INAYO TUMIA MFUMO WA SOLAR (mradi huu umesha jaribiwa na unaweza kuhakikiwa).

Mitambo inayotunza umeme ambayo itatumika katika kuendesha mashine za kunyolea maeneo ya vijijini.

Mtambo huu unakuwa unaweza kubebeka katika baiskeli,ambapo kijana wa kunyoa anakabidhiwa vifaa vifuatavyo

i.Mtambo wenyewe
ii.Baiskeli
iii. Vifaa vya kunyolea (mashine,kioo,dawa n.k)

UTENDAJI WA KIBIASHARA.
Kijana anakua akitembea na baiskeli katika kaya mbalimbali kutoa huduma ya kunyoa,ambapo anakuwa na uwezo wa kutembelea vijiji vya jirani ili kutoa huduma hiyo.

Pia atakuwa akitumia mikusanyiko ya minada,mashule na vilabu vya pombe kutoa huduma hiyo.

UPATIKANAJI WA KIJANA WA KUNYOA.

Kwa majaribio nilio fanya katika vijiji hua kuna vijana ambao wananyoa kwa kutumia vitana na wembe,mara nyingi hao ndiyo huwa wanafahamiana na wateja wengi wa kunyoa wa maeneo hayo na pia hao huwa rahisi kufundishika kutumia mashine ya umeme kunyoa.

Baada ya kumpata kijana huyo mnakubaliana katika malipo na mnaenda kukabidhiana na kuandikishiana katika ofisi ya kijiji ambayo huyo kijana ni mkazi.

Baada ya hapo unamkabidhi baiskeli na mtambo na vifaa vyake.

GHARAMA ZA MTAMBO MMOJA.

i. Mtambo na mashine yake ya kunyolea jumla ni 620,000/-
ii. Baiskeli 150000
iii.Vifaa vingine 30000

JUMLA Tsh 800,000/-

MAPATO NA MFUMO WA KUYAKUSANYA.

Mtambo huu umewekwa kifaa ambacho kinapima matumizi ya mtambo kwa masaa.

Jinsi mashine inavyofanya kazi ndivyo kipimo kinavyo soma,Kwa mashine moja ya kunyolea kipimo kitasoma point 1 baada ya mashine ya kunyolea kufanya kazi kwa masaa masaa 10,na point 2 baada ya masaa 20 na itaendelea hivyo hivyo kulingana na masaa.

Siyo lazima mashine ifanye kazi kwa masaa 10 mfululizo hapana hata kama inawashwa na kuzimwa mfano.

Mteja wa 1:kanyolewa dakika 45
2:Kanyolewa dakika 30
3:Kanyolewa lisaa 1

JUMLA itakua masaa 2 na dakika 15,hivyo itakua bado masaa 7 na dakika 45 kutimia masaa 10.

Baada ya kutimiza masaa 10 ya kazi kipimo kitaandika point .

Hivyo makubaliano ya malipo yatakuwa kulingana na pointi ikiwa na maana unaweza kukadilia kila lisaa 1 la kazi iwe unalipwa 1000/= kwa masaa 10 ya kazi utalipwa 10,000/=

Mita ya malipo itasoma muda pale tu wakati mashine ya kunyolea imewashwa. Na itasimama mashine ya kunyolea ikizimwa.

Hivyo kutokana na mfumo huu ni rahisi kufatilia malipo na kuepuka udanganyifu.

Unaweza ukawa unakusanya malipo yako baada ya kila pointi kadhaa ukijua kabisa kila pointi 1 ni sawa 10000 n.k

MAJARIBIO YA MASHINE NA WAZO LA MRADI.

Baada ya kuunda mashine hii niliitangaza hapa kwa kuiuza ila wadau wengi walionekana kuto zingatia sana sababu ni kitu kipya na baadhi wakawa waoga kujaribu.

Hivyo nikachukua jukumu la kuipeleka mashine field na kuangalia utendaji wa kazi na marejesho.

Kuna kijiji kipo wilaya ya kisarawe mkoa wa Pwani ambapo Mashine imepelekwa kule ambapo nikapata msimamizi na kinyozi.

Wastani wa mapato kwa wiki ni Tsh 50000

- Ambapo siku za minada ananyoa hadi 17,000/- kwa bei ya mkubwa 1000 mtoto 500. Ambapo kwa kule minada ni siku 2

Na siku za kawaida ananyoa kati ya 7000 hasi 10000 kati ya vijiji viwili hadi vitatu anavyo tembelea.

Tulivyo kubaliana kinyozi anachukua asilimia 40 ya mapato
Na mwenye mashine anachukua asilimia 60 ya mapato.

Hivyo kinyozi anachukua 2800 kwa siku sawa na 20000 kwa wiki sawa na 85000 kwa mwezi.

Mwenye mashine atachukua 4200 kwa siku sawa na 30000 kwa wiki sawa na 128000 kwa mwezi.

Uchangamfu na speed ya kinyozi,mazingira ya mabonde na milima,na idadi ya watu,idadi ya kaya,uwepo wa shule vinaweza kuathiri makadilio haya chanya au hasi.

Hivyo nashauri wadau ambao wanalengo la kuthubutu tujiunge tutengeneze kikundi,cha mradi huu.

Wadau tukutane tujuane tujue tunaweza kuwekeza kiasi gani,tutembelee kule ambako mashine ya majaribio imewekwa kwa uhakika na kujifunza zaidi.

Ikionekana tija ya jambo hili tunaweza unda uongozi wa kikundi tukafungua akaunti ya kikundi na watu wakaamua kuwekeza katika mradi huu.

Kusoma zaidi kuhusu mtambo huu bonyeza link hii

View attachment 1210881

Kwa maelezo ya miradi hii pakua pdf hii
am in mkuu, niweke kwenye kikundi tupeleke kusini mwa Tanzania hii kitu.
 
Mbona MTU anaeeza soma kwa Mamilioni but akianza kazi analippwa kidogo?.
Point hapa ni kwamba hicho kifaa ni cha kudumu.Haijalishi umenunua kiasi gani but kitakuwepo labda kiibiwe..
Pia mfano mzuri MTU anaweza jenga Nyumba yake kwa mapesa mingi Mingi mfano Flem za Nyumba.Unakuta ni sh.Elfu 50 tu kwa mwezi why kwa sababu kile kitu kipo na Ndo uwekezaji kwa long term.
Biashara kichaa yaani uwekezaji wa 800,000/= pia kuna process ndefu naiyo process yenyewe iwe imekamilika faida 120,000/= kwamwezi.

Biashara ya uwekezaji wa 1M+ faida 180,000/= tena kwa process ndefu na iyo process yenyewe iwe imekamilika.

Huwo mtambo hauna faida unless ukae chini kufanya reserch tena utakuwezesha vipi kuingiza pesa.
 
Asante kwa mchango umeafafanua vizuri sana.....hii ni fursa kubwa sana sema ni vile tumezoea kuwekeza katika vitu tulivyo zoea au kuona watu wanafanya.

Tujaribu katika hili sababu mashine ni ya kudumu na pia haitumii nishati ya kuunua inatumia nishati ya jua ukiwa nayo wewe unachosubiri ni marejesho tu.

Vijijini huko fursa hii ni kubwa sababu kule mtu anasafiri kwa gharama kwenda kufata saluni tu sasa kama tutaweza kuwafikishia huduma jirani nadhani ni kitu kizuri mi nadhani kujaribu so vibaya

Mi naami tutaanza kama kundi ila tunako enda kila mtu atataka awe nayo yake.

Mimi tayari ninayo hiyo moja na nimeona faida nilitamani niwe na mtaji niunde hata mia ila ndo hivyo.

Na mtu akitaka kuthibitisha aende pale kisarawe kijiji cha vikumburu mashine ipo pale kuna kijana anazunguka nayo vijiji vya jirani

Kutoka dar hadi kijijini hapo ni 6000 tu.

Mbona MTU anaeeza soma kwa Mamilioni but akianza kazi analippwa kidogo?.
Point hapa ni kwamba hicho kifaa ni cha kudumu.Haijalishi umenunua kiasi gani but kitakuwepo labda kiibiwe..
Pia mfano mzuri MTU anaweza jenga Nyumba yake kwa mapesa mingi Mingi mfano Flem za Nyumba.Unakuta ni sh.Elfu 50 tu kwa mwezi why kwa sababu kile kitu kipo na Ndo uwekezaji kwa long term.
 
Changamoto nayo ona ni hao vijana huko kijijini watakuwa na uaminifu gani ili kuhakikisha unapata hesabu yako kwa wakati?.
 
Pia ni kitu cha kushauriana hicho japo mimi sijapata hiyo changamoto ila inaweza kujitokeza kwa baadhi ya vijana kwasababu si wote waaminifu.

Nadhani watakao kuwa wanahusika na kitengo cha ukusanyaji mapato itabidi waje na solution ya hili.
 
Pia kipindi cha mafunzo ya vijana hawa ni muhimu kuwapa nao elimu kidogo ya ujasiriamali ili wajue ile ni ajira pia ni ni msaada kwao,na familia.

Elimu duni ya ujasiriamali inaweza pia pelekea mtu asiwe mwaminifu kwa kitu chake mwenyewe.
 
Sijawaikuamini katika kikundi lazima wazinguaji wawepo tuuh
Kampuni au taasisi yoyote ni kikundi...tunaomba ushauri jinsi gani unadhani tutaboresha ili uzinguaji usiwepo vitu kama akaunti ya benk,wahasibu wakusanya mapato na ukaguzi wa miamara ni vitu vya kuzingatia.

Sababu peke yako pekeyako pia ni ngumu kama mtaji ni mdogo labda kama unaweza kikopa benk.

Tupe ushauri katika hili
 
Biashara kichaa yaani uwekezaji wa 800,000/= pia kuna process ndefu naiyo process yenyewe iwe imekamilika faida 120,000/= kwamwezi.

Biashara ya uwekezaji wa 1M+ faida 180,000/= tena kwa process ndefu na iyo process yenyewe iwe imekamilika.

Huwo mtambo hauna faida unless ukae chini kufanya reserch tena utakuwezesha vipi kuingiza pesa.
Acha dharau mkuu
 
Sawa Asante mkuu tutarejea kwa wadau wote ambao wako tayari na tutaunda group la watsup ili tuanzie kujuana hapo na baadae tutakutana uso kwa uso kwa majadiliano zaidi na kupanga mkakati wa kibiashara kugawana majukumu na kujua namna ya kupata kibali cha kufungua akaunti ya mradi.

Kwa wa mikoani nao watakutana huko na tutapata marejesho kupitia group na tutajua tuanze na mikoa ipi vijiji vipi na mashine ngapi ambazo zitaashiria ajira ngapi zitatolewa za moja kwa moja.
Am in mkuu nicheki pm 50 ipo
 
Tayari ambao wako ndani ni watatu ukijumuisha na mimi mwenyewe.

Hivyo tuna 150,000/- Ahadi bado 650,000/-Tupate mashine moja na vifaa vyake.

Ambapo tutakuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa kijana 1.

Tuendelee kusapoti wazo wadau au kama kuna ushauri na maoni yanahitajika.
 
Back
Top Bottom