Kwa wenye mitaji tunaingia msimu wa kahawa

Kwa wenye mitaji tunaingia msimu wa kahawa

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,244
Reaction score
7,723
Nipo mbeya vijijini kwa sasa ni msimu wa kuvuna maharage. Kuanzia mwezi wa nne, tunaanza kuvuna zao la kahawa.

Nimeona kuna watu wengi wanaojihusisha na ununuaji wa kahawa mbichi (cherry) na kavu.

Nimekuja kwenu baada ya kufanya utafiti wa biashara hii. Hii biahsara ina faida kwa wenye mitaji ambao watanunua kahawa mbichi na kuisaga kisha kuianika.

Sasa basi, mimi nimekuja hapa kutangaza fursa kwa wenye mitaji ili tufanye biashara hii. Eneo la kufanyia huo uwekezaji lipo kwa kuanzia msimu huu wakati tunajipanga kwa misimu ijayo.

Kama una mtaji na unaona inafaa, tunaweza kuwasiliana na mimi nitasimama kama wakala kwa eneo hili na tutakamilisha taratibu zote za kisheria ili tuweze kufanya kazi hii.

Karibuni sana. Kwa mawasiliano ya simu, sms au whatsap 0752343579
 
Mkuu weka bei za maharage ya soya gunia shingap?? Tufanye biashara
 
Nasikiaga Ile kahawa ya bukoba Iko vizur Kuna mtu yupo uingereza aliniambia wanauhitaj sana na kahawa na Ile ya bukoba Iko vizur
 
Kahawa nzuri yenye international grade ipo Bukoba
Na huko ndipo kuna uwekezaji mkubwa, Traders wengi wa ndani na nje ya nchi wanamiminika sana Bukoba

Ila kama Mbeya napo mnauzalishaji mzuri basi tutatia timu
 
Nasikiaga Ile kahawa ya bukoba Iko vizur Kuna mtu yupo uingereza aliniambia wanauhitaj sana na kahawa na Ile ya bukoba Iko vizur
Hilo ni kweli kabisa,
wakulima wa kahawa wa mkoa kagera bado wanatumia mbolea ya wanyama na nyasi kavu
wakati wakulima wengi wa kusini wanatumia mbolea za viwandani,kwa wazungu wanapenda sana mazao yanayotumia mbolea za asili kuliko za viwandani.
 
Back
Top Bottom