Kwa wenye mapenzi mema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wenye mapenzi mema

Discussion in 'Matangazo madogo' started by kitalolo, May 19, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Saidi watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, vvu na yatima.

  kituo cha Santa maria kilichopo Arusha moivaro kinakukaribisha kuchangia chakula, mavazi fedha taslimu kwaajili ya watoto wanaotuzwa na kupatiwa elimu katika kituo chetu.

  kituo hiki kilianzishwa 5/1/2012 na Ngugu Collins Daniel kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, kuwapatia elimu na ushauri, kina jumla ya watoto 23 hadi kufikia sasa.

  Kituo kina mahitaji ya Chakula, Nguo pamoja na uniform za shule, madaftari, vitabu, kalamu, penselina viti au madawati.

  watoto waliopo kituni hadi sasa ni wa umri kati ya miaka miwili na nusu hadi minne

  Mchango wako sio laizma uwe wa fedha taslimu bali unaweza kuchangia chochote kati ya mahitaji hayo tuliyoainisha hapo juu.

  Kwa michango ya fedha itawezesha kusaidia kulipa kodi ya pango, kulipa mishahara ya waalimu, pamoja na mahitaji mengine.

  wasiliana nasi kwa simu nambari 0754 3393449/ 0769077910 /0784 988881 Au unaweza kufika kituoni Moivaro barabara ya kwenda moivaro lodge.

  michango inaweza kutumwa kwa Mpesa kwa namba tajwa hapo juu au kufikisha mchango wako katika kituoni au kwa akaunti namba 020121026095 KCB Banki Jina la akaunti Collins Daniel Makau.

  ASANTENI SANA PAMOJA TUNAWEZA KUWASAIDIA WATOTO NA KUWAPATIA ELIMU ILI WAWEZE KUJITEGEMEA NA KULIJENGA TAIFA LETU
   
Loading...