Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
here we go again lol
Mkuu kale kabinti kako hujakavalisha?
here we go again lol
wanavisha watoto wa kike kiunoni kwa mtoto wa kike ili kinuo kipate 'Figure',kweli yote haya nafanywa kwa imani na ni watu wa aina fulani bado wanawafunga watoto wao ,lakini kwa wasomi hawana imani hiyo.
Ashukuriwe MUNGU mambo hayo sikupitia. Meno mengi niliyatupa sana sana ilikuwa ni chooni (cha shimo) na kwa habari ya Kwikwi mara nyingi tuliambiwa tunywe maji au kubana pumzi. Sina uhakika kitabibu kama ndivyo inavyotakiwa kufanyika but somehow it works for me! lol!
Mkuu Matola......vipi anayevaa cheni ya dhahabuMimi Mwanamke anayevaa shanga simtaki sembuse ndio uniambie mtoto wangu avalishwe hizo kamba za kishirikina? ujinga mtupu.
Usinipeleke huko tafadhali, kuna imani za kigaidi zimeshaingia nchini kwetu. nilichosema mimi Mwanamke wangu kuvaa shanga marufuku hayo mengine ni ya kwako usinirishe maneno.Mkuu Matola......vipi anayevaa cheni ya dhahabu
Mshirikina ni yupi kati ya anayevaa kamba hii......anayetembea na tasbihi au anayevaa rozari????
Aghalabu mjinga ni yule asiyejua maana ya kitu na bado akadhani anachoelewa yeye ni sahihi kuliko vya wengine...a na akahukumu kwa vigezo vyake na si uhalisia wa muda wala sehemu husika....kwani hayuko tayari kuhoji na kutambua wanavyoelewa wenzake hata kama ni tofauti na anavyoelewa yeye....anaitwa ethnocentric
ule ni uchawi.Naomba kuuliza wanaJamvi wenye watoto. Zile kamba nyeusi wanazovalishwa watoto wadogo viunoni na wakati mwingine kwenye mikono huwa zina kazi gani? Mungu akijalia nikaja kupata mtoto na mke wangu, nisipomvalisha mwanangu hiyo kamba atapatwa na madhara gani?
If so why is it still applicable up to date wakati clinic zimezagaa kila kata, ukweli bado unaonesha kua kuna imani flani ina exist ktk kutumia hivyo vikambaenzi za zamani haikuwa rahisi mzazi kupima uzito wa mtoto wake klinik mara kwa mara.
Kamba ile nyeusi anayovalishwa mtoto kiunoni na au mkononi, ilikuwa ni katika kusaidia kupima ukuaji wa mtoto.
Kama ikiendelea kumbana mtoto, mzazi anajua mtoto anendelea vema, ila kama ikianza kupwaya, anajua kuna shida mahala.
Pia katika kamba hizo, kuna baadhi ya mila wanazitengenezea pamoja na kitovu cha mtoto, sijawahi kujua kwa nini.
Ila siamini kama kuna ushirikina hivyo, halafu kamba kuwa nyeusi nsdhani ni pamoja na kuficha uchafu ama rangi kubadilika ukilinganisha na rangi zingine.
Sasa hivi hata usipotumia kamba, klinik zipo kwa wingi.