Kwa Wazazi Tu!

Kwa Wazazi Tu!

Sumu

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
7,015
Reaction score
6,246
Naomba kuuliza wanaJamvi wenye watoto. Zile kamba nyeusi wanazovalishwa watoto wadogo viunoni na wakati mwingine kwenye mikono huwa zina kazi gani? Mungu akijalia nikaja kupata mtoto na mke wangu, nisipomvalisha mwanangu hiyo kamba atapatwa na madhara gani?
 
Mimi nina mtoto na hawajahi kuvaa kitu kama hicho na hakuna madhara yoyote yale aliyoyapata.

Hizo ni imani za watu, mara nyingi wafanyao hivyo huwa na imani kwamba hizo dawa ni kinga za magonjwa.
 
Kwa asilimia kubwa mambo hayo huambatana na imani za kishirikina. Tangu lini kucha na mavi ya tembo yakamponya mtoto?
 
ni hirizi tu zile, hazina lolote, tena vitoto vinavyovaa vingi unakuta vina utapiamlo na vimekondeana. . .yaani hamna lolote kwenye hivyo vi hirizi
 
enzi za zamani haikuwa rahisi mzazi kupima uzito wa mtoto wake klinik mara kwa mara.

Kamba ile nyeusi anayovalishwa mtoto kiunoni na au mkononi, ilikuwa ni katika kusaidia kupima ukuaji wa mtoto.

Kama ikiendelea kumbana mtoto, mzazi anajua mtoto anendelea vema, ila kama ikianza kupwaya, anajua kuna shida mahala.

Pia katika kamba hizo, kuna baadhi ya mila wanazitengenezea pamoja na kitovu cha mtoto, sijawahi kujua kwa nini.

Ila siamini kama kuna ushirikina hivyo, halafu kamba kuwa nyeusi nsdhani ni pamoja na kuficha uchafu ama rangi kubadilika ukilinganisha na rangi zingine.

Sasa hivi hata usipotumia kamba, klinik zipo kwa wingi.
 
Kwa asilimia kubwa mambo hayo huambatana na imani za kishirikina. Tangu lini kucha na mavi ya tembo yakamponya mtoto?

Eeeh! Kumbe zinakuwa ni kucha na mavi ya tembo? That's weird. Ahsante kwa kunijulisha.
 
ulivyotoka meno utotoni, ulirusha juu ya bati au uliweka chini ya mto??

Au ulipopata kwikwi walikuwekea uzi mweupe kwenye paji la uso??

Ni zaidi ya hapo kuna mambo mengi ambayo mengine hayafai hata kutamkwa yanayofinyangwa ndani ya vile vihirizi vidogo na kamba nyeusi viunoni mwa watoto! Tahadhari tu, USIJARIBU!
 
ulivyotoka meno utotoni, ulirusha juu ya bati au uliweka chini ya mto??

Au ulipopata kwikwi walikuwekea uzi mweupe kwenye paji la uso??

Ashukuriwe MUNGU mambo hayo sikupitia. Meno mengi niliyatupa sana sana ilikuwa ni chooni (cha shimo) na kwa habari ya Kwikwi mara nyingi tuliambiwa tunywe maji au kubana pumzi. Sina uhakika kitabibu kama ndivyo inavyotakiwa kufanyika but somehow it works for me! lol!
 
okay, hivi vilifanya kazi kwako lakini kuna vingine vinafanya kazi hizo hizo kwa wengine.

Ashukuriwe MUNGU mambo hayo sikupitia. Meno mengi niliyatupa sana sana ilikuwa ni chooni (cha shimo) na kwa habari ya Kwikwi mara nyingi tuliambiwa tunywe maji au kubana pumzi. Sina uhakika kitabibu kama ndivyo inavyotakiwa kufanyika but somehow it works for me! lol!
 
Ni zaidi ya hapo kuna mambo mengi ambayo mengine hayafai hata kutamkwa yanayofinyangwa ndani ya vile vihirizi vidogo na kamba nyeusi viunoni mwa watoto! Tahadhari tu, USIJARIBU!

Kama mambo yenyewe ndo hayo, siwezi kujaribu.
 
wee naye kiazi cha chipsi.

Kasema wanaweka vitu vingi vikorkoro, afu unajibu kama ni hivyo siwezi hata kujaribu.

Ingredients za vikokoro ni nini hadi umekonkludi huwezi?

Vipi mkuu? Hayo maswala ya kiazi cha chipsi yanahusiana vipi na huu uzi? Kwani tunagombana au tunaeleweshana? Natarajia kupata mtoto huko mbele ya safari ndo maana nikauliza ili nijue na kulingana na comments inaonekana hili jambo lina uhusiano na ushirikina. Nieleweshe nitakuelewa, sikuuliza ili tusutane. NATAKA KUJUA FOR THE SAKE OF MY CHILDREN.
 
Hivyo vitu vinatumika sana maeneo ya Pwani walikojazana akina naniiiiii, aahh nimesahau kidogo. Wakati fulani nilieenda Kisiwa cha Mafia huko ndiyo balaa kabisa. Kila mtoto niliyekutana nae barabarani alikuwa na kamba mkononi na shingoni. Inawezekana hata kiunoni zilikuwepo, you never know!
 
enzi za zamani haikuwa rahisi mzazi kupima uzito wa mtoto wake klinik mara kwa mara.

Kamba ile nyeusi anayovalishwa mtoto kiunoni na au mkononi, ilikuwa ni katika kusaidia kupima ukuaji wa mtoto.

Kama ikiendelea kumbana mtoto, mzazi anajua mtoto anendelea vema, ila kama ikianza kupwaya, anajua kuna shida mahala.

Pia katika kamba hizo, kuna baadhi ya mila wanazitengenezea pamoja na kitovu cha mtoto, sijawahi kujua kwa nini.

Ila siamini kama kuna ushirikina hivyo, halafu kamba kuwa nyeusi nsdhani ni pamoja na kuficha uchafu ama rangi kubadilika ukilinganisha na rangi zingine.

Sasa hivi hata usipotumia kamba, klinik zipo kwa wingi.

wanavisha watoto wa kike kiunoni kwa mtoto wa kike ili kinuo kipate 'Figure',kweli yote haya nafanywa kwa imani na ni watu wa aina fulani bado wanawafunga watoto wao ,lakini kwa wasomi hawana imani hiyo.
 
Sikuvalishwa nilivyokuwa mdogo!

Source: My dad (may he R.I.P)

My sonushka hajavaa

Source: Mimi

Na hatuna tofauti na watu wengi wa kawaida!
 
sikuvalishwa.......

Na kumbuka sista alirudi na mtoto (aliolewa na mtu wa tanga na mumewe alikuwa huko kikazi) kapigiliwa ya kiunoni na mkononi....bibi alimwambia yeye hakuwahi kuvaa na hakuwahi valisha wanae 8 hayo madude.. Mama alichukua mkasi akayakata na kutupa chooni

inasemakana wanatia mavi ya tembo wakiamini ni dawa kutokana na majani anayokula tembo...

Wanangu pia sijawahi kuwavyesha hayo madude....

Ni ushirikina na tu....naonaga haswa makabila ya pwani ndo wanavalisha watoto
 
Waislamu wengi wanavalishwa na mnaona jinsi wasivyokuwa waoga katika kudai haki zao,mf Sheikh Ponda,nyie msiovalishwa tunaona tofauti yenu mnapenda kusemea chini ya uvungu.
 
Back
Top Bottom