Kwanza niseme maelezo yako hayajijitosheleza, umezikonect vipi hizo PC? Connection zifanyike kwa Linux maana yake nini? I.P ya tatu ni nini?
Anyway hizo I.P ulizoweka zipo kwenye network tofauti, hiyo mask 255.255.255.0 maana yake octet 3 za kwanza za 192.168.1.2 na 192.168.2.2 ni za network(subnet) na octet ya mwisho ndo ya hosts(PC) hivyo haziwezi kuonana unless kuwe na routing kati yake.
Weka IP 192.168.1.2, 192.168.1.3, 192.168.1.4, mask ile ile na hizo mashine zote zitakuwa subnet moja na kuonana.