Jua Jinsi ya Kutroubleshoot Your network

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Ndugu wana Jambo Forums,katika kuhakikisha kuwa kila mutu anakuwa na ufahamu hata kwa kiwango kiduchu nimeamua kuandaa kama kaprogram ambacho kila week nitakuwa nawaleteeni katopic ambacho nina imani katakuwa kanasaidia baadhi ya watu.
Leo hii ninakuja na jinsi ya kutroubleshoo your Network.
Ni maranyingi watu huwa wanapatwa na matatizo kama haya na wasijue ni nini la kufanya na wao huona njia ya kwanza ni kukimbilia kupiga simu kwa Internet Service Provider(ISP) au kumuita IT Specialist na jamaa wakija maranyingi atakuambia unajua sijui NIC yako imekufa ooh sijui kuna stack haziendani inabidi nikakununlie mpya na mambo kibao ili mradi akuchukue kitu.So leo ninakupa technics ambazo unaweza kujua tatizo lipo wapi kabla ya kumuita huyo ISP au IT manager wako.
Unapoona huwezi kuaccess Internet/internet/intranet kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuwa ni sababu za kukusababisha wewe ushindwe kuaccess hizo service sasa nitakuelezea technics nne ambazo ni recomended(kwa watu wanaotumia Windows operating system tu) na causes zake na jinsi ya kuzirekebisha.
Kabla ya kufanya hivi unatakiwa kwanza ujue IP yako(Internet Protocol-Hapa nazungumzia kwa aina zote za Ip iwe IPv4 au IPv6 kwani kwa sasa nchi kama USA,JAPAN na CHINA wameshaanza kutumia new version of IP ambayo ni IPv6, nitakachambulieni ipasavyo katika mada zijazo),Default gateway(hii ni addres ya Router ambayo inakuconnect kwenda kwa ISP wako au Other LAN-kama hujui ni nini Router basi wewe isikuumize sana kichwa Router ni kifaa ambacho nikatumika kuprocess request toka network moja kwenda nyingine) TUANZE
Nenda kwenye start->run->andika cmd->itakotea kabox cheusi(ms DOS) andika ipconfig hii itakuletea IP yako na Default gateway yako so utaiandika pembeni then ukiwa bado upo kwenye hicho kadude cheusi(ms DOS) utaanza kutroubleshoot your internet kwa kufanya hizi process nne.
1.Ukiwa katika DOS,andika ping AAA.BBB.CCC.DDD(hapa namaanisha utaandika Hiyo IP yako uliyoiona baada ya kuandika ipconfig kwa mfano mimi Ip yangu ni 192.168.10.12 so nitaandika ping 192.168.10.12 sasa hapa kuna option mbili ikubali au ikatae kama ikikubali nenda step ya pili kama ikikataa basi hapa ndio wanga wakona inatakiwa uangalie IP configuration zako(nenda mynetworkplaces->right click->properties->utaona Local Area Network-LAN,iright click then chagua properties tena,utaona nyingi csroll hadi kwenye INternet protocol TCP/IP->left click(maranyingine inabidi udoubleclick) so hapo inabidi uangalie ni option gani imekuwa ticked na wewe unatumia service gani,kama ni Modem,iwe wireless au cable modem basi chagua Obtain IP automatic otherwise kwa wale wenzangu wa maofisini na mashuleni basi angalia angalia IP uliyopewa inaligana na hiyo hapo?? then hapo tumemaliza sehemu ya kwanza.kama bado tatizo nenda sehemu ya pili
2.andika ping 127.0.0.1 hii inaitwa loopback address ambayo inaangalia protocol stack(OSI Layers) katika computer zako ipo swafi.Hapa ninamaanisha kuwa kila Computer inakitu kinaitwa Network Interface Card(NIC) hiki kimeunganishwa pale unapochomeka nyaya ya net au kwa wireless kipo kwa ndani. sasa kama utaping hiyo 127.0.0.1 itakubali basi nenda step ya tatu la sivyo huyo anaweza kuwa ndio mchawi wako.so inabidi uangalie je hiyo kadi yako inafanya kazi,haijafa,je kama upo Shuleni au ofisini huyo IT manager wenu hatumii MAC stack(kuna kipindi katika kucontroll access control list unaweza kuconfigure kuwa ni computer moja tu inaweza pata access kwa kuangalia physical address-MAC)ukimaliza hayo yote na bado tatizo nenda step namba tatu
3.Andika ping defaultgateway nadha bado unakumbuka kama nilikuambia unatakiwa ucopy mahali hiyo IP na Default Gateway yako kwa mfano mimi defaule gateway yangu ni 192.168.10.1(mara nyingi hii inakuwa ni address ya kwanza katika kila subnet) so nitaandika ping 192.168.10.1 kumbuka hii ni kwangu mimi sio sawa na ile 127.0.0.1 ambayo ni moja na inafanana kwa watu wote duniani unless special casees ambazo ni beyond the scope kwa watu wengi.kama itakubali basi nenda step ya nne kama itagoma basi hapo ndio uchawi ulipo na fanya hivi so fanya hivi angalia kama waya wako wa Internet umeconnectiwa vzuri,kuna kale ka mwanga kanawaka pale unapounganisha waya wa network kwenye port ya PC au Laptop yako,kama ni wireless basi angalia je kale ka mwanga kanakoonesha connectivity kanawaka rangi ya kijani sio orange,kama hakuna kamwanga chochote hapa ndipo unaweza kumuita IT manager wako kwani inawezekana kuna open circuit,disconnectivity au la baada ya hapo kama ushasolve na bado huwezi kuaccess network nenda step namba nne.
4.nitaielezea kwa lugha nyingine ili watu wote waielewe la sivyo itakuwa ngumu,hapa andika hivi tracert www.jamboforums.com jambo forums.com ni mfano hapo unatakiwa uandike address inayogoma kufunguka,sasa kama itatrace successful inabidi uangalie mabo mawili 1.je hiyo Ip yako ni ipo kwenye valid range??(hii inabidi utafute wataalamu wa subnetting ila nitakuja katika mada hizi wiki zijazo) 2.Je hakuna overlapping of IP Address? kama itatrace UNsuccessful basi inawezekana hao jamaa server yao ipo down na unaweza kula pozi badala ya kuangaika kumuita Mtu akulie Michede yakokwani katika Networking tunatumia term inayoitwa Bandwidth kupima ni kiasi gani cha watu wanaoweza kuaccess on time katika the same throughput Ni kama traffic case,barabara ya mandela ni ngumu kuwa na mifoleni ya kizembe
ukilinganisha na barabara ya ubungo mwenge.
Kama Una maswali,maoni au ushauri usisite kunitumia kwenye e mail yangu 629489676@qq.com toka Uchinani-Kilongwe CCNA holder
 
Nimependa Ujio wako kwenye forum hii ya IT mkuu

Karibu sana for the past one month imekuwa imedolola sana.
Hii technologia naifatilia kwa makini sana..na imekuwa very helpfull kwenye kazi zangu..kama Extra skill.

Hii yote ni Jambo forum.Karibu sana mkuu.

Buswelu.
 
Siyo hapo tu,nipo njiani katika kukamilisha Maswala ya server ambapo nitatoka na website ambayo itakuwa ni Full swahili yaani nina maana ni kiswahili kwa asilimia mia moja ambayo itawawezesha watanzania wenye moyo kudownload baadhi ya software,vitabu,tutorial nk. Kwa sasa nipo kwenye masuala ya security kwani si unajua mambo ya security ndio baba wa IT.
Nilivyofika China kwa mara ya kwanza nilishangaa kuona window inauzwa kwa yuan nne(0.5 USD) na ukiingia online unaipata for free of charge,nikasema yebo.Sasa mimi nafikiri kama tutakuwa na kitu kama hiki kwetu Tanzania tutawasaidia vijana chipukizi ambao hatuna Vipato kuweza kupata access ya maswala.sasa kabla ya kutoka hapo nilikuwa naomba michango yenu wana JF especialy wale wenye utashi na IT hii sio Siasa kwa hali ya sasa ya TZ,mtazamo wa serikali yetu kwa sasa juu ya piracy nk ipo vp huko??
Asikuongopee mutu bila ya Piracy hatutoki na la muhimu ni---------------KUDUMISHA MATUMIZI YA KISWAHILI------------------------- Tutatumia kiswahili,so naomba michango nini tufanye,nini kiwepo na ninyi munaonaje??? Au tutakuwa tunawafanyia zambi wadhungu(hahahaha) kazi kwenu...
 
Karibu sana JF na hii post yako kwanza ni nzuri sana especialy ulichoonza nacho leo ni sahihi sana kwa sisi ambao tupo tunafanya kwenye ISP company ndio step ambazo tunawafanyie client kujua where the problem is whether is client side or ISP side.Big up.
 
Mkuu kilongwe,

Ahsante umeelezea vizuri sana na ni maelezo mafupi na sahihi.

Nasubiri sehemu yako ya nne ili twende sambamba.

Je unajifunza VPN na Telnet haya ni mambo ambayo yanasaidia sana suala la kuokoa muda.

Halafu je, unaweza kueleza kidogo kuhusu MikyMouse kwenye CGI na kwanini inawekwa hapo?
 
kama unaaccess ya ile IT forum ya Bongo nimegusia mambo ya VPN kule,kuhusu telnet siku hizi watu wanaprefer sana SSH(Secure Shell) kwani katika Telnet password na username zinafari kama Plain text ila kwenye SSH zinakuwa Encrypted so kwa watu wa kati inakuwa ngumu.kwa product za CISCO za sasa zote zina hiyo option so hakuna tena haja ya Kutumia TELNET(hahaha) si unajua mambo ya Technolojia kila cku mpya. By the wayu Ttutaonana kwenye next topic....
 
Hey Kilogwe.

Ni vipi check kama unaweza kutupatia link hiyo IT forum ya bongo.
Am chasing for all the information concern IT.

Thanks.

Buswelu
 
Kuhusu Micke Mouse,kama tunavyofahamu hao vijamaa wanaingia kwenye miaka ya 70 tangu waanza huo ukatuni wao,sasa wameingia kweny CGI(computer graphic Interface)format yaani ni 3D kama wenzao Shrek na Toy Story.Kama unakumbuka hawa jamaa walitokea kwenye black and white na sasa wanaingia kwenye 3D kama ni hatua mojawapo ya Firmdevelopment,hii ni biashara,nakumbuka katika kipindi cha marketing Mwalimu wangu aliniambia kitu kimoja In Marketing people Sense and respend while katika sales people make and buy so hapo utaona kuwa hawa Mickey Mouse walisense kuwa sasa watu wanahitaji #D animation ukizingadia hii age ya technology so wakarespond,kaka ndio maana sasa kuna hizi kozi kama Information Management and System ambako huwa wanaandaliwa mamanager katika hii dunia ya IT(Biashara na IT) na hiyo ndio Major Yangu so hayo yote ni mambo ya maendeleo tu,sisjui nimejibu,si unajua binadamu sisi si wakamilifu,haha,tupo kwenye kujenga Mkuu.
Mkubwa Buswelu forum ya IT bongo unaweza kugonga www.eThinkTankTz.org then utafata maelekezo jinsi ya kujiunga.
 
kama unaaccess ya ile IT forum ya Bongo nimegusia mambo ya VPN kule,kuhusu telnet siku hizi watu wanaprefer sana SSH(Secure Shell) kwani katika Telnet password na username zinafari kama Plain text ila kwenye SSH zinakuwa Encrypted so kwa watu wa kati inakuwa ngumu.kwa product za CISCO za sasa zote zina hiyo option so hakuna tena haja ya Kutumia TELNET(hahaha) si unajua mambo ya Technolojia kila cku mpya. By the wayu Ttutaonana kwenye next topic....

Kilongwe kwa lugha yetu ya kibenamanga,japo sikijui chote, maana yake kilicho tangulia.
Kweli wewe ni Kilongwe.
 
Kuhusu Micke Mouse,kama tunavyofahamu hao vijamaa wanaingia kwenye miaka ya 70 tangu waanza huo ukatuni wao,sasa wameingia kweny CGI(computer graphic Interface)format yaani ni 3D kama wenzao Shrek na Toy Story.Kama unakumbuka hawa jamaa walitokea kwenye black and white na sasa wanaingia kwenye 3D kama ni hatua mojawapo ya Firmdevelopment,hii ni biashara,nakumbuka katika kipindi cha marketing Mwalimu wangu aliniambia kitu kimoja In Marketing people Sense and respend while katika sales people make and buy so hapo utaona kuwa hawa Mickey Mouse walisense kuwa sasa watu wanahitaji #D animation ukizingadia hii age ya technology so wakarespond,kaka ndio maana sasa kuna hizi kozi kama Information Management and System ambako huwa wanaandaliwa mamanager katika hii dunia ya IT(Biashara na IT) na hiyo ndio Major Yangu so hayo yote ni mambo ya maendeleo tu,sisjui nimejibu,si unajua binadamu sisi si wakamilifu,haha,tupo kwenye kujenga Mkuu.

Nimekuuliza kuhusu Mickey Mouse kwani ni jina ambalo linatumika kuiita program yoyote ya kutrack hacker au fraudster anapokuwa anajaribu kuingiza string katika web server.

Sasa kwa kawaida mtu unapofanza request lets say katika web server ya Amazon na unahitaji kununua vitabu, ile web server inawasiliana na application inayohusiana na request yako na inaleta form kama ni ya malipo na kadhalika.

Hackers na watukutu wengine wamekuwa wakitunga na kuandika strings mbalimbali kujaribu ku-attack hizo web servers na hasa scripts ambazo programmers wameandika.

Ili kudhibiti hali hiyo makampuni mengi makubwa wameamua kuweka server ingine ya kama chambo kabla ya firewall na kabla ya web server yenyewe iliyo ndani ya firewall, kwa hiyo mtu unaweza kujua kwamba umeingia ndani ya web server ya kampuni lakini wenyewe wamekuwekea Mickey Mouse server ili uchezee huku wakikufuatilia.

Sasa kwa ndani iwe LAN au WAN(kwenye kampuni)kunakuwa na Web server halafu CGI (common Gateway Interface) halafu Firewall na mickey mouse Server kabla ya kwenda katika internet.

computer 1
\
computer 2 (LAN au WAN) <----> Web Server CGI & FIREWALL <--->Server (MM) <----> OUTSIDE (Internet)
/
computer 3

Hivo ndivo jinsi mickey mouse inavotumika katika IT pamoja na neno lingine liitwalo sacrificial lamb kwa hio mickey mouse server.
 
Kwa kuongezea mawezo ya mkuu,
Kuna kitu kidogo ambacho watu wengi wanakioverlook katika ku-trabo shuti network failures(end users - Windows ). kama network yako ilikuwapo naifanya kazi na baadaye unarudi hakuna internet kitu cha kwanza kabisa angalia kama router yako ipo ON na connections (cable) zipo connected.
Kama kila kitu kipo sawa turn off router yako (unplug kutoka kwenye power source) baada ya sekunde kama 20 au zaidi plug hiyo power cable kwenye router ita-reboot na kama kulikuwa na conflicts za IP itarequest ip mpya (ISP wengi wanakupa dynamic IP) ambazo zina expire kila baada ya muda fulani hivyo basi kwa kuanza ni vyema sana ukaanzia ku-reboot router. Na kama una router zaidi ya moja kwa wale wanaotumia VoIP phone kutoka kampuni tofauti na ile iliyokupa internet. zima router zote, baada ya 20 minutes turn on ile main router (ISP Router) ikiisha boot turn on ile ya VoIP halafu reboot your computer. Asilimia kubwa ya matatizo ya kuaccess internet yanatokana vitu vidogo sana ambavyo kila mmoja wetu anaweza kuvitatua.
 
True, hili ni jambo la kwanza kuanza nalo.
Heshima kubwa sana kwenu wakuu
 
Nimekuelewa sana mkuu, lkn nilkua nataka kujua tofaut kati ya internet, Internet na Intranet

Na swala lingne ktk hzo ha2a za kutrouble shoot vp kama tatzo litakua kwny hardware connection? Ntawezaje kujua?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom