How to connect two PC direct?

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Ni mara nyingi watu huitaji kuunganisha computer mbili directly bila ya kutumia kifaa kingine chochote kwa kutumia waya wa kawaida,hii ni useful endapo unataka kuhamisha data kutoka computer moja kwenda nyingine bila ya kutumia kifaa kingine kama USB ,hub,route nk





Tukiingia ndani kidogo tutagundua kuwa nyaya zinazotumika kuunganisha hivi vifaa(kwa mfano Ethernet cable) zina nyaya nane kwa ndani,computer huwa inatumia mbili kutuma na mbili kurudisha,sasa kama hivi vifaa ni vya aina moja eg hapa tunazungumzia PC,ina maanisha vyote vitakuwa vinatuma na kupokea data kupitia nyaya inayofanana.Kuweka mambo kidogo easy kwa mfano kama PC A inatumia waya namba moja na tatu kutuma packets basi PC B nayo itatumia vivo hivyo kutuma na kupokea,hapa inasababisha ajari ajari,kwani kipindi packets zinakuja toka A na nyingine zinakuja toka B,


Crossover Cable





Crossovercable ndio mkombozi wa hiki kit,hi nyaya ni kwa muonekano wa nje ni sawa na nyaya nyingine za zinazotumika kwenye port za ethernet,ila kwa ndani zao zimefanya trick fulani,kinachofanyika kwa ndani ni kuwa kwa mfano wa juu PC A hutumia waya namba 1 and 3 kutuma na 2 and 6 kupokea,sasa kinachotokea hapa ni kuwa inachukua namba 1 na 3 toka PC A na kuingiza kwenye namba 2 and 6 za PC B respectively nyaya nyingine hazibadiliki.Cheki picha hapo chini





How ro make Cross over cable??

Kutengeneza cross over cable ni simple fuatilia maelekzo yafuatayo

Connector 1 Connector 2

Pinout 1 Pinout 2
1 3
2 6
3 1
4 ipo wazi
5 ipo wazi
6 2
7 ipo wazi
8 ipo wazi

So pin 1 -> pin 3, pin 2 -> pin 6, pin 3 -> pin 1, and pin 6 -> pin 2. All of the other pins are left open.

NImesema zipo wazi nikimaanisha kuwa zina matumizi mengine,kwa mfano unapotumia IPTelephone,hizi nyaya zilizowazi hubeba charge(Power over ethernet) ndio maana hizi simu hazihitaji kuweka betri au umeme.
Picha ya chini itakusaidia kukuonesha tofauti kati ya straight through na cross over,






Configuration

Baada ya kuunganisha kitu cha mwisho ni kuzifanya hizo pc zitambuane ie ziongee lugha moja,hapa unatakuwa uzipe anuani(IP Address),unaweza kuzipa anuani yeyote provided ipo kwenye the same subnet,hapa ninamaanisha kuwa hizi address lazima ziwe kwenye range ambayo packet itasafiri bila kuhitaji translater aka routing protocol(inafanana na lugha,kama tunaongea lugha moja hatuhitaji mkarimani,ila kama lugha tofauti mkarimani ni lazima) kwa experience ndogo ni kuwa unashauria utumie private address kama 192.160.1.1 na nyingine 192.160.1.2,hapa utaweza kuzifanya zifanye kazi bila matatizo.

Troubleshoot
Katika swala la technology,huwezi kusema wewe ndio gwij mno na hakuna error inayoweza kutokea,so kuna wakati unatokea umeunganisha hizi PC lakini huwezi kushare data angalia yafuatayo
1.Sharing configuration
2.Firewall au intivirus
3.End points za cross over kwani kuna uwezekano kukatokea Unidirection links ambapo data hazifiki upande wa pili
4.Ip stack yako inawezekana imecorupt,kutest hii jaribu kuping loopback address(NIlishawahi kuelezea hili)

Tuonane wiki ijayo kwenye IP adress na MAC.
Kwa Technology,Knowledge na mengineyo cheki Afroit ICT forum
 

Attachments

  • 5493e509-1ff1-460d-97ff-cde8d0d056a9_3.jpg
    5493e509-1ff1-460d-97ff-cde8d0d056a9_3.jpg
    64.5 KB · Views: 65
  • cables.jpg
    cables.jpg
    52.4 KB · Views: 60
Last edited:
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom