Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Jaribu kucheck na hizi
Shine or go crazy
Jackpot
Hwarang
Rebel
Flower in prison
Moon lovers
Ruler master of mask

King gwanggaetto unaweza kuidownload kupitia drama cool au dramafire

Sent using Jamii Forums mobile app

Hizo nilizozibold nimekwisha kuzitazama, hizo nyingine nitazicheki bila shaka Mkuu.
Asante kwa mapendekezo



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
nahitaji sana series za kikorea hasa za kijijini na ziwe pure yan hazijatafsiriwa na wale jamaa
ombi lako ni gumu kutekelezeka kiupande wa pili wa shilingi, kwa sababu wakorea wana project takribani 100 zenye maudhui ya kihistoria. ingelipendeza zaidi kama ungeliweka list ya drama ulizowahi kuziangalia ndipo na wengineo wakusaidie kukuwekea nyenginezo ambazo hujabahatika kuziangalia.
Category:South Korean historical television series - Wikipedia

utachagua drama utakayokuvutia kwenye tovuti ya wikipedia halafu baadae utazitafuta kwenye tovuti zifuatazo kupitia search engine.
  1. https://kissasian.es/
  2. Watch free Drama Online at Dramanice
 
aminas hivi umeshazitayarisha mbavu zako vizuri kwa ajili ya kushuhudia season 2 ya waikiki drama panapo majaaliwa ya uhai na afya njema?

“Waikiki” Season 2 Confirms Cast: Lee Yi Kyung, Ahn So Hee, Kim Seon Ho, Moon Ga Young, And More
huyu director na crew yake nzima mpaka muda huu wameshindwa kuturudishia chewbacca wetu, nitawezaje kuishi bila ya my beautiful chewbacca, natamani kujinyonga kwa kutumia kamba ya kipolo cha saruji muda huu ila ndio hivyo wajukuu watakuwa na huzuni kwa siku 40.
huyu mwanadamu vituko vyake ni zaidi ya hotuba za rais nicolas maduro, ukichanganya na hotuba za rais wa philipino bila ya kusahau hotuba za rais wa pakistani ya afrika ya mashariki.
 
nimeyapenda maamuzi yako kwa sababu kwa hali inavyokwenda hapa nyumbani kwetu naiogopa siku nitakayotembelea humu nikakutana na taarifa ya kuhuzunisha, ni bora uendelee kuwa mwanaharakati kwa njia ya televisheni drama.


umenipa heshima kubwa sana isiyoendana na uwezo wangu
 
Kwangu Sambog ndiye Waziri mkuu bora wa Joseon master wa Hidden root
 
Nadhani mie peke yangu ndiyo nifika mbali maana hizi historical drama zimejenga kwa kiasi kikubwa uzalendo wangu halafu Miye nimeshajifunza kikorea hivyo nazidi tu kuongeza misamiati
 
jioni ya leo nilibahatika kuiangalia movie inayoitwa masquerade (Gwanghae: The Man Who Became King) ambayo muigizaji mkuu alikuwa ni lee byung hun. Ni movies inayozungumzia stori ya mfalme gwanghae ambaye anaamua kumtafuta mwanadamu anayefanana naye kisura na kumfanya kuwa mfalme kwa lengo la kujiepusha na wapinzani wake ambao walidhamiria kumuondoa madarakani.
kupitia movie hii muigizaji lee byung hun alishiriki nafasi mbili ambazo ni ya mfalme gwanghae na nafasi ya mburudishaji (clown) ambaye alifanana na mfalme gwanghae, inakadiriwa movie hii mnamo mwaka 2012 ilivunja rekodi ya mauzo ya tiketi ambapo takribani watu millioni 12 walinunua tiketi kwa ajili ya kuiangalia movie hii.

baadae ndipo nikaitafuta drama ya The Crowned Clown ambayo ni remake ya movie ya masquerade. Kupitia drama hii episode 2 za mwanzo tayari nimeshajifunza asilimia 80% ya matukio yaliotokezea kwenye movie ya masquerade, nimebaki najiuliza:
je niendelee kuifuatilia hii drama kila wiki wakati najua kitakachotokezea mbeleni?
  • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atajiweka karibu na malikia kama ilivyokuwa kwenye movie
  • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atajulikana na malikia ya kwamba ni fake
  • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atajulikana na wapinzani wake kutoka western faction
  • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atawapigania wananchi wake wasitolewe sadaka kwa ajili ya taifa la ming china na pia ataweka sheria ya matajiri kulipa kodi ya ardhi.
  • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king baadae atakimbilia uhamishoni ili kujiepusha na adhabu ya kifo kutokana na kuigiza nafasi ya mfalme gwanghae.
sijui niifuatilie pengine itaongezeka vionjo kama vya neymar wa barcelona?
hii ndio drama pekee mpya nilioifuatilia mpaka muda huu, nimekusudia mara hii nipunguze ulevi angalau kutoka chupa 50 za mwaka 2018 hadi chupa 25 za mwaka 2019.

nashindwa kuelewa kwa nini drama zote ninazoziangalia zinazowazungumzia mfalme seonjo na mwanawe gwanghae zinawaonyesha wawili hao wakiwa na uhusiano mbaya utafikiri wa Iran na Saudi arabia.
aigoooo kuna watu walifikiri nitaitaja Iran dhidi ya Izrail mataifa ambayo tokea bibi yangu ni kigori wanatambiana ujinga utafikiri ni ngumi za jogooo.
  1. THE KINGS FACE DRAMA: mfalme seonjo alimchukua demu wa mtoto wake.
  2. jingbirok the memoir of imjin war: vita ya urithi wa madaraka
  3. yi sooon shin drama : vita ya urithi wa madaraka
  4. gu am heo jun :mfalme seonjo hakupendelea kumuona mtaalamu wa tiba heo jun akiwa na ukaribu na gwanghae.
dunia na watu wake ni vitu viwili tofauti, kuna watu wanajishangaa kwa kufanikiwa kusoma vitabu 50 kwa mwaka wakati mjinga mimi najishangaa kwa kufanikiwa kuangalia drama 50 kwa mwaka 2018.
 
bado munaendelea kugoma kuifuatilia sky castle drama?
leo inaendelea episode ya 15 na tukumbuke episode ya 14 iliangaliwa na asilimia 16 ya watu wanaoishi korea ya kusini. kutoka 1% hadi 15% ni hatua kubwa sana tumepitia.
JTBC hawajawahi kuonyesha drama iliovuka 13% kwa kuangaliwa nchini korea.
au na nyinyi munadanganya maisha humu ndani?
musigope bwana hakuna asiyedanganya.
 

Attachments

  • 1547233853384.png
    145.6 KB · Views: 34
Kwa sasa naifuatilia Yi san ambayo inamuelezea mfalme Joeng Jo wa Joseon ambaye ni moja katika ya Mfalme bora kabisa wa Joseon dynast huyu aliachiwa Nchi na Babu yake Yoeng Jo ambaye pia alikuwa Genius na alipenda watu sana. Kumbuka King Yoeng Jo of Joseon ni mtoto wa King Sukjong na mama yake ni Constort Suk bin Choe(Dong Yi) Inasemekana alirithi U-Genius na Uzuri wa sura toka kwa mama yake Suk bin choe(Dong Yi)
 

Sasa mimi nimeacha kuangalia Yi San nilishafika episode 5 ndio naangalia Gwanggaeto nipo episode 5! Lol

Ila nashukuru kwa haya maelezo yako maana sikuwa nikijua kama Yi San ni mtoto wa kipenzi changu Dong Yi.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…