MREMBO WA AFRIKA
Member
- Feb 6, 2014
- 65
- 17
Imekua tabia ya wadada weng sasa hv kuishia kulala na wanaume lukuki kwa sababu ya kupenda kuwa tegamezi na kuishia kutoolewa kwa sababu ya katabia hako.ushauri; hakikisha unafanya kila uwezalo kuonyesha kuwa unaweza kufanya mambo yako kivyako bila kuomba-omba (vibomu) unless umekwama kweli kweli yaani malipo yamechelewa au biashara hajaenda vema mwezi huu na mwenye nyumba anatishia kukuweka nje, hakikisha tukio hilo halijirudii mara kwa mara.
Kumbuka kuzungumzia malengo yako ya baadae (sio ndoa) malengo yako kimaisha kwamba ungependa unatafuta kiwanja ili ujenge nyumba hata ya chumba kimoja Mungu akikujaalia, ungependa kununua shamba mahali na kufanya kilimo cha mboga-mboga n.k.
Sahau au usithubutu mambo ya kisistaduu uchwara ya ningependa kufungua duka la kuuza nguo, kufanya pati kubwa ya kuzaliwa kwangu au kununua Prado.....haitosaidia kwani ni kama vile unamwambia akupe mtaji.....zungumzia vitu vikubwa vya kudumu.....atakuona una akili ya kimaendeleo na unafaa kua wa milele Daima.
Sisemi kuwa usipokee zawadi au "mshiko" aki-offer si kajitolea bwana.....hiyo bomba lakini kale ka mchezo ka' kumfanya mpenzi wako kitega uchumi sio njema kwani kila mtu anamajukumu yake ujue! Mwanaume akionakuwa unaweza kujitegemea bila kuwa na kiburi (uswawa kwa sana)anakuwa na uhakika na maisha yenu ya baadae kama familia, na hivyo kusogeza swala la uchumba na ndoa karibu zaidi kuliko alivyopanga kuwa mpaka ajenge nyumba, kumiliki biashara kubwa n.k.
Kwani atajua wazi kuwa mtashirikiana na kufanikisha mambo haraka zaidi ikiwa mko pamoja kama mke na mume......ni kweli ukiwa mwenyewe kufikia malengo inachukua muda mrefu sana (kutokana na uzoefu wangu) lakini mkiwa wawili ktk ndoa malengo yanafikiwa chap-chap....kumbuka usemi usemao umoja ni nguvu na...........!
Hivyo mwanamke usibweteke fanya bidii ktk shughuli zako na onyesha kuwa unaweza kuweka tofauti ktk maisha yenu (ikiwa mtafunga ndoa) hali itakayomvuta mpenzi kutangaza ndoa.[nimecopy mahali koz naona ni msaada kwa single ladies]