Kwa wanaume tu: Ukitoa hakikisha unadai risiti yako

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,185
7,491
mara nyingi wanaume wenzangu wemekua wakileta thread wakilalamika humu mara oooh! napigwa sana mizinga! mara tumejuana jana tu leo anataka nimtumie laki mbili, mara ooh! jana tu nimempa 50, leo tena anataka 100k, mara nimempa 20, anasema hazitoshi nimpe laki mbili na ndio tumejuana leo leo N.k.

Any way mimi sina shida na wapiga mizinga wala watoaji. Ninachowaasa wanaume wanaotoa kwa hiari au kupigwa vizinga ni kwamba waache kulialia bila vielelezo, watakuja gutuka ilishakula kwao! haya!

Ni hivi: "kila ukitoa kiasi chochote cha hela kwa malengo yoyote yale Omba risiti yako! " (na hakikisha risiti yako inaeleza kuwa umetoa kwa ajili ya nini na kiasi gani) hii itakusaidia kwanza kujua kiasi cha hela unachotumia kwenye ishu husika lakini pia kubaki na kumbukumbu kwa ajili ya matumizi mengine na hata mtu akija kulialia humu atakuwa na ushahidi badala ya maneno matupu.Hili pia nadhani litapunguza malalamiko maana ni ajabu kutoa pesa bila kujua hasa unatoa pesa kwa ajili ya nini? halafu baadae unalalamika sijui unalalamika nini!
 
shida watu wanashindwa kuwa wawazi na kunyoosha maelezo mwishowe wanaanza kulaumiana bila sababu.kwa sababu kama mtoaji anatoa zawadi, si kutoa zawadi ni hiari na hutakiwi ulalamike baada ya kutoa au kuiulizia tena zawadi hiyo? na kama si zawadi, kwa nini wahusika wasiwekane sawa kwamba hela ni ya nini, ni kiasi gani n.k ili mtu mtu akilalamika awe na hoja ya msingi?

Mi huwa nasema hapana, sina.

Na kama nikitoa basi natoa kwa hisani halafu naendelea na mengine.
 
Haaaaa lol nae anajibu
"sina baba.... wewe ndio kama baba angu kwa sasa"
hapo utatoa ukijua unatoa kama mzazi, na kwa upande mwingine utatakiwa uchukue na majukumu ya ulezi ukiwa kama mzazi ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu ya muhusika.
 
The first impression utayompa mwanamke ndio itamfanya ajue nini cha kukwambia kila mnapokutana...ukimjia kipredesheee tegemea mizinga sana tu,ukimjia kigentleman nae atajitahidi awe mstaarabu n a lady....so muwe careful na namna mmavyochagua wenza wenu.
 
The first impression utayompa mwanamke ndio itamfanya ajue nini cha kukwambia kila mnapokutana...ukimjia kipredesheee tegemea mizinga sana tu,ukimjia kigentleman nae atajitahidi awe mstaarabu n a lady....so muwe careful na namna mmavyochagua wenza wenu.
Hivi mnaposema mwanaume jentomeni mnakusudia anayechomekea shati au?
 
Back
Top Bottom