Kwa wanaoifahamu kampuni ya'GNLD'

Babu mchumi

Member
Jul 5, 2011
62
11
Habari zenu tha great thinkes!
Naomba wanaifaham vizuri kampuni ya GNLD wanieleweshe kama ni kweli inawasaidia members wake,kwani kwa sasa kumekua na ushawishi mkubwa kwa watu ili wajiunge nayo,ninaomba ni ufafanuzi zaidi kwani hata mimi nimepigiwa simu kushawishiwa kujiunga!
 
Wewe uliwahi kuwa memmber wa DECI?
Hilo ni jina lingine la DECI!

Msitafute utajiri wa rahisi, pesa haitengezwi hivyo kiujanjaujanja tuu!
 
Hiyo GNLD kwa hakika ni pyramid scheme nyingine.

Pia hakuna uhakika wa madawa yao kufanya kazi - bali yana gharama za kuua mtu!
 
GNLD NA forever living products ni kampuni za kimataifa zinazojihusisha ni uuzaji na ununuaji wa madawa katika maradhi na mapungufu mbalimbali .Kiafya products zake zinasifika lakini kibiashara zimekaa kimtindo wa kiunyonyaji kwani zina mfumo wa piramid na kuna ushawishi wa kutengenza pesa kwa haraka lakini wafanikiwao ni wachache.Kifupi ni umachinga fulani hivi wa kumfanyia kazi aliye juu yako. Internationally ,their system of bussiness is quetioned and highly criticised. Kwa maelezo ya kirefu ingia wikipedia utapata maelezo ya kina kabisa. I dont encourage you to have.high expectation whwn joining coz u may fail.
 
tatizo tumekubali uharibifu wa mazingira yanayoweza kutupa vitu asilia, so no way! kwa upande wangu bidhaa zinanisaidia sana na kitambo sasa sijaonana na daktari. mtaponda saaana lakini siku mtakumbuka bidhaa lakini itakua too late kama kilichotokea kwa marehemu bingu wa mutharika rais wa zaman wa malawi... siku ikikupata hiyo kansa utakumbuka tu usemi wako. sasa hivi hata masuala ya mapenzi full migogoro! kisa nini? mnadhani tunapata kila kitu katika chakula?
 
What about 4Life iliyopo Mwenge, Jengo la NAKIETE? Nimeambiwa hawa wana bidhaa bora katika haya makampuni.
 
Habari zenu tha great thinkes!
Naomba wanaifaham vizuri kampuni ya GNLD wanieleweshe kama ni kweli inawasaidia members wake,kwani kwa sasa kumekua na ushawishi mkubwa kwa watu ili wajiunge nayo,ninaomba ni ufafanuzi zaidi kwani hata mimi nimepigiwa simu kushawishiwa kujiunga!

bwana wee product zao za ukweli bwana hilo sio lakubisha mie mtumiaji na nimzikubali sema pesa ndefu...kizuri gharama.

kuhusu kufanikiwa. this is a business like any other businness inabitaji commitment na dedication. sasa tatizo kuvwa ni kwamba watu wana angalia tuu oh nitapata mamilion...forgeting kwamba inahitaji juhudi ya kufa mtu. na ata ukienda kwebye semina zao wanakwambia kabisa kuwa its not easy na muwa its a real business andd success comes after struggle.
 
GNLD NA forever living products ni kampuni za kimataifa zinazojihusisha ni uuzaji na ununuaji wa madawa katika maradhi na mapungufu mbalimbali .Kiafya products zake zinasifika lakini kibiashara zimekaa kimtindo wa kiunyonyaji kwani zina mfumo wa piramid na kuna ushawishi wa kutengenza pesa kwa haraka lakini wafanikiwao ni wachache.Kifupi ni umachinga fulani hivi wa kumfanyia kazi aliye juu yako. Internationally ,their system of bussiness is quetioned and highly criticised. Kwa maelezo ya kirefu ingia wikipedia utapata maelezo ya kina kabisa. I dont encourage you to have.high expectation whwn joining coz u may fail.

They call it "Gamble" take care its more than hazard!!
 
Nashauri msimpotoshe mleta mada, hizo product zina ubora mzuri na kampuni zote tatu GNLD, Forever Living na 4Life wanafanya biashara ya Network Marketing na si Pyramid Scheme.

Tofauti ya MLM (Multi Level Marketing) kulinganisha na Pyramid Scheme ni kuwa ili uweze kufaidika na hayo 'mamilioni' lazima ufanye kazi inayoonekana (kutokana na taratibu za WAZI kampuni ilizojiwekea), faida hiyo ni sehemu tu ya pesa ulizotengeneza katika biashara ya jumla (aidha kwa kuuza bidhaa, kuingiza watu wapya au kutumia binafsi) na inapanda na kushuka kutokana na juhudi yako ya biashara ya kila siku. Katika MLM hakuna kulala nyumbani miezi sita bila kufanya kazi halafu utengeneze pesa, unatengeneza kulingana na kazi uliyofanya. MLM haiangalii nani kaanza mwanzo bali yule anayefanya kazi kwa bidii kuitengenezea kampuni husika biashara.

'Pyramid Scheme' ni tofauti maana inashawishi uingize pesa mwanzo halafu ukachape usingizi ukisubiri pesa, na faida yake inaangalia aliyewahi mwanzo na wengine wote wanaoingia baadaye ni kumtajirisha wa mwanzo au aliye juu.

Nashauri msome zaidi ili kutofautisha hizi biashara mbili.
 
Back
Top Bottom