sitaki kubeza wenye kueneza upendo na kuwalisha kondoo neno la Mungu. tatizo langu katika huu uzi ni mtindo wa LADIES FIRST, NAMBA YA SIMU na kauli fulani ya ubabe kama huhusiki USIKOMENTI. tumeshuhudia katika madhabahu, mikutano ya maombezi watumishi/waombezi wakitoa wito kwa WENYE ndugu, jamaa, marafiki ambao hawakufanikiwa kufika hapo wajitokeze mbele au washike viungo vyenye maradhi kwa niaba ya muombewa. najiuliza huyu anayesisitiza utume namba ya simu, jina na kuchagua muda kama hatakuwa na simu ndio kusema fursa imempita. nawaza kama robert na hayo ndiyo mashaka yangu. mwingine yeyote aweza kutofautiana nami. pia WAOAJI ni sisi, tunaomba mleta uzi aongeze maelezo na SISI waoaji tuombewe labda tu kama JINSIA HAIZINGATIWI katika ndoa ZILIZOLENGWA