Kwa wanandoa wa kesho; vitu vya kubeba kwenye fungate | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanandoa wa kesho; vitu vya kubeba kwenye fungate

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Oct 14, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,233
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  KWANZA NAWATAKIA HARUSI NJEMA INGAWA MMENINYIMA KADI YA HARUSI BASI WATOTO ZENU
  MNAOENDA KUWAZAA WATATUKUMBUKA KWA NEEMA ZA MWENYEZI MUNGU NAWATAKIA MAISHA MEMA NA YENYE FANAKA KILA UKIFIKIRIA KURUSHA NGUMI KWENYE NDOA WEKA WIMBO A NIBEBE NIBEBE NIBEMBELEZE NIBEBEBE WA ROSEMHANDO AMANI HIYOOOO KWA SH 1500
  KWA KANDA MWISHO TUKUMBUSHANE VYA KUBEBA KESHO AIJALISHI UNAENDA MANYANA GUEST HOUSE,,FUNGATE LODGE ,KUTETERE LODGE
  FUNGUA HAAPA LODGE PALE MAPAMBANO HIVI NDIVYO VY A KUBEBA MPWA UKIENDA NA MAMAA FUNGATE

  (Sasa safari imeiva kwenda honeymoon)[​IMG] Vitu Muhimu Kubeba unapoenda Honeymoon:
  Kujua ni vitu gani utavibeba kwenda navyo honeymoon ni hatua muhimu sana na inabidi uwe makini ili ukifika huko usiwe na muda wa kulalamika kwamba, kuna kitu ulipaswa kuwa nacho lakini umekisahau.
  Pia inabidi uwe makini, maana unaweza kubeba vitu ambavyo hata hutavitumia.
  Kitu cha msingi ni kuangalia kwanza yale mambo utaenda kufanya ukiwa huko, aina ya hali ya hewa, je ni sehemu za baridi au sehemu za joto?
  pia muda utakaotumia kukaa huko na huyo mpenzi wako.

  Unaweza pia kufuatilia kuona je sehemu mtakayo tumia (hotel) kwa honeymoon yenu inatoa vitu gani kwenye huduma zao ili msije beba vitu ambavyo nao wanatoa pia.

  Suala la nini kinafaa kuchukua, ni muhimu kujadiliana pamoja na mwenzi wako ili kupunguza vile vitu ambavyo mnaweza kuvibeba wote na kuongeza mzigo wa bure.

  Ifuatayo ni Orodha ya vitu Muhimu Kuvibeba kwa Ajili ya Honeymoon.

  Begi (Luggage)
  Ni vizuri kubeba begi ambalo si kubwa sana hadi linachosha kubeba.
  Usichukue begi kubwa au mizigo mikubwa sana, zingatia kwamba mnaenda kupumzika (relax) baada ya hekaheka nyingi za harusi na pia kuanza maisha mapya na yule anayetimiza ndoto zako hapa duniani.
  Haina umuhimu kubeba nguo zote na kujaza kwenye begi, kitu cha msingi unaweza kubeba zile nguo za kawaida (casual wear) nguo za kuvaa mchana, nguo za kuvaa usiku, nguo za kuvaa chumbani na nguo za ndani (inner wear).

  Nyaraka Muhimu (Documents)
  Vitambulisho, ATM cards (pesa), orodha ya namba za simu muhimu, ticket, passport nk.
  Pia inategemea umesafiri kwenda sehemu gani kwa ajili ya honeymoon, lolote linaweza kutokea, iwe ajali au dharura hivyo unahitaji kuwa na nyaraka muhimu ili kikitokea kitu chochote inakuwa rahisi kupata solution hata kuomba msaaada.

  Nguo
  Mwanaume
  Mwanaume usisahau vitu vifuatavyo, Mkanda (hiari), Mashati, Viatu, Sandals, Kofia (fun), Jacket au koti (kama kuna baridi sana), Tshirts, bukta (shorts), Nguo za ndani za kutosha, socks na nguo za sports na vingine unavyooona wewe vitakufaa

  Mwanamke
  Mwanamke usisahau vitu vifuatavyo Bras, Kofia, Jacket au koti (kama kuna baridi), Vito kama herein nk, Nguo za ndani za kutosha na zenye style tofauti na rangi tofauti, Sandals, Skirts na tops pia nguo zingine ambazo wewe unaona zitakufaa.

  Camera, CD player, Laptop, memory card, Simu (mobile)
  Hakikisha kama umebeba simu unachukua na chaja yake.
  Kupiga picha ni muhimu sana hasa kutokana na wakati muhimu kama huo wa ku-relax na mwenzi wako na kutengeneza kumbukumbu muhimu za maisha mapya na msingi wa maisha pia.
  Pia mnaweza kusikiliza mziki mzuri mnaopenda wakati mnajipumzisha chumbani au wakati wa mambo fulani fulani hapo kitandani.
  Kuna hotel zina wireless connection ya internet hivyo mnaweza kutumia laptop yenu kuweza kujua nini kinaendelea duniani.
  Siyo lazima uwe na vitu vyote nimevitaja hapo juu ni uamuzi na pia kama mnavyo.
  Pia ni muhimu kuwa na simu hasa ikitokea dharura.
  Pia mnaweza kubeba dawa za kutulia maumivu kama kichwa nk, kalamu na karatasi na miwani .

  Afya, usafi na kuoga (Bathroom)
  Mwanaume
  Ni muhimu kubeba vitu vifuatavyo, dawa ya kusukutua (mouthwash), dawa ya meno(toothpaste), mswaki, Shampoo, nyembe za kunyolea (razar) na shaving cream, kitana, Deodorant, na taulo la kuogea pia mints na vitu vingine unavyovifahamu.

  Mwanamke
  Ni muhimu kubeba vitu ambavyo mume wako havitumii kwani wewe na yeye ni kitu kimoja kwa hiyo unahitaji kubeba vitu vile ambavyo ni kwa ajili yako kama vile Pads and tampons, mswaki, tissue, taulo na vipodozi vyote unavyoona vinakufaa.

  Mahaba (Romance)
  Kwa kuwa mnaenda kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza (kama ni mabikira) ni muhimu kujiandaa vizuri na kama ni mara ya kwanza kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa hii ni kudhihirisha kwamba atahitaji lubricants kwa ajili ya kulainisha (njia) ili kupunguza maumivu kwa mara ya kwanza.
  Na kama hamuhitaji kupata mtoto mapema, naamini inabidi mfikirie mtaenda na kifaa gani au njia gani ya birthcontrol (kuzuia mimba) au Njia ya asili (muwe mmepanga tarehe vizuri)
  Pia ni muhimu kuwa na sabuni zinazozuia bacteria na fungus kwani tendo la ndoa kwa mara ya kwanza husababisha maambukizi ya fungus na bacteria kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.
  (Tutaangalia kwa upana zaidi kwenye somo la Lubricants kwa ajili ya mwanamke bikira)

  Tutaendelea na somo.............................................................
   
 2. DULLAH B.

  DULLAH B. JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 674
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Asante!
   
 3. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  thanx.............
   
 4. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Da..,.,kama umenigusa vile pale kulipo..sijui hata umejuaje nilikuwa nahitaji ili somo..
   
 5. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,334
  Likes Received: 2,332
  Trophy Points: 280
  Ubalikiwe kaka
   
 6. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii mada ya muhimu sana na afadhali siku hizi kuna ATMs, M-Pesa nk.
  Wakati niko O level kuna harusi ya jamaa namfahamu ilifanyika pale Tanga, nafikiri labda kwa sababu ya ubusy hakula vizuri jana yake, siku ya arusi yenyewe hizo harusi za kibongo tafrija zinaisha late, basi jamaa wakati wa msosi akagusa tu kama hataki vile. Kufika hoteli wakakuta hakuna mtu aliyekumbuka kuwatangulizia chakula kule! Jamaa anacheki mfukoni hana hata senti halafu njaa kama imetumwa vile! Basi asubuhi best wao anaenda kuwapa hi anakuta jamaa yuko nyang'anyang'a kwa njaa na uchovu, ilibidi msosi utafutwe kwa nguvu zote.
  Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa makini na maandalizi ya kinachofuata immediately after harusi. Vinginevyo panic ya hapo ni balaa.
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  mhhhhhhhhhhhhh! kila jambo lina wenyewe, mweeeeeeee!
   
 8. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2015
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,678
  Trophy Points: 280
  Asante!
   
 9. tang'ana

  tang'ana JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2015
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 6,609
  Likes Received: 4,230
  Trophy Points: 280
  Kondomu haziruhusiwi kubebwa?
   
 10. n

  nasamu100 Senior Member

  #10
  Nov 23, 2015
  Joined: Mar 31, 2015
  Messages: 198
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Somo limeeleweka kwa walioko kwenye maandalizi
   
 11. ISO M.CodD

  ISO M.CodD JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2015
  Joined: Feb 17, 2013
  Messages: 2,657
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Thank you for stating the obvious.
   
 12. espy

  espy JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2015
  Joined: Jul 19, 2013
  Messages: 44,068
  Likes Received: 50,949
  Trophy Points: 280
  Kumbeeeeee!
   
 13. Shonnah

  Shonnah JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2015
  Joined: Dec 3, 2013
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bikira
   
 14. Sojita

  Sojita Member

  #14
  Nov 23, 2015
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 5
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Thaaks
   
 15. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2015
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,630
  Likes Received: 3,014
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu,maana hayo mambo kule Instagram utasikia lipa 1500,isimuliwe
   
 16. M

  Muay Member

  #16
  Nov 23, 2015
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....hilo somo n kwa mabikra tu...ndoa za ckuiz watu washalana saaana na mtoto juu...sasa lubricant za nn hapo
   
 17. Roger Sterling

  Roger Sterling JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2015
  Joined: May 10, 2015
  Messages: 11,105
  Likes Received: 9,585
  Trophy Points: 280
  Smartphone, laptop, external HDD, WiFi router, powerbank. And I'll be fine.
   
 18. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2015
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 21,350
  Likes Received: 13,133
  Trophy Points: 280
  Kumbe fungate ni kitu cha kawaida tu, sijaona kitu ambacho ni exceptional hapo!
  Ila asante mleta uzi.
   
 19. b

  bagain JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2015
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Kwa "ndoa fresh" kama siku si nyingi 2-4 days, vitu kama computer etc wala havitatumika.

  Maana ile tu kuoga, kulala na kukaa mkiwa wawili chumbani itasahaulisha hata kwamba kuna hata kutoka nje ya room.

  Hakuna raha nzuri kama kuoana mkiwa wote bikra. Hata hatua ya kujuana wote mnaanza kujifunza pamoja.

  Unakuta bado kuna hata aibu za kukaa bila nguo au kuoga pamoja. Ikija muda wa tendo takatifu wote hamna uzoefu mnajifunza pamoja.

  Wanaooana wakiwa bikra wote wawili honeymoon huwa na maana sana.

  Huwa nikikaa na mke wangu na kukumbuka honeymoon yetu inatukumbusha kuzidi kuwa waaminifu kwenye ndoa yetu.

  Hakuna raha tamu kama kujifunza pamoja tendo la ndoa mkiwa mme na mke baada ya kufunga ndoa.
   
 20. Little Princess

  Little Princess Member

  #20
  Nov 23, 2015
  Joined: Aug 21, 2015
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha haa duh
   
Loading...