Hii story kuna watu wataichukulia easy tu coz haijawatokea, wadada wa kutusaidia kulea si wote ni wabaya but tunatakiwa kuwa nao makini sana, kujua angalau hata historia yake na mengineyo.
Mimi binafsi iliwahi kunitokea si kwa jinsi hiyo but tulikua tukimwachia dada mtoto chakula anakula yeye mtoto anaambulia mabaki na afya ya mtoto inayumba vibaya sana, wife akiwa na off ya siku mbili tatu mwanetu afya inabadilika, anachangamka tukawa tunajiuliza why?haipiti wiki 2 hatujampeleka mtoto hosp yani ikatuchanganya sana, kufuatilia dr akatwambia mtoto hashibi vyema, wife kaamua kuchukua likizo ya mwezi mzima ili amwangalie mtoto, baada ya muda mtoto afya ikarudi anachangamka, wife akaamua kuchukua maamuzi magumu kwa faida ya mtoto aka resign, tukamrudisha yule msaidizi kwao na mabadiliko yakaonekana, in short jamani kazi ni muhimu but tuwe makini na hawa wadada wa kazi.