Kwa wanachadema tu: Mikakati ya kukuza chama chetu

mwmbeki

Member
Apr 8, 2017
91
124
Ndugu wapendwa wanachadema,nawasalimu katika Bwana,nikiwa kama kada na mkereketwa wa chama hiki,Leo naomba niwadokeze machache ya moyoni mwangu na fikrani mwangu ni namna gani tunaweza kukinyanyua chama.

Ni dhaili na ni ukweli ulio uchi kwamba chama chetu sasa nguvu inapungua kwa kasi sana,kwa hili siwezi kusema ni udhaifu wa viongozi wetu bali ni hila za kiibilisi zinazotumika kuwanyamazisha wasiseme. Naamini hoja tunazo nyingi na ambazo hajipatiwa majawabu, mimi naona tukizingatia haya chama kitasonga mbele.

1: Kujenga hoja imara: Tujenge hoja nzuri na tuje na mbadala wa mawazo ni jinsi gani tunaweza kutatua kero zilizokosa majawabu,na sio kupinga au kukosoa tu bila kuwa mbadala critical thinker watatuona ni wababaishaji,

2: Hoja zenye uhusiano wa moja kwa moja na wananchi mfano elimu.
Elimu
Ikumbukwe kwamba elimu ndo idara pekee iliyopewa dhamana ya kuandaa taifa LA kesho. Kwa wataalam wa elimu tukiitazama elimu iliyopo na inayoendelea tunatamani kulia,ni elimu inayoaandaa taifa la vijana wazururaji na vibaka,elimu ya sasa inachimbia taifa kaburi la hatari

Maisha.
Pia ni ukweli usopingika kuwa sasa maisha yanatoa arufu ka uozo,kila kona ya nchi ni mafuriko ya machozi tutaona hadi chozi LA kipofu hawam hii,staki niseme mengi mtalia.

Ajira
Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila mwananchi anapata elimu na ajira,kwa sasa wasomi wa vyuo vikuu ni kama takataka mtaani, yaani hawana pa kushika eti wajiajili kwanini wao hawakujialili.

Wanajisifia barababara na flyover hayo siyo maendeleo ni vyanzo vya maendeleo.Maendeleo ni ya watu,namna watu wanavyofanya shughuli za kiuchumi.

Usalama wa taifa, ndo hawamo hii watu wanawindana ka wanyama,
Afya.

Bado ni kitendawili maospitalini dawa hakuna n.k

Tuna hoja nyingi lakini nachosisitiza ni kuja na maajabu sio hoja tu.Kwa ufumbuzi wa elimu yaani mfumo upi wa elimu unatakiwa kulingana na maisha ya sasa na yajayo, wanitafute kwa namba 0766789635.Nina hoja nzuri sana juu ya elimu ambazo zinaweza kukipa chama nguvu.

Mwisho kwa Uzi huu: Tusiogope kukosoana,chama si cha mtu,hoja za wanaohama chama tusizipuuze,tuzifanyie kazi.

Nina mengi naomba niishie hapo.

Ni imani yangu nchi itatoka mikononi mwa CCM.

Nawasilisha
 
Unatukana Taifa la wasomi wazururaji wakati mwenyewe hujui kuandika vizuri! Washukuru mods kwa kukurekebishia bandiko lako na kuonekana la kisomi.
 
Mikakati madhubuti.
20180119_101744.png
 
Fukuzeni Lowassa. Na mbadilishe m/kiti Mbowe kashindwa kazi.
 
Back
Top Bottom