Kwa wana ndoa tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wana ndoa tu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Jan 22, 2011.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Je umeshawahi kujiuliza maswali haya? Na uliyapa majibu gani? na uliyafanyia kazi? Nini matokeo yake? Na umepata faida gani?

  1. Ni nini kinachohitajiwa ili kuwa mume mzuri?
  2. Mwanamke anawezaje kufaulu kutimiza jukumu lake akiwa mke?
  3. Ni nini kinachohitajiwa ili kuwa mzazi mzuri?
  4. Watoto wanaweza kufanya nini ili maisha ya familia yawe yenye furaha?

  Karibuni tujadili
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Umetunyanyapaa ambao hatujaolewa ingawa tungeweza kuwa na ushauri hapo.
  Haya ngoja niaccept terms & conditions.
   
 3. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  unaweza kuchangia tu mi nadhani unaweza kutoa mchango mzuri zaidi ya walio kwenye ndoa. So, jimwage mama.
   
 4. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  kumbe hujaolewa...asavali ngoja niku pm tutete!
   
 5. D

  DON G Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  eeeeeeeeeeeee bwana enh mi nadhani mume bora ni yule mwenye kutimiza wajibu woooooooooooooooote anaopaswa kutimimiza jibaba lolote ambalo limevuta mke!!!!! ikiwemo kumjali mke wake, familia yake na dugu na jamaa
   
 6. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Sometimes the poorest man leaves his children the richest inheritance.
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  pm yangu giza nene. Kwanza tunaopm huwa hatusemi semi.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hivi hamna wanandoa humu??Ungeomba ushauri bila masharti..ona sasa wanandoa hawataki kujulikana kwahiyo hawachangii!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Wanandoa mpo wapi mchangie? Au hadi tuwaite kwa majina?
   
 10. M

  Miss Pirate JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kweli hii kwa wanandoa mana nimepata kizungu zungu na hayo maswali.
   
 11. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  maisha hayana general formula inayo apply kwa kila mtu.
   
 12. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  sasa hayo maswali yanabidi watu wajiulize
  kabla hawajaingia mkenge wa ndoa ili waweze
  kufanya uchaguzi/uamuzi mwema.

  na hilo sharti la kusema "kwa wana ndoa tu" limewafanya
  watu wauchune. panua uwingo mazee
   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Napita tu, siruhusiwi kusema hapa:car::car:
   
 14. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  siafiki mama...hebu vaa miwani usome tena!!
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  huafiki nini wakati heading ishajielezea.
  Haya nipe hiyo miwani ya mbao.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  2naotaraj kuja kua wanandoa 2bak az viewerz
  WAKUBWA NDO WANAOFAID
   
 17. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umeuliza maswali ambayo ni ya msingi na yanastahili kutendewa haki kwa kujibiwa kwa uzoefu wa wanandoa. Ni kweli kanuni moja haiwezi kufanya kazi kwa mwingine ila kanuni ni kanuni na inapotumika huweza kuleta manufaa.

  Mwanzoni mwa ndoa yangu (sasa ni kama miaka mi-4 tu na nusu hivi) tulikubalana na mwenza wangu juu ya kanuni za msingi za kuendesha ndoa yetu kwa mfanikio. Ndoa isiyo kuwa na kanuni haiwezi kuzaa baba bora, mama bora wala watoto waliofundwa na kulelewa vema. Kanuni lazima ziwe za ndoa na wala sio za mume au mke peke yake. Ni za kukubaliana pamoja. Tulipokubaliana tumeziweka "ikulu" kwetu na kila mara tuwapo ndani tunaziona na kukumbushana  Kwa upande wangu, kanuni zetu za msingi ni hzi na unaweza kuzitumia ukaanza kuona matunda yake  (i) Companionship ----hii inatilia umaanani namna unavyomchukulia mwenza wako kwenye mahusiano. Je unamchukulia kama sehemu yako ya muhimu ya maisha ambae bila yeye kuna kitu hakitakuwa sawa. Hii inatilia umaanani zaidi ile hali ya kama mwanaume au mwanamke kujiona kuwa ni mpungufu mahali Fulani kama mwenza wake hatakuwa sehemu ya maisha. Pale utakapokoma kumuona mwenzako kama sehemu ya muhimu sana ya maisha yako hapo ndipo utaanza kuona ladha ya ndoa yako inapungua.


  Kwenye companionship utakutana na kitu kinachoitwa gratitude. Hii ni ile hali ya kumkubali mwenza wako. Mpaka kufikia hatua ya kufunga nae ndoa lazima kuna vitu ulimkubali ndio maana ukakubali kufunga nae ndoa. Focus kwenye hivi vitu vilivyokupa kumkubali na kuamua kufunga ndoa kwa ahadi ya kuishi nae daima hadi kifo kiwatenganishe. Nikiweka msisitizo wa kiingereza naweza kusema Gratitude is the awareness of all the kindness your spouse does for you, of which you must recognize i.e appreciating your spouse's virtues, positive attributes and character traits. Unaweza ukajijengea kwa week kuweka kumbukumbu yam mambo matano tofauti nay a pekee ambayo mwenzako amefanya na yamefanya tofauti kwenye mahusiano yenu. Note and communiocate them.

  (ii) Completeness through understanding and forgiving; Kila mtu anaelewa ya kuwa hakuna mtu aliekamilika duniani. Wazungu wanasema “To err is human, to forgive is divine . Hakuna kitu cha muhimu kwenye mahusiano kama kutafuta kumsaidia mwenza wako kuwa mkamilifu kuliko kupambana nae. Kama utafanikiwa kwenye hilo la kwanza hapo juu utagundua pia unajukumu la kumsaidia mwenza wako kufikia ule ukamilifu unaoutaka huku ukijua ya kuwa sio malaika na wakati wowote anaweza kukosea jambo na hivyo utarudi tena na jukumu la kumrekebisha.

  Help your spouse towards seeking that wholeness you want to see in him/her. Usisahau ya kuwa na wewe mwenyewe unayo mapungufu ambayo yatahitaji yeye akuelewe na kukusamehe. All in all kanuni ya msingi ya mahusiano ya Bwana Yesu (kwa wale walio wa Kristo) “mtendee mwingine kile unachotaka wewe kutendewa”. Kama unapenda mwenza wako akuelewe basi jitahidi nawe umuelewe kwa karibu zaidi

  (ii) Communication.
  Hii ndiyo ya msingi ambayo inabeba hizo zilizotangulia hapo juu. Kama hakuna mawasiliano hapo ujue uko hatarini. Ndani ya nyumba yangu huwa kila mara lazima tukumbushane kwa utani mdogo. Huwa namuuliza mwenzangu, hivi kama nataka kuachana na wewe leo nifanyaje…huwa ananijibu “Ninyime nafasi ya kunisikiliza”…Yes indeed, a marriage without communication cannot survive. Mawasiliano ndiyo yanayotoa muongozo na muelekeo. Ndiyo chakula cha ndoa. Kila mgongano unaotokea mara nyingi athari zake unapokuja kuzitathmini utagundua ni kwa sababu mmoja ameshindwa kutoa nafasi ya kumsikiliza mwingine. Ukisikiliza hakuna litakaloharibika. Fanya assessment ya mahusiano yaliyo tata utagundua kusikilizana kumekwisha na sio kama ilivyokuwa hapo awali.


  Ni muhimu ujihakikishe katika haya

  • Je nimeacha kumsikiliza na KUMUELEWA mwenza wangu?

  • Am i a compulsive talker? Usipitilize kiasi ukawa wewe tu ndio unataka kusikilizwa.
  • Do you listen without presuming or judging? Je natafuta suluhu au natafuta nani mwenye kosa? Katika mawasiliano yenu central focus iwe ni katika kujenga uhusiano zaidi na sio kumtafuta aliekosea ili umpe adhabu…tafuta suluhu yenye kuhuisha uhusiano wenu

  • Je unasikiliza kwa kugusa au kwa kusikiliza? Mara nyingi nimejigundua kuna maelezo mengine siwezi kumuelewa mke wangu kwa masikio. Nahitaji mikono yangu iwepo kazini ndipo nitamuelewa. Sihitaji kuzungumza jambo akiwa mbali au kutafuta maelezo akiwa kakaa kochi jingine na mimi niko mbali..wakati mwingine nataka anieleze jambo ambalo linaleta utata nikiwa nimemshika na kumkumbatia au yu karibu zaidi na mimi. Kama naona hali hairuhusu labda ni jambo lenye kukera huwa naondoka kwa muda mpaka nitulie kisha narudi kuzungumza nae nikiwa karibu nae kama hakuna kitu kilichotokea, maadamu tu kutafuta suluhu…Yes, listening is not always done by the ears; sometimes it invloves holding or touching hasa kwa yale matata zaidi.

  • Je unawasiliana kwa uwazi na hu-take advantage ya kusikilizwa? Be a man/woman of honesty and integrity. Usitumie vibaya kusikilizwa na kuheshimiwa na menzako maana kunaweza kumuondolea kukuamini na ikawa mwisho wa kila kitu
  ZAIDI YA YOTE MSIACHE KUOMBA PAMOJA
   
Loading...