Wanajamvi mpooooo!?
Salaam,natumaini jumapili ni njema kwa kila mmoja.Kwanza natanguliza ka stori haka;
Kulikuwa na vipepeo wawili waliokuwa wanapendana sana,siku 1 waliamua kucheza mchezo wa mahaba.Walichagua UA na walipanga kesho ambaye atakuja mapema na kukaa juu ya UA atakuwa anampenda mwenzake zaidi.Asubuhi kipepeo dume alienda mapema sana na kukaa juu ya UA.Maskini alichokikuta...!!
Ua lilipofunguka alishtuka kuona kwamba kipepeo jike amekufa ndani ya UA.Kumbe yeye kaingia tangu jana jioni,alikuwa anasubir kumwonesha mpenzi wake ni jinsi gani anavyompenda..!! Jee !! wewe,utamuonesha nini umpendae ili aone ni kiasi gani unampenda??
hebu tupia,ili tupate ujuzi zaidi ktk kuwa show love wenzi wetu,hasa jp kama ya leo.