Kwa waliosoma shule za msingi Iringa mjini miaka 90 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa waliosoma shule za msingi Iringa mjini miaka 90

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by namanyele, Oct 29, 2012.

 1. namanyele

  namanyele JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,795
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Wana jf hebu tujikumbushe kidogo wale tuliopitia shule za msingi iringa mjini,binafsi nimesoma sabasaba primary sc nilianza mwaka 1991 namkumbuka sana mwl Danga alinifundisha kusoma na kuandika darasa la kwanza,wengine walimu kama solomon na mwl admin duu! usipime walikuwa wanagonga stiki balaa,pia mwl komba wa wilolesi alikuwa mlemavu mwanamichezo,mwl ndeme wa kilimani huyu hata uvae mikombozi lakini stiki zake maumivu the same,mwl.Ibobo,vp wengine mnakumbuka nini enzi hizo? PASUKENI WANA JF!!! mlandege,
   
 2. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nilisoma shule ya Misingi wilolesi, namkumbuka Mwalimu Kajiba alikuwa mwalimu mkuu ingawa baadae alihamishwa, shule yetu ilikuwa inasifika kwa kuponda kokoto, kucheza gwaride safi kila alhamisi, pia mwalimu wangu wa darasa alikuwa mwalimu Matola alitufundisha sayansi na hisabati, alikuwa mchapakazi, hodari asiyependa mchezo katika masomo alikuwa anasifika kwa viboko na kutupigisha magoti kwenye kokoto tulizoponda wenyewe kama adhabu pale tunapokosa.

  Ila kiukweli alikuwa mwalimu mzuri na hodari katika kufundisha alipanda cheo na kuwa mwalimu mkuu kwenye shule nyingine ila baada ya mimi kumaliza darasa la saba.

  Shule yetu pia ilikuwa na sifa ya uoga wa kimazingara yaani kuwa kuna majini katika ile shule. kuna vyoo ambavyo inasemakana vilifungwa visitumiwe tena kwa ajili ya majini, kuna miti miwili ya mitoo ilikuwa inazaa mitoo lakini twaogopa kula matunda yake kwa kuogopa majini, na pia ilikuwa kuwa eti kila mwaka lazima mwanafunzi afe kwa sababu ya makosa waliyoyakosea majini. Kha. Mungu atunusuru na awanusuru waliobaki na wanaondelea kubaki.

  Mbali na hayo ilikuwa shule nzuri sana niliyoipenda.
   
 3. namanyele

  namanyele JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,795
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  mkuu Rubi hapo juu umenikumbusha kweli kabisa wilolesi ili inasifika kwa majini eti vyooni kuna kipindi wanafunzi wanaskia harufu ya pilau inawavutia wanafunz kuifuata na mmoja lazima afe,pia kimazingira ilikuwa kama jangwa fulani,nimesalia sana sunday school moravian kwenye madarasa yao wakati kanisa kubwa lilikuwa la mbao kando ya shule kabla ya kujenga kule kihesa,ni mda mrefu sana
   
 4. m

  msagalam Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya hapa mimi wa Mlandege nimesoma kuanzia 1991 pale tulikuwa na mwalimu mkuu Mfikwa mwanzoni baadaye kama darasa la tano hivi akaja Mwalimu Lumbila da alikuwa balaa anachapa fimbo yani akikukuta na kosa fimbo si chini ya tano na kuendelea hadi 30 na akimaliza anasema useme asante, usiposema zinaendelea,Tulikuwa na mwalimu taremwa, Simbili-la kwanza lazima akufundishe huyu, Mwano, Muhinda(hisabati) na Chazua(english),Ki ukweli shule ilikuwa bomba sana kipindi hicho kwa iringa kufaulu ni lugalo tu ndio unaonekana una akili hakuna cha highland,mwembetogwa wala ruaha yani ukisoma huko ah alifeli yule
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mi nilisoma shule ya msingi Ilala pale nyuma ya Mkwawa University bahati mbaya simkumbuki mwalimu hata mmoja
   
 6. namanyele

  namanyele JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,795
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  we ndo kilaza kweli,inaonekana ulikua mtoro sana,mwaka 1997 nakumbuka tulifanya joint exam sabasaba na ilala,mwalim mkuu ilala alikuwa wa kike aliamishwa toka sabasaba,alikuwa white fulani hivi ila jina limenitoka
   
 7. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hapana mimi sikua mtoro wala nini, nilikuwa mtu wa matwishen ndo maana hata walimu nilikuwa siwafahamu.Ulizia shule ya msingi Nyumbatatu pale nyuma ya Denish mission wananijua sana vitu vyangu maana ndo tuliokuwa tunafanya nao mitihani ya ujirani mwema
   
 8. C

  CAY JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii ni ajabu kidogo!
   
 9. namanyele

  namanyele JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,795
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  jamaa amesoma darasa la kwanza mpaka la saba hamkumbuki mwalimu hata mmoja,eti matwisheni sana wakati kipindi kile twisheni tulikuwa unasoma hapohapo shuleni kwako na waalimu wa hapohapo,hata Mlingi Ibobo,Manase Mlonganile,khalid Idd,Hamza kioko,Godfrey Malinga,Jacob Rueben,Sikutegemea Damian,Aloyce Nelson,Nancy Limo,Getruda Vitusi,Leornad John,Humphrey Amani,Chesko Pera,Bosco Nukosi,john mathias,dogo kiroboto,wanafahamu sana enzi hizo
   
 10. K

  Karim Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Salaam's Mimi nimesoma Sabasaba ,Nimemaliza mwaka 1986 ,Nakumbuka Mwalimu Mkuu alikuwa Mama Staki ,Mwalimu wangu wa Darasa la Kwanza alikuwa Mwalimu Seme ,pia naakumbuka Baadhi ya walimu kama Mwalimu Saidi ,Mwaitebele ,Phidelis ,Mwalimu lupola, mwalimu Mohamed kamanda wa Chipukizi ,Mama Komba ,Mwalimu Edmin ,Mama Msafiri na wengine nimewasahau ,lakini hii thread Imenikumbusha mbali sana !!
   
 11. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimemaliza mwaka 1997 Ilala nilihamia kuanzia darasa la sita, nawakumbuka mwalimu Mwang'onda, Bernard, mwalimu Mkuu Kyembela alikuwa na mwanae tulisoma naye aliitwa Emmy sasa yupo Mbeya, mwl Mgohamwende s/kimu, tuition kwa mwakeja, mwl wa sayansi Kweka huyu jamaa alikuwa noma ukichelewa ukiwa zamu au hujafanya zoezi anapiga viboko vya kuinama unashika vidole, hata upige dabali lazima usikilizie utamu kudadeki
   
 12. namanyele

  namanyele JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,795
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  du! noma kuna kitu nimekumbuka huwa sisahau ktk maisha yangu,darasa la pili pale sabasaba kuna jamaa tulikuwa tunasoma naye alikuwa kila siku ya Mungu tukiwa darasa ishara ya kutambua kwamba yupo darasani ni lazima ajambe bila sauti,alikuwa anaitwa Msafiri Kikoti alikuwa anatokea kihesa,akiachia kitu darasa zima lazima mtoke nje hata Raymond Mihayo,christina pera,Moses Sanga,marehem dogo chande,jerry,John Francis watakumbuka mbali sana kwa hilo
   
 13. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  mie nilisoma KIHESA PS ila sitaki kukumbuka background yangu aisee........ IT IS TERRIBLE.......
   
 14. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ulikuwa mwizi wa mapera na mikusu nini asigwa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  haha ha mkuu umegusa kwenyewe aiseee ...you are genious aisee.... enzi hizo naatokea gangilonga ni mwendo wa kujificha kwenye vitindi tuu
   
 16. namanyele

  namanyele JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 1,795
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  kati ya shule za msingi zilizokuwa zinaongoza kwa ubaya wa matokeo,majengo mabovu na mazingira machafu ni KIHESA PR,sasa mkuu assigwa anashndwa kuwa muwazi na utoro wake pia uwizi wa mapera,mitoo,misasati,mifudu na maembe machanga
   
 17. t

  testa JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2013
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimesoma sabasaba namkumbuka mwalimu Kisunda,Adimini,Myonga,Nyakunga walikuwa walimu wangu Kihesa kulikuwa na mwanafunzi anaitwa Juma Mpwisu alikuwa mkorofi sana
   
 18. faby

  faby JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2013
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 2,231
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mimi nilisoma mapinduzi kwanzia mwaka 1988
   
 19. s

  serggally Member

  #19
  Oct 30, 2013
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Mimi nilisoma kichangani enzi za mwlm mlelwa, sister vero, mwlm kassim, mama komba,mwlm mpako


  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 20. t

  testa JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2013
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ilikuwa njia yangu ya kwenda home nikitoka shule,wewe utakuwa umesoma kipindi cha kina Samwel Kisigo au marehemu Muna Lipangile
   
Loading...