Kwa waliosoma shule za msingi Iringa mjini miaka 90

mkuu Rubi hapo juu umenikumbusha kweli kabisa wilolesi ili inasifika kwa majini eti vyooni kuna kipindi wanafunzi wanaskia harufu ya pilau inawavutia wanafunz kuifuata na mmoja lazima afe,pia kimazingira ilikuwa kama jangwa fulani,nimesalia sana sunday school moravian kwenye madarasa yao wakati kanisa kubwa lilikuwa la mbao kando ya shule kabla ya kujenga kule kihesa,ni mda mrefu sana
kweli ya kale ni dhahabu natamani kweli enzi ingekuwa inarudi. nakumbuka nilivyokuwa napenda mikusu, misaula, maembe mabichi ya chunvi, kabla ya kuhamia wilolesi nilikuwa Njombe katika shule ya Mpechi primary school, nilikuwa na marafiki zangu , vinga, Roida,sevanu, nawakumbuka sana tangu tumeachana sijawahi kusikia habari zao wala kukutana nao.
 
kweli ya kale ni dhahabu natamani kweli enzi ingekuwa inarudi. nakumbuka nilivyokuwa napenda mikusu, misaula, maembe mabichi ya chunvi, kabla ya kuhamia wilolesi nilikuwa Njombe katika shule ya Mpechi primary school, nilikuwa na marafiki zangu , vinga, Roida,sevanu, nawakumbuka sana tangu tumeachana sijawahi kusikia habari zao wala kukutana nao.

imenikumbusha shule ya msingi wilolesi tulikuwa tunakula sana mifudu pale shuleni.
 
nimesoma ubungo N.H..nilimaliza mwaka wa 1999..shule yetu ilikuwa vizuri kwa mchakamcha, fujo pia tulikuwa tunaziweza tambaza,makurumra mugabe walituogopa..nakumbuka wamasai walikuwa wanakamata sana wanafunzi watolo na wavuta bangi..wengi tulikuwa vijobu(wategeaji kuingia darasani) sana enzi hizo tunaacha masomo tunaenda mugabe au mlimani chuo kikuu au nyuma ya bonde la perfect vision high school kupoteza mda..tulikuwa wazuri kielimu na kimichezo asa umitashumta na sanaa pale mlimani enzi hizo kulikuwa na matamasha ya mashule kimashindano yalikuwa yanafanyika chuo kikuu cha mlimani tulikuwa tunawakilisha vizuri sana (nakumbuka ule wimbo wa tamasha tamasha 98 tamasha tunaimba imba tamasha tunacheza cheza tamasha kalibuni nyote" nawakumbuka wakina shira..saidi..mwalabu jimmy..na mwalimu mmoja wa kiume wa somo la kiingeleza hivi alikuwa anapiga bakora hatari..mie nilikuwa naudhuria kipindi cha dini tu sababu kulikuwa kuna mwalimu wa hadithi alikuwa anatuadithia hadithi nzuri na mawaidha nilikuwa nampenda ila jina nimelitoka..kifupi nilisota sana shule ya msingi ila kwa sasa nipo vizuri na chuo ninemaliza...nikikumbukaga mambo ya shule ya msingi machozi yananitoka..walio maliza UBUNGO N.H MWAKA WA 1999..TUKUMBUKANE
FADHIL..
 
jamaa amesoma darasa la kwanza mpaka la saba hamkumbuki mwalimu hata mmoja,eti matwisheni sana wakati kipindi kile twisheni tulikuwa unasoma hapohapo shuleni kwako na waalimu wa hapohapo,hata Mlingi Ibobo,Manase Mlonganile,khalid Idd,Hamza kioko,Godfrey Malinga,Jacob Rueben,Sikutegemea Damian,Aloyce Nelson,Nancy Limo,Getruda Vitusi,Leornad John,Humphrey Amani,Chesko Pera,Bosco Nukosi,john mathias,dogo kiroboto,wanafahamu sana enzi hizo
Hivi zamani kulikuwa kuna umuhimu wa tuisheni kweli?
 
Raha ya Gangilonga ilikuwa ni kuchuma mavunja genge na upupu ule wa Maharage.
Halafu jioni mnapita ile njia ya Mahakama mpya au Garden ya zamani mnaenda kula mazambarau na kuogelea Ruaha........

Nakumbuka miaka hiyo Iringa hata magari shidaaaa wenye Magari walikuwa ni wakina Mwakatundu, Mzee Mwakingwe, Mzee Malipula, Mzee Abri, Mzee Luvinga, Mzee Siyovelwa, Mzee Mlawa, yaaani daah....

Good old days.....
Luvinga aliyekuwa mkufunzi Wa kleruu college
 
Nilianzia shule pale Makanyagio, nikahia nyumbatatu, then sabasaba tangu la pili mpaka namaliza. Wale waliomaliza 1995 sabasaba tutakuwa tunafahamiana vizuri tu.
 
Back
Top Bottom