Pamoja na kwamba wengi mnaiponda hii shule, lakini ukweli unabaki kwamba ubora wa shule ni kichwa chako!! Sisi tumesoma pale miaka hiyo ya 2000 na tukanyoosha vizuri tuu.. Uzuri ni kwamba shule hii ukiamua kuwa serious, materials + walimu wazuri wapo, ila ukiamua kuwa muuza sura ndio hivyo tena!
Nimewakumbuka sana walimu wa enzi hizo sijui kama bado wapo kina Mr. Lyatuu, Mr. Mlay, Mr. Sendoro (RIP), Mr. James, "Prof" Makundi, Miss Mkonyi, Mama Minja, Mushi B, Pedejee Kichawele.. na kuna yule mzee mpishi Mr. James.. mlinzi Mzee Ali tulikua tunamtoa shing 100 anatuacha tunaenda kula Fast Fry.. dah..
Halafu kuna wanafunzi walikuwa maarufu sana miaka ya 98 - kina Edgar Kisakisa, Ombeni, Mawenya.., sijui wako wapi ssa ivi? Na kile kiduka pale ndani cha matozi waliokuwa wanashindia "matofali" na coca mwaka mzima sijui kipo? dah..