Kwa waliopo kwenye mahusiano...

Kwa waliopo kwenye mahusiano...

selina mrembo

Member
Joined
May 18, 2020
Posts
54
Reaction score
68
Jamani machungu yangu hayaelezeki, hii naomba mjifunze hata nyie mlioko kwenye mahusiano. Usizae kama hujafunga ndoa yamenikuta naitwa single mother sasa hivi bila kupenda mwanaume alinionesha kunipenda na kunipa moyo ipo siku anaweza ishi na mimi lakini mambo yamekuwa tofauti kabisa na nilivyotegemea.

Niliacha kazi yangu iliyonipa kipato japo kilikuwa kidogo kilitosha nikaacha kazi yangu kwenda shule kuongeza elimu mana niliona kwa level yake ilibidi na mimi nijiongeze kidogo!

Ndugu yangu mwanaume sio ndugu yako sasa hivi kaniambia nisimtafute ana mahusiano yake, naumia nimeishiwa nguvu kabisa hata za kwenda shule tena.
 
Back
Top Bottom