Kwa waliokuwa wanakula Pizza Mgahawa wa Uchumi Supermarket

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Walikuwa na Pizza tamu sana tena kwa bei nzuri tu ambayo ilitufanya sisi wapenzi wa pizza tule pizza kila mara. sasa baada ya uchumi kuondolewa nimekuwa nikihangaika kwa mimi nliye mjini ntapata wapi pizza kama zile za bei rahisi na zenye ubora pia?

Maana town ukigusa pizza tsh 12,000 + kiukweli hapo hatuwez kula kila siku sisi wenye kipato kidogo.

Tufahamishane wadau kijiwe kingine cha kula pizza kwa bei nzurikama ya uchumi ni wapi?

WAKATI WENGINE WANAKULA ILI WASIFE, WANAKULA KUJAZA MATUMBO. SISI KWETU KULA NI SEHEMU YA STAREHE.
 
nielekeze vizuri ndugu yangu hiyo njia si mtumiaji sana .halaf kwa sisi tunaofanya kazi posta sehemu gan itakuwa rahisi sana na bei reasonable. hapo kamata panaitwaje huo mgahawa wenyewe?wanaweza kudeliver nilipo?

Jaribu "Pizza Hut" pale Kamata,jengo jipya la Halmashauri ya Ilala.
Unapata Margareta nzuri tu kama ya upo kwenye viunga vya Napoli na Sicilia.
 
nielekeze vizuri ndugu yangu hiyo njia si mtumiaji sana .halaf kwa sisi tunaofanya kazi posta sehemu gan itakuwa rahisi sana na bei reasonable. hapo kamata panaitwaje huo mgahawa wenyewe?wanaweza kudeliver nilipo?
Opposite na bandari ya nchi kavu ya TALL,Nyerere Road ukivuka mataa ya Chang'ombe,unavuka daraja,mbele upande wa kulia utaona jengo kubwa na Mkuki House...Hapo hapo utapata
 
Daaaaaaaaaaahhh yani mimi ujue nakaa hapa Makumbusho. Sasa nilikuwa naenda hapa uchumi supermaket hata mara nne kwa siku.
Sasa hivi naenda piza hati ila nako mbali sana daah... Yani umenikumbusha mbali sana
Muongo kweli wewe Kama ulikuwa unaenda Mara 4 kwa siku 3000*4= 12000
Kwanini usiende pale millennium tower jirani na hapo makumbusho ah 9000/= ..??
 
nyie wanawake wa mikoani mmezoea kula ugali na mlenda/maharge mnadhan ndo maisha. unajua pizza inatengenezwa na aina gani ya vyakula? ushamba mzigo sana unadhani vyakula vigumu ndo nguvu? basi dawa za kuongeza nguvu zingekuwa ni kama mawe. ungejua dawa za kuongeza nguvu kuna za unga na za maji basi ungejua kuwa kuwa na nguvu hakutokani na kula ugali maharage kila siku. ficha ujinga wako dada.

maisha ni pamoja na kula vitu vizuri .kama unataka kupimana ubavu na mimi nakukaribisha uone kama unaweza. nakula roho inachopenda na si ushamba wa wanawake wa huko mikoani wanashindwa kula chakula kizuri wanashindia mavyakula magumu tu wakidhani ndo nguvu.

Wanaume wa dar mnashida sana aisee ndio maana kina scorpion wanawaonea sana
 
nyie wanawake wa mikoani mmezoea kula ugali na mlenda/maharge mnadhan ndo maisha. unajua pizza inatengenezwa na aina gani ya vyakula? ushamba mzigo sana unadhani vyakula vigumu ndo nguvu? basi dawa za kuongeza nguvu zingekuwa ni kama mawe. ungejua dawa za kuongeza nguvu kuna za unga na za maji basi ungejua kuwa kuwa na nguvu hakutokani na kula ugali maharage kila siku. ficha ujinga wako dada.

maisha ni pamoja na kula vitu vizuri .kama unataka kupimana ubavu na mimi nakukaribisha uone kama unaweza. nakula roho inachopenda na si ushamba wa wanawake wa huko mikoani wanashindwa kula chakula kizuri wanashindia mavyakula magumu tu wakidhani ndo nguvu.
Wasamehe mkuu ni mawazo mgando, hivi unahabari tanzania hii hii bado watu wanaamini kuna wanyonya damu, na kwa tahadhari kuna baadhi ya maeneo huko mikoani, usivae vizuri ukatembea vizuri vijijini, watakuona wewe mnyonya damu.
 
Back
Top Bottom