Kuna babaangu mdogo alipewa amri na babu ya kunitandika kila asubuhi iwapo nitakuwa nimekojoa, bahati mbaya kwangu jamaa alikuwa ananichukia mbaya kwakuwa nilikuwa napendwa sana na babu, basi akachukua nafasi hiyo kuniadhibu kila siku, nikojoe, nisikojoe lazima nichezee stick za kutosha...Kama unakumbuka kukojoa kitandani ni kashikashi zipi ulipata by that time..mimi nakumbuka nilikuwa napigwa na kuambiwa nitoe matandiko huko nikila fimbo!
Raha niliyokuwa naipata nipale niliota nipo upenuni nakujoa huku washikaaji wananisibiria nusu dakika najiluta nipo kwenye dimbwi!!![]()
