Kwa walioko kwenye ndoa, mawazo yenu please

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,383
1,354
Jamani mimi ni kijana wa kiume nimeoa miezi mitatu iliyopita, naomben wadau mnisaidie kina jambo linanitatiza. Mimi kwetu ni Dar es Salaam na wazazi wangu wanakaa Dar es Salaam. Lakini mke wangu yeye kwao ni mkoani na wazazi wake wanaishi huko mkoani. Swali langu ni hili, hivi naweza kwenda nyumbani kuwasalimia wazazi wangu bila kuwa na mke wangu mfano nimetoka kazini halafu nikapitia nyumbani then nikamwambia mke wangu kuwa nimepitia kwetu, hiyo itakua mbaya au inatakiwa kila nikienda nyumbani niwe na mke wangu au nimfahamishe mapema kabla ya safari? Naombeni ushauri wenu na namna ya kuhandle hili suala maana mimi bado mchanga kwenye ndoa.
 
duuu, hapa sina la kuongea kwani sijaoa, lakini kwa mtazamo wangu haina shida unaweza kupitia ukamwambia mkeo kuwa umepita nyumbani, ila angalizo safari za nyumbani kwenu zipungue sasa, unaenda kwenu kufanya nini tena, kusalimu?? tumia simu bana, usimtenge mkeo, kwenda nae ndio vizuri zaidi na atajisikia furaha na amani, kuliko kwenda alone
 
duuu, hapa sina la kuongea kwani sijaoa, lakini kwa mtazamo wangu haina shida unaweza kupitia ukamwambia mkeo kuwa umepita nyumbani, ila angalizo safari za nyumbani kwenu zipungue sasa, unaenda kwenu kufanya nini tena, kusalimu?? tumia simu bana, usimtenge mkeo, kwenda nae ndio vizuri zaidi na atajisikia furaha na amani, kuliko kwenda alone

Kwani anavyokwenda si halali kama ni kupita tu mimi sioni kama kuna ubaya
 
Me cjaolewa ila kwa upeo wng mdogo naona:Cku moja moja c mbaya ila ucjenge mazoea sasa...but wekeends ni vizur zaid ukaenda na mkeo,mnawapelekea chochote kitu n mkipata nafac pia mnapanga mnaenda mkoan kwa wazaz wa mkeo ili kuonesha pande zote mbili ni muhimu kwako n unazijali...
 
Kwa upande wangu hata mwanamke nae anaweza kujipitia nae anapojisikia na ni vyema mnapokuwa na muda mkaenda kwa pamoja na mkawasabahi!
 
punguza safari za kwenda kwa wazazi na utenge muda zaidi kwa mkeo... mwisho utaanza kulinganisha msosi anaopika mama na mkeo sasa
 
Me cjaolewa ila kwa upeo wng mdogo naona:Cku moja moja c mbaya ila ucjenge mazoea sasa...but wekeends ni vizur zaid ukaenda na mkeo,mnawapelekea chochote kitu n mkipata nafac pia mnapanga mnaenda mkoan kwa wazaz wa mkeo ili kuonesha pande zote mbili ni muhimu kwako n unazijali...

Zingatia huu ushauri ndugu..ni mzuri!
 
Kwanza siko kwenye ndoa so sidhani kama naweza ruhusiwa changia hapa!
 
unaweza kwenda bila tatizo,ila mfahamishe mwenzio akisema twende sote sio mbaya.
 
Aendae kwao ahagi. Mimi wazazi wako Dar na kama baba ndio njia ya kwenda kwangu. Si mimi wala hubby anayesema in advance akipita kwa Mzee. Nii baba yangu lakini mume wangu mara kadhaa amekuwa akipita kumpa Hi na kunipa taharifa tu.

Unless kuna kitu hujatuambia lakini naona kama ni odd question kuuliza kama ni sawa au si sawa kwenda kwenu. Hizo ndoa si zitakuwa jela sasa

Unajua kipindi hiki cha mwanzo wa ndoa si cha kupretend. Mtajajuta kwa masheria mnayojiwekea bila kujua. Be yourselves (ila with limits ofcourse).
 
Ah .. Nimejikwaa tu.. Nilikua napitapita tu..ila.....

nijioneleavyo mimi baada ya ndoa kwako kunakuwa kwake Na kwake kunakuwa kwako.. Ila ni mpitaji tu Mie..

Ansnt
 
Hakuna formula katika hilo ila jua wewe ni kiongozi wa familia yako na ni mtoto kwa wazazi wako yet ni mkwe upande wa mkeo so yu have to strike a very fine balance hapo otherwise utaonekana a double standard man na kupoteza heshima yako.

Mawasiliano ndo uti wa mgongo wa ndoa mkuu so wasilianeni as much as possible na discuss as much as you can hata issues ambazo zinaonekana kama trivial......... kila kitu kitakaa sawa with time.....kwa imani yako muombe muumba akupe busara sana juu ya maisha ya ndoa

All best
 
mie nahisi umeoa ukiwa mdogo sana,maswala mepesi kama hayo yanakushinda kufanya maamuzi,je yakija mazito si utakufa kwa pressure?
 
Bornagain,we ndo kichwa cha nyumba mjengee mkeo mazingara kungali mapema ajue si kila unapokwenda lazima umuage.
........samaki mkunje angali mbichi......fuata ushauri wa nyumbakubwa hapo juu.
 
Mmh hvi mzaz au mke wako akiskia una0mba ushaur kitu ordinary kama hvi c utharaulika wew? Kuwa na c0nfidenc bhana aah
 
Mwanaume ndio kichwa, mke ni wakumpa taarifa tu, ukimsikiliza sana mwanamke huwezi kumkotloo mambo wanayotaka huwa ni mengi sana, mfano: sitaki ufanye urafiki na fulani, nataka ukitoka kazini uje moja kwa moja home, mimi nimechoka kuishi hapa tafuta nyumba nyingine na mengine mengi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom